Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za Soka Ulaya: Arsenal, Man United na Chelsea vitani kumwania Rogers
Kiungo wa Aston Villa na timu ya taifa ya England, Morgan Rogers, anatarajiwa kuwa kitovu cha vita kubwa ya usajili katika majira haya ya kiangazi, baada ya Arsenal, Manchester United na Chelsea kuonyesha tena nia ya kumtaka mchezaji huyo mwenye miaka 23 (Times).
Bayern Munich pia wanavutiwa na Rogers na wanaweza kushindana na klabu za Ligi Kuu England kumsajili (Mirror).
Juventus wana matumaini makubwa ya kumsajili kipa wa Brazil Alisson Becker kutoka Liverpool, huku mchezaji huyo mwenye miaka 33 akiripotiwa kuwa tayari kuhamia Serie A (La Gazzetta dello Sport).
Wamiliki wa Liverpool, Fenway Sports Group, wanaamini kuwa kocha Mholanzi Arne Slot ataendelea kuiongoza timu hiyo msimu ujao licha ya timu hiyo kupokea kipigo kingine wiki hii (Telegraph).
Aston Villa ni miongoni mwa vilabu vinavyotarajiwa kuwania saini ya kipa wa Manchester City na England, James Trafford, mwenye miaka 23 (Football Insider).
Enzo Fernandez aomba radhi Chelsea
Enzo Fernandez pamoja na wakala wake wameiomba radhi Chelsea kufuatia kauli alizotoa kiungo huyo mwenye miaka 25 akiwa kwenye majukumu ya timu ya taifa Argentina kuhusu uwezekano wa kuhamia Real Madrid (Sky Sports).
Real Madrid wanafikiria kuongeza juhudi za kumsajili winga wa Bayern Munich na Ufaransa, Michael Olise, mwenye miaka 24, ambaye pia anawindwa na Liverpool (Christian Falk).
Liverpool na Manchester City wameungana na Arsenal katika mbio za kumsajili mshambuliaji mwenye miaka 19 wa Bayer Leverkusen na Cameroon, Christian Kofane (Teamtalk).
Nottingham Forest bado hawajapokea ofa rasmi kwa ajili ya kiungo wa England Elliot Anderson, mwenye miaka 23, lakini wanatarajia kupokea ofa hiyo kabla ya kuanza kwa fainali za Kombe la dunia 2026, huku Manchester City na Manchester United zikionyesha nia ya kumsajili (Talksport).
Klabu ya RB Leipzig na beki Castello Lukeba wamekubaliana kuwa mchezaji huyo ataondoka majira haya ya kiangazi, huku Arsenal, Chelsea, Liverpool na Manchester United zikimfuatilia kwa karibu (Teamtalk).