Zelensky ailaani Marekani kwa kuongeza muda wa msamaha wa vikwazo kwa Urusi
Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky, amelaani uamuzi wa Marekani wa kuongeza muda ambao Urusi inaruhusiwa kuuza mafuta licha ya vikwazo vya Magharibi.
Hatua hiyo inamaanisha nchi zinaweza kununua mafuta na bidhaa za petroli za Urusi ambazo tayari zimeshapakiwa kwenye meli baharini hadi tarehe 16 Mei.
Marekani inasema msamaha huo unalenga kupunguza upungufu wa nishati uliosababishwa na vita kati ya Marekani na Israel dhidi ya Iran.
Lakini katika kauli yake Jumapili, Zelensky alisema kuwa “kila dola inayolipwa kwa mafuta ya Urusi ni pesa ya kufadhili vita” nchini Ukraine.
Vikwazo vikali vimewekwa dhidi ya Urusi tangu Rais Vladimir Putin alipoanzisha uvamizi mkubwa dhidi ya nchi jirani mwezi Februari 2022.
Mashambulizi makubwa ya Marekani na Israel dhidi ya Iran yamesababisha nchi hiyo kujibu si tu dhidi ya Israel na kambi za kijeshi za Marekani katika Ghuba, bali pia dhidi ya miundombinu ya nishati na maeneo ya raia katika nchi za Kiarabu washirika wa Marekani katika eneo hilo.
Aidha, Iran imezuia kwa kiasi kikubwa Mlango wa Hormuz, njia nyembamba ambayo karibu asilimia 20 ya mafuta na gesi asilia ya dunia husafirishwa kupitia kwayo.
Hali hiyo imesababisha mabadiliko makubwa katika masoko ya nishati, huku hofu ikiongezeka kwamba huenda uchumi wa dunia ukaingia katika mdororo iwapo njia hiyo haitafunguliwa hivi karibuni.
Unaweza kusoma;