Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za soka Ulaya: Arsenal, Chelsea zinamfukuzia Bergvall
Kiungo wa Sweden wa Tottenham Hotspur, Lucas Bergvall (20), anafuatiliwa na klabu kadhaa, huku Arsenal na Chelsea zikionesha nia ya kumsajili. (Caught Offside)
Mshauri wa michezo wa Paris Saint-Germain, Luis Campos, amefanya mazungumzo na wawakilishi wa mshambuliaji wa Brazil wa Arsenal, Gabriel Martinelli (24), pamoja na winga wa Ivory Coast anayechezea RB Leipzig, Yan Diomande (19). (L'Equipe)
AFC Bournemouth wako tayari kumuuza mshambuliaji wa Ufaransa Eli Junior Kroupi (19), anayehitajika na Manchester United, kwa zaidi ya pauni milioni 50. (Football Insider)
Kocha wa Aston Villa, Unai Emery, yupo kwenye 'rada' za Manchester United na Real Madrid, ingawa Villa wana matumaini ya kumbakiza. (Teamtalk)
Beki wa Czech wa Wolverhampton Wanderers, Ladislav Krejci (27), anahitajika na Leeds United. (Express & Star)
Southampton wana imani ya kumbakiza winga wa Brazil Leo Scienza (27), licha ya kuskwa na Leeds United. (Football Insider)
Wakala wa mshambuliaji wa Poland wa FC Barcelona, Robert Lewandowski (37), anatarajiwa kukutana na Juventus wiki hii, huku AC Milan pia wakionesha nia. (La Gazzetta dello Sport)
Beki Mdenmark wa FC Barcelona, Andreas Christensen (30), amekataa ofa ya mkataba mpya lakini bado anataka kubaki klabuni. (Mundo Deportivo)