Tetesi za Soka Ulaya Alhamisi: Liverpool yaongoza mbio za kumsajili Senesi

Muda wa kusoma: Dakika 3

Liverpool wanaongoza katika kinyang'anyiro cha kumnunua beki wa Bournemouth na Argentina Marcos Sensi, 28, ambaye mkataba wake unamalizika msimu huu. (i paper)

Manchester City inamfuatilia kwa karibu beki wa Feyenoord Mholanzi Givairo Read, 19, lakini Bayern Munich pia ina hamu ya kumsajili. (Sky Sports)

Liverpool inavutiwa na winga wa Newcastle Muingereza Anthony Gordon, 25, na mshambuliaji wa Everton na Senegal Iliman Ndiaye, 26, huku wakitafuta kuimarisha safu yao ya ushambuliaji msimu ujao. (Team Talk)

Aliyekuwa meneja wa Chelsea na Manchester United Jose Mourinho anaweza kuwania nafasi ya kocha wa Newcastle iwapo wataamua kumtimua Eddie Howe. (Talksports)

Bournemouth imepiga hatua katika mazungumzo ya kumsajili mkufunzi wa zamani wa Borussia Dortmund na RB Leipzig Marco Rose kuwa kocha wao mkuu. Mjerumani huyo mwenye umri wa miaka 49 akiwa hana klabu kwa sasa. (Telegraph - usajili unahitajika)

Chelsea na Newcastle ni miongoni mwa vilabu vinavyotarajiwa kumenyana kumnasa mlinzi wa Ujerumani Karim Coulibaly, 18, baada ya kuwa na msimu mzuri katika klabu ya Werder Bremen. (Bild - kwa Kijerumani)

Juventus inawafuatilia mlinda lango wa Liverpool wa Brazil Alisson, 33, na kiungo wa kati wa Manchester City na Ureno Bernardo Silva, 31, huku wakitarajia kufanyia marekebisho kikosi chao msimu wa joto. (Corriere dello Sport - kwa Kiitaliano)

Newcastle United iko tayari kuwasilisha tena dau la kumsajili Ousmane Diomande katika majira ya joto. The Magpies walionyesha nia ya kumsajili mchezaji huyo wa kimataifa wa Ivory Coast aliye na umri wa miaka 22 mwezi Januari, lakini Sporting haenda isikubali ada ya chini ya pauni milioni 40. (Football Insider)

Beki wa Como Mhispania Jacobo Ramon, 21, anavutia vilabu vingi vikiwemo Arsenal na Chelsea. (Team talk)

Arsenal iko tayari kumuuza mshambuliaji wa Brazil Gabriel Jesus, 29, na mshambuliaji wa Ujerumani Kai Havertz, 26, msimu wa joto ili kutafuta fedha za kumnunua mshambuliaji wa Atletico Madrid na Argentina Julian Alvarez, 26. (Caughtoffside)