Tetesi za soka Ulaya Jumamosi: Mohamed Salah azikatisha tamaa klabu za Saudia - kunani?

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mohamed Salah
Iliyochapishwa
Muda wa kusoma: Dakika 2

Mshambuliaji wa zamani wa Liverpool, Mohamed Salah, mwenye umri wa miaka 34, huenda akajiondoa kwenye uwezekano wa kuhamia Ligi ya Saudi Pro kutokana na klabu kusita kukubali madai yake makubwa ya kifedha. (Sun)

Bayern Munich imeiambia Real Madrid kusahau kuhusu kumsajili mshambuliaji wao raia wa Ufaransa, Michael Olise, mwenye umri wa miaka 24, ambaye hauzwi katika dirisha hili la usajili la majira ya joto. (Marca)

Mshambuliaji wa Borussia Dortmund na Ujerumani, Karim Adeyemi, mwenye umri wa miaka 24, anaelekea Barcelona kwa dili la thamani ya euro milioni 31 (pauni milioni 26). (Bild - in Germany)

Arsenal na Liverpool zinachuana kumsajili beki wa RB Leipzig na Uholanzi, Lutsharel Geertruida, mwenye umri wa miaka 25, ambaye alicheza kwa mkopo Sunderland msimu uliopita. (Caughtoffside)

Manchester City na Tottenham zinamtaka winga wa Ureno, Francisco Trincao, mwenye umri wa miaka 26, na huenda zikaingilia kati uhamisho wake wa euro milioni 50 (pauni milioni 42.6) kwenda klabu ya Saudi Arabia, Al-Ahli, akitokea Sporting. (Record via Sport Witness)

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Michael Oliseh

Barcelona inatarajiwa kuongeza kasi ya kumsajili mshambuliaji wa Atletico Madrid na Argentina, Julian Alvarez, mwenye umri wa miaka 26, baada ya Kombe la Dunia la majira haya ya joto, kwa ofa ya euro milioni 130 (pauni milioni 110). (Sport - in Spanish)

Hull City imeweka ofa kwa kiungo wa Mjallby na nyota wa Kombe la Dunia wa Sweden, Elliot Stroud, mwenye umri wa miaka 24. (Expressen - In Swede)

Manchester United inatafakari uwezekano wa kusajili viungo wengine wawili baada ya kukamilisha dili la kiungo wa Chelsea na Brazil, Andrey Santos, mwenye umri wa miaka 22. (Football Insider)

Beki wa kati wa Ugiriki, Konstantinos Mavropanos, mwenye umri wa miaka 28, anavutia hisia za klabu kadhaa za Ligi Kuu ya England na klabu nyingine barani Ulaya kufuatia kiwango chake bora binafsi akiwa na West Ham, timu iliyoshuka daraja. (Sky Sports)

Como inatumai kumsajili beki wa Colombia, Davison Sanchez, mwenye umri wa miaka 30, lakini huenda ikakatishwa tamaa na bei ya euro milioni 30 (pauni milioni 25.6) inayotakiwa na Galatasaray. (La Gazzetta dello Sport - In Italy)

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mavrapanos
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Manchester United inamtafuta mlinda lango atakayetoa ushindani kwa Mbelgiji Senne Lammens, mwenye umri wa miaka 24, na huenda ikamgeukia Mparaguay Orlando Gill, mwenye umri wa miaka 26; inafahamika kuwa ana kipengele cha kuondoka kwa ada ya pauni milioni 5.2 kutoka klabu ya Argentina ya San Lorenzo. (Manchester Evening News)

Matumaini ya Newcastle United kumsajili mlinda lango wa England James Trafford, mwenye umri wa miaka 23, kutoka Manchester City yameongezeka huku Aston Villa - ambayo ingeweza kuwa mshindani katika kumsajili - ikionyesha nia ya kumbakiza kipa wake namba moja, Margentina Emiliano Martinez mwenye umri wa miaka 33. Hata hivyo, Chelsea nayo ina nia ya kumsajili. (Chronicle)

Kocha mpya wa Benfica, Marco Silva, anataka kumsajili kiungo wake wa zamani wa Fulham, Joao Palhinha, mwenye umri wa miaka 31, na ofa ya euro milioni 25 (pauni milioni 21.3) tayari inaandaliwa ili kumnasa mchezaji huyo wa kimataifa wa Ureno kutoka Bayern Munich kufuatia kipindi chake cha mkopo huko Tottenham msimu uliopita. (Record - In Portuguese)