Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za soka Ulaya: Bayern, Arsenal 'zatoana roho' kwa Anthony Gordon
Bayern Munich wameonyesha nia ya kumsajili mshambuliaji wa Newcastle United na England, Anthony Gordon, mwenye miaka 25, ambaye pia anafuatiliwa na Arsenal (Caughtoffside).
Manchester United wanatarajia kutumia uhusiano ulioko ndani ya kikosi cha England kuwazidi kete Manchester City katika mbio za kumsajili kiungo wa Nottingham Forest, Elliot Anderson, mwenye miaka 23 (Teamtalk).
Liverpool wanamfuatilia winga wa Brighton & Hove Albion na Gambia, Yankuba Minteh, mwenye miaka 21, aliyewahi kufanya kazi chini ya Arne Slot huko Feyenoord, kama mbadala wa mshambuliaji wa Misri, Mohamed Salah, anayeondoka mwishoni mwa msimu (Mirror).
Arsenal na Manchester City wameungana na Aston Villa katika mbio za kumsajili beki wa Real Betis, Oscar Mingueza, mwenye miaka 26 (Teamtalk).
Aston Villa na Leeds United pia wanamgombania beki wa Union Berlin, Danilho Doekhi, mwenye miaka 27, ambaye pia anafuatiliwa na Besiktas (Inside Futbol).
Tottenham Hotspur wanamfuatilia kiungo wa RB Leipzig, Arthur Vermeeren, mwenye miaka 21, ambaye aliwahi kufanya kazi chini ya Roberto De Zerbi akiwa kwa mkopo Marseille (Caughtoffside).
Real Madrid bado wanaweza kumsajili beki wa Borussia Dortmund, Nico Schlotterbeck, mwenye miaka 26, licha ya mchezaji huyo kusaini mkataba mpya na klabu hiyo ya Bundesliga (Goal.com).