Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Kwa nini Einstein hakutaka kuwa Rais wa Israel?
Chaim Weizmann, mtaalam wa biokemia ambaye alizaliwa nchini Urusi, na baadaye kuwa raia wa Uingereza, alikuwa maarufu kutokana na uvumbuzi wake wa bidhaa aina ya acetylene, ambayo ilikuwa muhimu kwa silaha za kijeshi mwaka wa 1910.
Bidhaa hiyo ilitumika kuzalisha Cordite, kilipuzi ambacho kilitumika sana kipindi cha vita vya kwanza vya dunia.
Ila Weizmann alikuwa na safari ya kushangaza kisiasa.
Alikuwa miongoni mwa waanzislishi ya hamasisho la kizayuni, harakati ilioanzishwa Karne ya 19 ambayo ilianzisha taifa la wayahudi na wapalestina.
Mwaka wa 1947, baada ya kuuawa kwa wayahudi wengi, baraza kuu la umoja wa mataifa, iliidhinisha kugawanywa kwa eneo la Palestina kuwa maeneo mawili, ya wayahudi na waarabu.
Israel ilijitangaza kuwa taifa huru mwaka wa 1948, ila Wapalestina kufikia sasa hawana taifa huru, ingawa sasa inatambuliwa kuwa taifa na Zaidi ya nchi 140.
Mwaka wa 1949, Chaim Weizmann alichaguliwa kuwa rais wa taifa hilo kutokana na harakati zake za kuwapigania wazayuni.
Wadhfa wake haukuwa wa kutekeleza majukumu ya serikali, kwani katiba ya Israel inamtambua Waziri mkuu kama kiongozi wa taifa.
Weizmann alifariki mwaka wa 1952 akiwa na umri wa miaka 77.
Waziri mkuu wa taifa hilo wakati huo David Ben Gurion, aliwaalika wanasayansi kuchukua nafasi hiyo ya urais, na wakamlenga mwanasayansi maarufu duniani.
Kutumiwa mwaliko na kukataa
Abba Eban, balozi wa Israel nchini Marekani, alimtafuta Albert Einstein.
Mwanafizikia huyo raia wa Ujerumani alikuwa akiishi Marekani tangu mwaka wa 1933, mwaka ambao Adolf Hitler aliingia madarakani na mateso dhidi ya Wayahudi nchini Ujerumani yakaanza.
Abba Eban alimwandikia Einstein barua kwa niaba ya Ben-Gurion.
"Israel ni nchi ndogo kieneo, lakini inaweza kufikia ukuu kwa sababu inabeba urithi wa juu wa kiroho na akili za kale za wayahudi."
Abba Eban pia alisisitiza kwamba Einstein hangelazimika kuacha kazi yake ya kisayansi. Hata hivyo, angelazimika kuondoka New Jersey nchini Marekani, ambako aliishi na kufanya kazi ya utafiti, na kwenda Israel.
Einstein alikuwa na umri wa miaka 73 wakati huo. Hakuamini pendekezo hilo. Alijibu kwa heshima, akieleza kufurahishwa na mwaliko huo, lakini hakuwa tayari kuchukua wadhfa huo.
"Nimeguswa sana na ombi ya serikali ya Israel, na wakati huohuo ninahuzunika na kuona aibu kwamba siwezi kuikubali."Alijibu Eisten
"Nimejihusisha maisha yangu yote na mambo ya kisayansi, hivyo sina kipaji cha asili wala uzoefu unaohitajika kutekeleza majukumu rasmi. Kwa sababu hizi pekee, sihitimu kutekeleza majukumu ya cheo kama hicho." Aliongezea Einsten.
Kulingana na Alice Calapris, mwandishi wa vitabu kadhaa kuhusu Einstein, Ben-Gurion alifarijika baada ya Einstein kukataa mwaliko huo.
Einsten na Israel
Hii haikumaanisha kwamba Albert Einstein alikuwa hajali mwelekeo wa kisiasa wa Israel.
"Einstein alikuwa mwanachama wa harakati ya Kizayuni," anasema Michel German, mwanahistoria na profesa katika
Mwisho wa mwaka wa 1948, yeye na wasomi wengine wa Kiyahudi waliandika barua ya wazi kwa New York Times wakikosoa ziara ya mwanasiasa wa Israel Menachem Begin nchini Marekani.
Menachem Begin, kiongozi wa Irgun, alikuwa kiongozi wa kikundi cha kijeshi cha Kizayuni kilichotekeleza "mashambulizi ya kigaidi" dhidi ya Wapalestina na Waingereza kabla ya kuundwa kwa Israel. Mwaka huo, Irgun ilitekeleza mauaji katika kijiji cha Deir Yassin karibu na Jerusalem, na kuua zaidi ya raia mia moja wa Kipalestina, wakiwemo wanaume, wanawake, na watoto.
Mwaka 2024, baadhi ya watumiaji wa mitandao ya kijamii nchini Brazil waliirejelea barua hiyo baada ya Rais wa Brazil, Luiz Inácio Lula da Silva, kulinganisha hatua za Israel katika Ukanda wa Gaza na Maangamizi ya Wayahudi .
Iwapo kauli hizi zitatolewa bila kuzingatia muktadha, zinaweza kuibua hisia kwamba Einstein alikuwa mpinzani wa Israel.
Mwanahistoria wa Uingereza Richard Crockett anahitimisha katika kitabu chake Einstein and Twentieth-Century Politics: "Einstein ameoneshwa kama mkosoaji na pia kama mtetezi wa Uzayuni na Taifa la Israel"
Huyu ndiye Einstein huyo huyo ambaye alialikwa kugombea urais wa Israel mwaka 1952.
"Einstein alialikwa si tu kwa sababu alikuwa Myahudi, bali pia kwa sababu ya uhusiano wake wa kisiasa na harakati ya Kizayuni na uungaji wake mkono kuanzishwa kwa Israel," anaeleza.
"Wayahudi wengine mashuhuri pia wamealikwa mara nyingi kushika nyadhifa tofauti kwa lengo la kuboresha taswira ya nchi hiyo."
Kwa mfano, mwanzoni mwa miaka ya 1990, Waziri Mkuu wa wakati huo Shimon Peres alipendekeza mwandishi mashuhuri Amos Oz aingie katika siasa.
Mwaka 1952, harakati ya Brit Shalom, kundi la wasomi wa Kizayuni ambalo Einstein alikuwa mwanachama wake, lilikuwa na msimamo wa wachache, lakini msimamo huo haukuwa peke yake au kutengwa na harakati nyingine.
Wanachama wake walijumuisha wasomi mashuhuri kama Hannah Arendt, Martin Buber, na Gershom Scholem. Baadhi ya wanachama wa Brit Shalom walikuwa miongoni mwa waanzilishi wa Chuo Kikuu cha Kiebrania cha Jerusalem.
Lakini leo, kwa mujibu wa Crockett, wanachama wa kundi hili huonekana kama "wasaliti" na serikali ya sasa ya Israel, kwa sababu serikali ya Benjamin Netanyahu haitoa nafasi kwa mitazamo tofauti kuwepo, ikiwemo kupatikana kwa suluhisho la mataifa hayo mawili, palestina na Israel.