Zawadi 6 'walizokomba' Arsenal baada ya kutwaa ubingwa wa EPL

Iliyochapishwa
Muda wa kusoma: Dakika 4

Arsenal wameandika historia mpya baada ya kutwaa ubingwa wa Ligi kuu ya England msimu wa 2025/26, wakimaliza ukame wa miaka 22 bila taji la ligi. Ubingwa huu umeambatana na heshima, zawadi na mafanikio makubwa ndani na nje ya uwanja.

Ushindi huu umeweka Arsenal tena kileleni mwa soka la England baada ya ushindani mkali dhidi ya vigogo wengine wa ligi hasa Manchester City.

Mashabiki wa Arsenal duniani kote wamefanya sherehe kubwa baada ya taji hilo kuthibitishwa rasmi. Hii ni mara ya kwanza kwa klabu hiyo kushinda ligi baada ya miaka mingi ya kusubiri na kukosa mafanikio ya juu.

Ushindi huo pia umefungua milango ya zawadi mbalimbali za kimichezo na kifedha ambazo huambatana na ubingwa wa EPL, lakini za dhahiri ni hizi sita.

1. Kombe la ubingwa wa EPL

Arsenal wamekabidhiwa rasmi kmbe EPL, lenye utepe wa rangi za klabu yao. Kombe hilo ndilo alama kuu ya ubingwa wa ligi ya juu England na hutolewa kila msimu kwa bingwa mpya.

Kombe hilo lina uzito mkubwa na lina muundo wa kipekee wenye simba watatu wanaowakilisha soka la England. Nahodha wa timu ndiye huwa wa mwisho kulinyanyua mbele ya mashabiki.

Litatunzwa na Arsenal hadi msimu ujao pale bingwa mpya atakapopatikana. Pia lina historia ndefu ya vilabu vikubwa vilivyolitwaa kabla yao.

Kwa Arsenal, kombe hili lina maana ya kurejea kwenye hadhi ya mabingwa wa England baada ya miaka mingi ya kukosa taji hilo.

Medali 40 za ubingwa

Arsenal pia wamepata medali 40 za ubingwa wa EPL kwa msimu huu. Medali hizo hutolewa kwa wachezaji, makocha na baadhi ya maafisa wa klabu.

Kwa mujibu wa sheria za ligi, mchezaji lazima awe amecheza angalau mechi tano ili kustahili medali moja moja kwa moja. Hata hivyo, klabu inaweza kugawa medali hizo kwa mapenzi yao ndani ya kikosi.

Nyota kama David Raya, Bukayo Saka, Declan Rice na Martin Ødegaard ni miongoni mwa waliotoa mchango mkubwa msimu huu. Wao ni sehemu muhimu ya mafanikio ya ubingwa huo.

Medali hizo zina thamani ya kihistoria zaidi kuliko kifedha, kwani zinabaki kama kumbukumbu ya ushindi wa kipekee wa msimu.

3. Fedha za nafasi ya ubingwa

Ingawa EPL haina "bonus" maalum ya ubingwa, klabu hupata mgao mkubwa wa mapato kulingana na nafasi yao baada ya msimu kumalizika. Arsenal, kama mabingwa, wanapata sehemu kubwa zaidi ya mgao huo. Bingwa wa mwaka jana, Liverpool walipata jumla ya £174.9 million, kiasi ambacho Arsenal watakipata kama ama zaidi kidogo ya hicho.

Fedha hizi zinatokana na mfumo wa malipo wa ligi, ambapo kila nafasi hupewa thamani tofauti ya kifedha. Nafasi ya kwanza hupata kiwango cha juu zaidi.

Hii ina maana kuwa mafanikio ya uwanjani yana athari moja kwa moja kwenye mapato ya klabu. Kadri unavyofanya vizuri, ndivyo unavyopata fedha zaidi.

Zaidi ya hayo, ubingwa huongeza thamani ya kibiashara ya klabu duniani kote kupitia udhamini, urushwaji wa mechi na mauzo ya bidhaa.

4. Nafasi ya kushiriki ligi ya mabingwa Ulaya

Kwa ubingwa huu, Arsenal wamefuzu moja kwa moja kushiriki michuano ya Klabu bingwa Ulaya msimu ujao, michuano ambayo ina thamani kubwa ya fedha.

Mashindano hayo huwakutanisha vilabu bora zaidi kutoka ligi mbalimbali za Ulaya. Kwa Arsenal, ni nafasi ya kujaribu kuimarisha hadhi yao kimataifa. Msimu huu imeingia fainali na itacheza na PSG Mei 30, 2026 huko Budapest.

Mbali na mapato makubwa ya klabu kupitia matangazo na tuzo za ushindi, kushiriki michuano hii pia huwavutia wachezaji wakubwa zaidi kujiunga na klabu yenye ushindani wa kimataifa.

Kuvaa jezi yenye nembo ya dhahabu msimu mzima

Kuanzia msimu ujao, Arsenal watavaa nembo ya dhahabu kwenye jezi zao kama mabingwa watetezi. Hii ni alama maalum inayotolewa kwa mabingwa wa EPL pekee.

Nembo hii hutumika msimu mmoja tu na inaonyesha hadhi ya klabu kama bingwa wa sasa wa England. Ni ishara ya heshima na mafanikio.

Mashabiki tayari wameanza kununua jezi mpya zenye nembo hiyo kupitia maduka rasmi ya klabu. Hii pia huongeza mauzo ya bidhaa za klabu.

Ni mara ya kwanza kwa kikosi hiki kuvaa nembo hiyo tangu mfumo huu ulipoanzishwa.

6. Kucheza FA Community Shield

Kwa kushinda taji la EPL, Arsenal pia wamepata nafasi ya kucheza mechi ya FA Community Shield dhidi ya mabingwa wa FA Cup ambaye ni Manchester City. Mechi hii huashiria ufunguzi wa msimu mpya wa soka England.

Mchezo huo kwa kawaida huchezwa Wembley na huwakutanisha mabingwa wa ligi na wa kombe la FA. Ni mechi ya heshima lakini pia ya ushindani.

Kwa Arsenal, hii ni nafasi ya kuongeza taji lingine kabla ya kuanza kwa msimu mpya. Pia huongeza maandalizi ya timu kuelekea michuano ya ligi ya mabingwa Ulaya.

Mechi hii pia huleta mapato na heshima zaidi kwa klabu zinazoshiriki.