Moja kwa moja, Marekani yachukua udhibiti wa mapipa ya mafuta nchini Venezuela
Rais wa Marekani Donald Trump, ametangaza kuwa Marekani imefikia makubaliano na Venezuela ya kudhibiti zaidi ya mapipa bilioni 65 ya mafuta nchini humo.
Marekani yachukua udhibiti wa mapipa ya mafuta ya Venezuela
Moja kwa moja
Na Beldeen Waliaula
Watu 27 wafariki katika shambulio la Urusi mjini Kyiv
Chanzo cha picha, Reuters
Takriban watu 27 wameuawa baada ya shambulio la ndege isiyo na rubani ya Urusi kushambulia ghala moja mjini Kyiv, nchini Ukraine.
Watu wengine 42 wamejeruhiwa, huku zaidi ya 380 wakihamishwa kutoka eneo lililoshambuliwa katika wilaya ya Bucha.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema kuwa shambulio hilo dhidi ya ghala lilisababisha mlipuko, huku miundombinu iliyoko karibu ikiharibiwa, ikiwemo majengo ya makazi ya watu na kituo kinachotoa huduma ya uangalizi kwa wazee.
Zaidi ya watu 600 wameaga dunia kutokana na mafuriko yaliyotokea Nepal - Tibet
Chanzo cha picha, Reuters
Operesheni
ya kuwatafuta manusura wa mafuriko
nchini Nepal, imeingia siku ya nne baada ya mafuriko hayo kusababisha maafa katika mpaka wa Nepal na Tibet
siku ya Jumatano.
Idadi
ya waliofariki nchini Nepal imeongezeka na kufikia watu 626,
kwa mujibu wa mamlaka za taifa hilo.
Watu
2,426
wanaripotiwa kutojulikana walipo.
Katika eneo la Tibet,
idadi rasmi ya waliofariki imefikia saba,
huku watu 554
wakiripotiwa kutojulikana walipo kwa mujibu
wa vyombo vya habari vya serikali ya China.
Kupata
taarifa kutoka Tibet imekuwa vigumu, lakini China sasa imetoa baadhi ya picha
za tukio hilo.
Nchini
Nepal, angalau raia 517 wa kigeni wameripotiwa kutoweka, wakiwemo
mahujaji na watalii waliokuwa wakifanya safari za milimani.
Waziri
wa Fedha wa Nepal amekadiria kuwa nchi hiyo itahitaji kati ya dola bilioni
4 au 5, kwa ajili ya kujenga upya taifa hilo baada ya mafuriko hayo makubwa.
“Haya ni
makadirio tu. Tathmini ya hasara na uharibifu bado inaendelea,”
Swarnim Wagle aliiambia shirika la habari la Reuters.
Niger: Uwanja mkuu wa ndege walengwa huku milio ya risasi ikiripotiwa mjini Niamey
Chanzo cha picha, Getty Images
Milio
ya risasi na milipuko imeripotiwa katika maeneo kadhaa ya mji mkuu wa Niger,
Niamey, karibu na uwanja wa ndege wa kimataifa, na kambi ya kijeshi iliyo karibu na
ikulu ya rais.
Chanzo kimoja kimeiambia shirika la habari la Reuters
kwamba washambuliaji walilenga Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Diori Hamani na
kujaribu kuvuka ukuta unaozunguka
ikulu ya rais.
Inasemekana vikosi vya
usalama vimefanikiwa kurejesha udhibiti wa Kambi ya Anga ya 101, iliyoko karibu
na uwanja wa ndege, ingawa taarifa hiyo haijathibitishwa.
Serikali ya Niger bado haijatoa taarifa
yoyote kuhusu tukio hilo, na hakuna kundi ambalo limedai
kuhusika na shambulio hilo. Bado haijulikani ni nani waliotekeleza shambulio hilo
au iwapo kuna watu waliojeruhiwa au kuuawa.
Uwanja
huo wa ndege na maeneo ya kijeshi yaliyo karibu, tayari yamelengwa mara mbili
mwaka huu na makundi yenye
itikadi kali.
Wanamgambo
wa Islamic State walishambulia eneo hilo mwezi Januari, huku kundi la JNIM
lenye uhusiano na al-Qaeda likitekeleza shambulio jingine mwezi Juni.
Jeshi
lilichukua mamlaka nchini Niger mwaka wa 2023, na kuipundua serikali ya kiraia iliyokuwepo, na kuahidi kukabiliana na uasi ambao ulikuwa umeongezeka nchini humo.
Mamlaka
za kijeshi nchini Niger zimewataka wananchi katika mji mkuu, Niamey, kuwa watulivu baada ya milio ya
risasi na milipuko kuripotiwa katika maeneo kadhaa ya mji huo.
