Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za Soka Ulaya Jumatano: Manchester United inawafuatilia wachezaji wawili EPL
Manchester United inawafuatilia mshambuliaji wa Bournemouth Mfaransa Junior Kroupi, 19, na beki wa Argentina Marcos Senesi, 28. (Mail - usajili unahitajika).
Bayern Munich ina nia ya kumsajili winga wa Newcastle na England Anthony Gordon, 25. (Talksport)
Aston Villa ndio klabu ya hivi punde zaidi ya Ligi Kuu ya Uingereza kuonyesha nia ya kumsajili mlinda lango wa England James Trafford. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 alisajiliwa na Manchester City msimu uliopita wa joto lakini nafasi yake ikachukuliwa na Muitaliano Gianluigi Donnarumma, 27.(Mail)
Liverpool inamtaka Bazoumana Toure msimu wa joto. Winga huyo wa Ivory Coast mwenye umri wa miaka 20 amefanya vyema katika klabu ya Hoffenheim msimu huu na anaweza kuimarisha safu ya mashambulizi ya klabu hiyo ya Anfield. (Team talk)
Beki wa Liverpool, Ibrahima Konate anakaribia kusaini mkataba mpya wa kusalia Anfield. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 26 alitarajiwa kuondoka msimu huu wa joto lakini sasa anaweza kusaini mkataba wa miaka minne. (RMC - kwa Kifaransa)
Beki wa Borussia Dortmund na Ujerumani Nico Schlotterbeck, 26, ana kipengele cha kutolewa cha takriban £43m-£52m ambacho kinatumika kwa vilabu vitatu pekee - ikiwa ni pamoja na Liverpool na Real Madrid, lakini sio Bayern Munich. (Bild - kwa Kijerumani)
Napoli inataka kumuongezea mkataba wa kiungo wa Scotland Scott McTominay kabla ya Kombe la Dunia msimu huu wa joto. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 amekuwana mchnago mkubwa kwa Naples tangu ajiunge nao akitokea Manchester United mwaka wa 2024. (Il Mattino - Kwa Kiitaliano)
Winga wa Uingereza Jadon Sancho, 26, atalazimika kukubali kupunguziwa mishahara kwa kiasi kikubwa ikiwa anataka kujiunga tena na Borussia Dortmund mkataba wake wa Manchester United utakapokamilika msimu huu. (Mirror)
Bournemouth inamfikiria kocha wa Rayo Vallecano Inigo Perez, meneja wa Coventry City Frank Lampard na bosi wa Ipswich Town Kieran McKenna huku wakijiandaa kwa maisha bila Andoni Iraola, ambaye ameamua kuondoka mwishoni mwa msimu huu. (i Sport)