Tetesi za Soka Ulaya Jumapili: Sunderland bado inamuwinda Grealish Man City

Chanzo cha picha, Getty Images
Sunderland inaendelea kufuatilia uwezekano wa kumsajili kwa mkopo winga wa Manchester City, Jack Grealish. Klabu hiyo inaamini inaweza kufanikisha dili la kumpata mchezaji huyo wa kimataifa wa England mwenye umri wa miaka 30.(Football Insider)
Vilabu kadhaa vya Serie A nchini Italia vimeripotiwa kuonyesha nia ya kumsajili mshambuliaji wa Newcastle United, Nick Woltemade. Napoli inaonekana kuwa miongoni mwa vinavyoongoza katika mbio hizo, ikitajwa kuwa na nia ya kumchukua Mjerumani huyo mwenye umri wa miaka 24 kwa mkopo. (Sky Sports)
Arsenal inafuatilia kwa karibu hali ya mshambuliaji wa Lille, Matias Fernandez-Pardo. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ubelgiji mwenye umri wa miaka 21 anatajwa kuwa na thamani ya takriban pauni milioni 60. (Caught Offside)
Winga wa Crystal Palace, Ismaila Sarr, anaripotiwa kuvutiwa na uwezekano wa kuhamia Liverpool. Mazungumzo kati ya pande husika yanaendelea kuhusu uhamisho wa mchezaji huyo wa kimataifa wa Senegal mwenye umri wa miaka 28.(Sun)
Sunderland pia inatafakari uwezekano wa kumsajili mshambuliaji wa Levante, Karl Etta Eyong. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 ana kipengele katika mkataba wake kinachoruhusu kuondoka kwa ada inayokadiriwa kufikia pauni milioni 26. (Sun)
Fiorentina imeanzisha mawasiliano na Leeds United kuhusu uwezekano wa kumsajili winga wa Italia Wilfried Gnonto, mwenye umri wa miaka 22.

Chanzo cha picha, Getty Images
Sunderland iko karibu kufikia makubaliano ya ada ya uhamisho kwa ajili ya winga wa Marseille, Igor Paixao, ingawa klabu hiyo ya Ligue 1 bado inafanya juhudi za kumbakiza Mbrazili huyo mwenye umri wa miaka 26.
Aston Villa imeripotiwa kuwasilisha ofa kwa Manchester United kwa ajili ya mshambuliaji wa Ivory Coast, Amad Diallo, mwenye umri wa miaka 24.
Wakati huo huo, kocha wa Hull City Sergej Jakirovic ameshauri klabu hiyo kutomruhusu Ryan Giles kujiunga na Burnley kwa mkopo, licha ya pande husika kufikia makubaliano kuhusu mchezaji huyo wa nafasi ya beki wa kushoto.
Nayo AC Milan imefikia makubaliano na Nottingham Forest kwa ajili ya usajili wa winga wa England mwenye umri wa miaka 22, Omari Hutchinson.
Imetafsiriwa na Ambia Hirsi












