Mazungumzo yanaweza kufutwa ikiwa masharti ya Tehran hayatatimizwa - ripoti
Mwandishi kituo cha habari cha serikali ya Iran IRINN ambaye anaripoti moja kwa moja kutoka Islamabad ameonya kwamba mazungumzo huenda yakafutwa ikiwa masharti ya Iran hayatazingatiwa.
Alisema kujiondoa kwenye mazungumzo ambayo hayaheshimu "maslahi na matakwa " ya Iran kunaweza kutazamwa kama "mafanikio" kwa kile maafisa wanachokielezea kama "diplomasia ya uthubutu".
Mapema asubuhi ya leo, mwandishi huyo pia alisema wajumbe wa Iran walitarajiwa kukutana na Waziri Mkuu wa Pakistani Shehbaz Sharif kwanza, ambapo maelezo zaidi - ikiwa ni pamoja na muda wa mazungumzo yoyote na ujumbe wa Marekani - yanaweza kuwekwa wazi.
Ripoti zinasema kuwa Iran inaweza kuendelea mbele bila mazungumzo ikiwa masharti yake hayatatekelezwa.














