Tetesi za Soka Ulaya Jumatatu: Pulisic aingia kwenye rada ya Tottenham

Chanzo cha picha, Getty Images
Tottenham imeonyesha nia ya kumsaini Christian Pulisic baada ya kuwasiliana na AC Milan kuhusu upatikanaji wake. (Teamtalk)

Chanzo cha picha, Getty Images
Liverpool na Everton zinamwania winga wa Stuttgart Jamie Leweling, 25, huku AS Roma nayo ikiongeza juhudi za kumsajili Mjerumani huyo. (Patrick Berger, external/Sky Sport Germany)

Chanzo cha picha, Getty Images
Newcastle inaendelea kufuatilia kwa karibu uwezekano wa kumnasa mshambuliaji wa Lille Matias Fernandez-Pardo, 21, lakini hadi sasa hakuna hatua kubwa iliyopigwa katika mazungumzo ya kumsajili nyota huyo wa kimataifa wa Ubelgiji. (Florian Plettenberg)

Chanzo cha picha, Getty Images
Everton inaendelea na juhudi za kukamilisha makubaliano ya pili ya mkopo kwa ajili ya winga wa Manchester City na timu ya taifa ya England, Jack Grealish. (Athletic)

Chanzo cha picha, Getty Images
Crystal Palace imeazimia kumbakisha kipa wa England Dean Henderson, mwenye umri wa miaka 29, kufuatia ofa iliyowasilishwa na Nottingham Forest kwa ajili ya kumsajili. (Mail - subscription required)
Newcastle United, Aston Villa na Chelsea zote zinavutiwa na kumsajili mshambuliaji wa Cameroon mwenye umri wa miaka 20, Christian Kofane, kutoka Bayer Leverkusen. (Football Insider)











