Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za Soka Ulaya Jumatatu: Pulisic aingia kwenye rada ya Tottenham
Tottenham imeonyesha nia ya kumsaini Christian Pulisic baada ya kuwasiliana na AC Milan kuhusu upatikanaji wake. (Teamtalk)
Liverpool na Everton zinamwania winga wa Stuttgart Jamie Leweling, 25, huku AS Roma nayo ikiongeza juhudi za kumsajili Mjerumani huyo. (Patrick Berger, external/Sky Sport Germany)
Newcastle inaendelea kufuatilia kwa karibu uwezekano wa kumnasa mshambuliaji wa Lille Matias Fernandez-Pardo, 21, lakini hadi sasa hakuna hatua kubwa iliyopigwa katika mazungumzo ya kumsajili nyota huyo wa kimataifa wa Ubelgiji. (Florian Plettenberg)
Everton inaendelea na juhudi za kukamilisha makubaliano ya pili ya mkopo kwa ajili ya winga wa Manchester City na timu ya taifa ya England, Jack Grealish. (Athletic)
Crystal Palace imeazimia kumbakisha kipa wa England Dean Henderson, mwenye umri wa miaka 29, kufuatia ofa iliyowasilishwa na Nottingham Forest kwa ajili ya kumsajili. (Mail - subscription required)
Newcastle United, Aston Villa na Chelsea zote zinavutiwa na kumsajili mshambuliaji wa Cameroon mwenye umri wa miaka 20, Christian Kofane, kutoka Bayer Leverkusen. (Football Insider)
Crystal Palace na Fulham zinafanya mazungumzo ya kumsajili kiungo wa Eintracht Frankfurt, Hugo Larsson, 22, huku dau la takriban pauni milioni 25 likitajwa kuwa linaweza kutosha kumpata nyota huyo wa Uswidi. (Teamtalk)
Liverpool inamfuatilia kipa wa Genk Lucca Brughmans, 18, lakini iwapo makubaliano ya kumsajili yatafikiwa msimu huu wa joto, hatajiunga na klabu hiyo mara moja. Mchezaji huyo wa timu za vijana za Ubelgiji ataendelea kubaki kwa muda. (Ben Jacobs)
Crystal Palace imeanzisha upya mazungumzo na Marseille kuhusu uwezekano wa kumsajili kiungo wa Uholanzi mwenye umri wa miaka 25, Quinten Timber. (Mail - subscription required)