Mabaharia watatu wa India wauawa katika shambulio la Marekani karibu na Oman
Waziri wa Meli wa New Delhi, Sarbananda Sonowal, ametangaza kwamba mabaharia watatu wa India wameuawa baada ya shambulio la Marekani kwenye meli ya Settebello yenye bendera ya Palau, akielezea tukio hilo kuwa la "kusikitisha".
Katika chapisho kwenye mtandao wa X, amesema kwamba vifo vyao ni "pigo kubwa".
Meli ya Settebello yenye bendera ya Palau ilishambuliwa Jumatano baada ya jeshi la Marekani kuishutumu kwa kukiuka kizuizi cha Marekani kwa "kujaribu kusafirisha mafuta kutoka Iran". Kulikuwa na wafanyakazi 24 wa India ndani ya meli hiyo - 21 waliokolewa.
Kamandi Kuu ya Marekani ilisema ilifyatua risasi kwenye chumba cha injini cha meli hiyo baada ya wafanyakazi "kushindwa mara kadhaa kufuata" masharti ya vikosi vya Marekani.
Manoj Yadav, katibu mkuu wa Muungano wa Mabaharia nchini India, aliliambia gazeti la The Economic Times kwamba "haamini" kuwa Marekani haikuwa na taarifa kuhusu uraia wa watu waliokuwa ndani ya meli hizo. Alisema kuwa kuzuia meli hizo badala yake ni "njia mbadala iliyofaa".
Hii ni meli ya pili yenye wafanyakazi wa India ambayo imeshambuliwa wiki hii. Siku ya Jumatatu, vikosi vya Marekani viliishambulia Marivex, ambayo pia ni meli ya mafuta yenye bendera ya Palau yenye wafanyakazi wa India, katika Ghuba ya Oman baada ya kushindwa kufuata maagizo ya Marekani, Centcom ilisema.
Wafanyakazi wote 24 waliokolewa na jeshi la Oman, mamlaka ya India ilisema.
Soma zaidi: