Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Ndege za kivita za Marekani zilizoshambuliwa na Iran wakati wa Vita
Ripoti mpya ya Bunge la Congress ya Marekani imefichua ukubwa wa hasara za kijeshi za Marekani katika vita vyake na Iran, huku ripoti ikiongezea kuwa jumla ya ndege 42 za kivita za Marekani zilishambuliwa na kuharibiwa wakati wa vita hivyo.
Ripoti hii ilitayarishwa na Huduma ya Utafiti ya Bunge la Congress ya Marekani, kulingana na taarifa kutoka Idara ya Ulinzi ya Marekani, Kamandi Kuu ya Marekani na vyombo vya habari.
Ripoti hiyo ilichapishwa kwenye tovuti ya Congress ya Marekani.
Idara ya utafiti ilitoa taarifa kuhusu matatizo yaliyokabili idara za mipango ya kijeshi, bila kujali vyama vya kisiasa.
Ripoti hiyo ilisema vifaa vya kijeshi vilivyoharibiwa ni pamoja na ndege za kivita, ndege zisizo na rubani, helikopta zenye silaha, na ndege za operesheni maalum.
Ripoti hiyo pia inamnukuu afisa wa Wizara ya Ulinzi ya Marekani, Jules W. Hurst, ambaye aliliambia Bunge la Congress kwamba Marekani ilitumia zaidi ya dola bilioni 29 katika vita hivyo, ikiwa ni pamoja na gharama za ukarabati na utengenezaji wa ndege zilizoharibiwa .
F-15E
Ndege za kijeshi zilizotajwa kwenye ripoti hiyo ni pamoja na ndege nne za F-15E Strike Eagle.
Kamandi Kuu ya Marekani ilisema baadhi ya ndege hizo zilidunguliwa ndani ya Kuwait, katika kile ilichokitaja kama "mashambulizi ya kimakosa ya vikosi vya muungano."
Katika tukio moja, wanajeshi sita walitoroka bila kujeruhiwa.
Kamandi Kuu ya Marekani ilisema kwamba mnamo Aprili 5, 2026, ndege ya kivita ya F-15E Strike Eagle ilianguka wakati wa uvamizi ndani ya Iran, na marubani wake wawili waliokolewa katika operesheni kubwa ya uokoaji.
Ripoti hiyo pia ilinukuu taarifa iliyotolewa Mei 19, ikisema kuwa ndege ya kivita ya Marekani F-35 Lightning II ilipotea baada ya kudunguliwa na mfumo wa kujilinda na makombora wa Iran.
Wakati huo, Kamandi Kuu ya Marekani ilithibitisha kwamba ndege ya F-35 Lightning II ilitua kwa dharura baada ya kushambuliwa nchini Iran, lakini ilitua salama, na rubani alikuwa mzima wa afya.
Hata hivyo, Kituo cha Operesheni za Kijeshi hakikutoa maelezo zaidi kuhusu tukio hilo, ingawa kituo cha habari cha Marekani CNN kiliripoti kuwa ndege hiyo ilishambuliwa.
Mnamo 2026, Mwenyekiti wa Wakuu wa Pamoja wa Wanajeshi wa Marekani, Jenerali Dan Caine, alisema kuwa mnamo Aprili 3, ndege ya A-10 Thunderbolt II ilidunguliwa na adui na kisha kuanguka, lakini rubani alinusurika.
Ndege ya kujaza mafuta angani KC-135
Zaidi ya hayo, ndege ya mafuta ya KC-134 ilianguka katika anga ya Iraq, na kusababisha hasara ya marubani sita.
Ndege nyingine tano pia ziliharibiwa katika shambulio la kombora kwenye kambi ya kijeshi ya Prince Sultan nchini Saudi Arabia.
Ripoti hiyo pia ilithibitisha kuharibiwa kwa ndege ya uchunguzi na upelelezi ya Marekani E-3 Sentry, ambayo ilishambuliwa ndani ya Saudia
Picha zilizotolewa baadaye zilionyesha mabaki ya ndege hiyo ikiwa imevunjika vipande viwili.
Ndege ya kutoa tahadhari ya E 3 Sentry
Ripoti hiyo inaeleza kuwa mnamo Machi 28, shambulio la kombora la Iran na ndege zisizo na rubani zililenga kambi ya ndege ya Prince Sultan nchini Saudi Arabia, ambapo ndege aina ya E - 3 Sentry iliripotiwa kuharibiwa.
Mnamo Machi 7, iliripotiwa pia kuwa ndege hizo ziliegeshwa katika eneo lisilo salama.
Wakati huo, picha zilizopigwa kutoka uwanja wa ndege zilionyesha jinsi ndege ya Jeshi la Anga la Marekani ilivyoanguka.
Kitengo cha kuangalia ukweli cha BBC kilithibitisha kwamba picha hizo zilipigwa ndani ya kambi ya Prince Sultan, takriban kilomita 100 kutoka mji mkuu Riyadh.
Majengo yaliyoonekana kwenye picha, kama vile vituo vya data na maghala ya kuhifadhi, yalisemekana kuwa sawa sawa na picha za satelaiti.
Ndege ya kivita aina ya MC 130J Komando
Mnamo Aprili 5, ripoti zilisema kwamba ndege mbili za Marekani aina ya MC-130J Commando II zilizokuwa zikisaidia katika shughuli za uokoaji zilitunguliwa baada ya ndege ya kivita ya F-15E Strike Eagle kuanguka nchini Iran.
Ripoti hiyo ilisema moja ya ndege hizo ilishindwa kuruka au kufanya kazi kama kawaida kutoka eneo la kutua, ingawa marubani walifanikiwa kuokolewa.
Pia iliripotiwa kuwa Iran ilimpiga Tai mwengine wa F-15E, huku mmoja wa marubani ambaye hakufahamika jina lake akiwa ndani ya ndege hiyo, na kusababisha operesheni kubwa ya uokoaji.
Taarifa kutoka kwa baadhi ya vyombo vya habari vya Iran zilisema kuwa kulikuwa na mapigano kati ya majeshi ya Marekani na Iran wakati wa operesheni ya kumtafuta rubani ndani ya Iran.
Rais wa Marekani Donald Trump alielezea tukio hilo kama "operesheni kubwa sana ya uokoaji" ndani ya Iran, iliyohusisha ndege nyingi.