Marekani yazuia mali za kidijitali za 'zaidi ya dola milioni 130' zinazohusishwa na Iran
Waziri wa Fedha wa Marekani Scott Besant ametangaza kufungia mali za kidijital za Iran zilizo na thamani ya "zaidi ya dola milioni 130".
"Idara ya Fedha ya Marekani imejitolea kudhibiti shughuli haramu za kifedha za Iran, ikiwa ni pamoja na matumizi mabaya ya mali za kidijitali,"Scott Besant alisema katika chapisho kwenye mtandao wa kijamii X
Aliongeza kusema: "Idara ya Udhibiti wa Mali za Kigeni ya Wizara ya Fedha ya Marekani iliidhinisha kuzuiliwa kwa akaunti kadhaa za kidijitali zilizounganishwa na Benki Kuu ya Iran, na kusababisha kufungiwa kwa zaidi ya dola milioni 130."
"Tutaendelea kufuatilia na kudhibiti utakasaji wa pesa na kuinyima serikali ya Iran ufikiaji wa mapato ya programu zake haramu za mapato."
Idara ya Udhibiti wa Mali za Kigeni ya Marekani hivi karibuni iliwekea vikwazo masoko kadhaa makubwa ya Iran ambayo, kulingana na idara hiyo, yalihamisha mabilioni ya dola kila mwaka kwa niaba ya benki za Iran zilizowekewa vikwa kutumia mtandao wa makampuni ya siri kuficha shughuli haramu za kifedha za serikali.
Maelezo zaidi: