Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.

Bofya kuelekea tovuti kuu

Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data

Moja kwa moja, Wanaanga wa Artemis II watua salama baada ya kukamilisha safari ya kihistoria mwezini

Nasa imesifia mbinu iliyotumiwa na wanaanga hao wanne kutu katika bahari ya Pacific baada ya kusafiri umbali ambao haujawawahi kufikiwa na binadamu yeyote.

Muhtasari

Moja kwa moja

Na Ambia Hirsi

  1. Katika picha: Hali ilivyo mjini Islamabad

    Usalama umeimarishwa katika mji mkuu wa Pakistan, Islamabadtaifa hilo likijiandaa kwa mazungumzo kati ya Marekani na Iran baadaye leo.

    Tayari wajumbe wa pande zote mbili wamesili mjini humo.

    Hiz hapa mkusanyiko wa picha zinazoonyesha hali ilivyo.

  2. Rais wa Djibouti Guelleh ashinda muhula wa sita madarakani

    Rais wa Djibouti Ismail Omar Guelleh ameshinda uchaguzi uliosusiwa na upinzani, baada ya kupata zaidi ya asilimia 97.81 ya kura zilizopigwa, data rasmi kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani Jumamosi ilionyesha.

    Kura ya Ijumaa ilimkutanisha mpinzani mmoja pekee na aliyemaliza muda wake, Mohamed Farah Samatar. Takwimu za Wizara ya Mambo ya Ndani zilionyesha kuwa aliibuka wa pili kwa 2.19% ya kura 168,233 zilizopigwa.

    Guelleh alishinda uchaguzi uliopita wa 2021, ambao pia uliosusiwa na wagombea wengi wa upinzani, kwa zaidi ya 97% ya kura.

    Alikuwa ametangaza kujiuzulu mwaka huu, lakini marekebisho ya katiba mwezi Novemba yaliondoa ukomo wa umri wa juu wa miaka 75 kwa wagombea urais.

    Wakosoaji wamepuuza matokeo ya uchaguzi huo wakisema haukua na ushindani, huku wafuasi wakihoji kuwa kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 78 ameleta utulivu katika taifa hilo la kimkakati la Pembe ya Afrika.

    Mpinzani maarufu Daher Ahmed aliiambia BBC kwamba wanasusia uchaguzi nchini Djibouti kwa sababu hawaruhusiwi kuwa na uchaguzi huru na wa haki, jambo ambalo wanaamini linadhoofisha mchakato wa kidemokrasia na uhalali wa matokeo ya uchaguzi.

    Kampeni ya Rais Ismail Omar Gelleh ilijikita zaidi katika kuleta utulivu huku kukiwa na mvutano wa kikanda, hasa unaohusishwa na migogoro katika Mashariki ya Kati, wakati Samatar amejikita katika mageuzi ya kiuchumi na elimu.

    Rais huyo amekuwa madarakani tangu mwaka 1999 na ndiye rais wa pili wa nchi hiyo tangu ilipojipatia uhuru wake kutoka kwa Ufaransa mwaka 1977.

  3. Guterres atoa wito kwa Iran na Marekani kufanya mazungumzo kwa 'nia njema''

    Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres anakaribisha mazungumzo ya amani ya Marekani na Iran yaliyopangwa na kuzitaka pande zote mbili kuingia katika mazungumzo hayo kwa "nia njema".

    Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari wa Umoja wa Mataifa siku ya Ijumaa, msemaji wa katibu mkuu Stephane Dujarric alisema Guterres "anatoa wito kwa wahusika kuchangamkia fursa hii ya kidiplomasia kushiriki mazungumzo kwa nia njema kuelekea makubaliano ya kudumu."

    "Katibu Mkuu anasisitiza kwamba hakuna njia mbadala inayofaa kwa utatuzi wa mizozo ya kimataifa, kwa mujibu wa sheria za kimataifa, ikiwa ni pamoja na Mkataba wa Umoja wa Mataifa," Dujarric alisema.

    Mjumbe binafsi wa Guterres yuko katika eneo hilo kusaidia juhudi za kidiplomasia, aliongeza.

    Soma zaidi:

  4. Makamu wa Rais wa Marekani Vance awasili Pakistan kwa mazungumzo ya amani

    Makamu wa Rais wa Marekani JD Vance amewasili mjini Islamabad muda pamoja na ujumbe wa Marekani, chanzo cha usafiri wa anga kimeiambia BBC.

    Anatarajiwa kuhudhuria mazungumzo na Iran baadaye leo, pamoja na mjumbe maalum Steve Witkoff na Jared Kushner.

    Vance na timu yake ya wapatanishi waliondoka Marekani kuelekea Pakistan jana, na kabla hajaondoka, makamu wa rais aliwaambia waandishi wa habari kuwa "anatazamia mazungumzo yenye tija", lakini akaonya Iran "isijaribu kuichezea" Marekani kwania haitakubali.

    Wakati huo huo Waziri wa Mambo ya Nje wa Pakistani Mohammad Ishaq Dar amepongeza dhamira ya Marekani ya kufikia amani ya kudumu ya kikanda na kimataifa alipompokea JD Vance mjini Islamabad.

    Katika taarifa iliyotolewa na wizara ya mambo ya nje ya nchi hiyo, Dar imenukuliwa ikisema anatumai Iran na Marekani "zitajadiliana kwa amani, na kusisitiza hamu ya Pakistan ya kuwezesha pande husika kufikia suluhisho la kudumu la mzozo huo".

    Tutakufahamisha yote yatakayojiri nchini Pakistan. Endelea nasi.

    Pia unaweza kusoma:

  5. Katika Picha: Jinsi wanaanga wa Artemis II walivyorejea duniani

    Shirika la anga la Marekani NASA limetoa picha za wanaanga wakirejea duniani kwa chombo cha Orion.

    Picha zinaonyesha msururu wa matukio kutoka walipotua kwa myavuli kwenye bahari ya Pacific hadi walipotembeakuelekea kwenye ndege ya USS John P Murtha iliyokuwa ikisubiri kuwapeleja katika kituo cha matibabu ili kufanyiwa uchunguzi wa kiafya.

  6. Wanaanga wa Artemis II waatua salama baada ya kukamilisha safari ya kihistoria mwezini

    Kikosi cha wanaanga wa Artemis II kimerejea salama duniani baada ya kukamilisha safari yao kihistoria mwezini.

    NASA ilitoa picha nzuri zilizopigwa kutoka upande wa mbali wa Mwezi wakati wa misheni hiyo.

    Mojawapo ya kuvutia zaidi ni picha hii, ambayo Nasa imeiita Earthset.

    Inaonyesha Dunia ikiwa nyuma ya upeo wa Mwezi - picha maarufu ya Earthrise iliyopigwa wakati wa misheni ya Apollo 8.

    Picha nyingine inaonyesha Mwezi ukilifunika Jua. Wanaanga walipata fursa ya kipekee ya kujionea tukio hilo kwa karibu dakika 54 walipokuwa wakipita nyuma ya Mwezi.

    Kutoka ndani ya chombo cha Orion wanaanga waliweza kuona Dunia inayokaa kama mwezi mwandamo ikiongezeka kwa ukubwa polepole nyuma yao walipokuwa wakiendelea na safari yao ya nje ya maili 250,000 (400,000km).

    Kufikia umbali huo kutoka duniani hadi Mwezini kungewachukua siku nne.

    Hakuna mtu ambaye ameenda mbali sana na dunia, isipokuwa wanaanga wa Artemis II

    Maelezo zaidi:

  7. Natumai hujambo.