Ndejembi aapishwa rasmi kuwa Makamu mpya wa Rais nchini Tanzania
Chanzo cha picha, URT
Deogratius John Ndejembi,ameapishwa rasmi kuwa Makamu mpya wa rais nchini Tanzania, baada ya kujiuzulu kwa aliyekuwa Makamu wa Rais Emmanuel Nchimbi.
"Usiwe samaki, mwanetu nenda ukakue, tumekupa majukumu makubwa na ni imani yangu utaweza" alisema Rais Samia Suluhu akimpongeza makamu huyo mpya.
Hafla hiyo ya uapisho imefanyika katika ikulu ya Chamwino, Dodoma.
Ndejembi mwenye umri wa miaka 43, atakuwa Makamu wa rais wa 13 tangu Tanzania ipate uhuru, akiwa miongoni mwa Makamu wa rais vijana zaidi kuwahi kushika nafasi hiyo.
Iran yalaani vikwazo vya kiuchumi vya Marekani, huku uchumi wa taifa hilo ukiendelea kudorora
Chanzo cha picha, Getty Images
Iran
imelaani vikwazo vipya vya kiuchumi villivyotangazwa na Marekani, ikiviita 'ugaidi dhidi ya serikali yake' huku Kiongozi Mkuu wa Iran akipiga marufuku vitendo vyovyote vinavyoweza kuathiri 'mshikamano
wa kijamii.'
Kuna hofu kuwa kuongezeka
kwa changamoto za kifedha kunaweza kusababisha
machafuko nchini humo.
Vita vya Marekani na Iran sasa vimetimiza
miezi sita, huku mazungumzo ya
kutafuta suluhu yakiwa yamekwama.
Utawala
wa Rais Donald Trump umeongeza
juhudi za kuiadhibu Iran kifedha kupitia mpango uliouita “ Economic D-Day.”
Vikwazo hivyo vinaongeza madhara ya vita kwa uchumi wa Iran, ambako mfumuko wa
bei umefikia asilimia 66 mwezi uliopita.
Washington
imeonya nchi mbalimbali zipunguze uhusiano wao wa kibiashara na Iran au
zikabiliwe na vikwazo vya kiuchumi,
ingawa Wizara ya Fedha ya
Marekani bado haijatekeleza
adhabu hizo.
Wizara
ya Mambo ya Kigeni ya Iran imesema katika taarifa iliyotolewa hapo jana kuwa nchi zote zina wajibu chini ya
sheria za kimataifa kukataa kutekeleza vikwazo vya Marekani dhidi ya Tehran.
Iran
imetaja hatua mpya za Marekani kuwa “uhalifu dhidi ya ubinadamu”, ikisema zinaweka
afya na maisha ya mamilioni ya raia katika hatari kubwa.
Marekani yachukuckua udhibiti wa mafuta ya Venezuela
Chanzo cha picha, Getty Images
Rais wa Marekani Donald Trump, ametangaza
kuwa Marekani imefikia makubaliano na Venezuela ya kudhibiti zaidi ya
mapipa bilioni 65 ya mafuta nchini humo.
“Makubaliano haya ya kihistoria yatazidisha
zaidi ya mara mbili akiba ya mafuta ya Marekani,
utaongeza kwa kiasi kikubwa
usambazaji wetu wa mafuta na kupunguza
bei ya petroli kwa Wamarekani wote,” Trump aliandika kwenye mitandao ya
kijamii.
Rais
wa mpito wa Venezuela, Delcy Rodriguez, amepongeza makubaliano hayo, akisema
yatasaidia kufufua uchumi wa taifa lake.
Trump
alikuwa ameahidi kutumia akiba ya mafuta ya
Venezuela, ambayo ni kubwa zaidi duniani, baada ya Marekani kumkamata rais wa taifa hilo Nicolás Maduro, mapema mwaka huu.
Hivi
karibuni, Trump amekuwa akikabiliwa na shinikizo la kupunguza bei za mafuta
nchini Marekani, ambazo zimepanda
kutokana na mzozo wa Iran.
Waziri
wa Mambo ya Kigeni wa Marekani, Marco Rubio, alitaja
makubaliano hayo ya mafuta kuwa “ushindi mkubwa kwa wananchi wa Marekani na Venezuela.”
Hata hivyo, maelezo machache kuhusu makubaliano hayo yametolewa.
“Kwa
wananchi wa Venezuela, makubaliano haya yataleta karibu dola bilioni 100 za
uwekezaji kutoka sekta binafsi, na
kutengeneza ajira zenye mishahara
mizuri na kuimarisha uchumi wa
Venezuela,” Rubio alichapisha
kwenye mitandao ya kijamii.
Maelezo zaidi kuhusu makubaliano hayo hayajatolewa.
Trump alidai kuwa makubaliano hayo yalifikiwa “bila gharama yoyote kwa walipa
kodi wa Marekani.”