Kombe la Dunia 2026: Kwa nini timu za Ulaya zinatawala?

k

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Uswisi yaishinda Colombia kwa mikwaju ya penalti
Iliyochapishwa
Muda wa kusoma: Dakika 4

Kihistoria, timu za Ulaya hazifanyi vizuri katika Makombe ya Dunia yanayofanyika nje ya bara hilo.

Ni mara mbili tu tangu 1930 wameshinda katika mashindano kama hayo - Uhispania ikishinda kule Afrika Kusini mwaka 2010 na Ujerumani nchini Brazil miaka minne baadaye.

Kwa mwaka 2026, kuna timu sita kati ya nane zitakazoshiriki robo fainali zinatoka Ulaya: Ubelgiji, Uingereza, Ufaransa, Norway, Uhispania na Uswisi, huku Argentina na Morocco zikikamilisha orodha.

Orodha hii ndio timu nyingi zaidi za Ulaya kufikia robo fainali katika Kombe la Dunia lililofanyika nje ya Ulaya tangu 1994.

Nguvu ya timu za Ulaya

Timu kutoka Ulaya zimejijenga wakati Kombe la Dunia likiendelea, kwani timu saba kati ya 10 za Ulaya zilicheza michezo yao ya kwanza ya hatua ya makundi huku zikishindwa kushinda.

Joto la Amerika Kaskazini lilikuwa gumzo kabla ya mashindano kuanza huku timu kadhaa - ikiwa ni pamoja na Uingereza - zikijikita katika maeneo yenye joto ili kuzoea kwa ajili mechi zao za ufunguzi.

Baada ya Ubelgiji kuanza kwa sare na Misri, kocha Rudi Garcia alisema: "Iwe ni nyuzi joto 10 au 30, tunapaswa kufanya vizuri zaidi," huku kocha wa Uswisi, Murat Yakin, alizungumzia kiwango kibovu cha timu yake baada ya sare ya 1-1 na Qatar, na hakulaumu hali ya hewa.

Lakini hatimaye timu za Ulaya ziliingia katika hatua ya makundi na kufikia mwisho wa hatua ya makundi kulikuwa na ushindi mara 17, sare 12 na kupoteza michezo saba kwa timu za Ulaya dhidi ya timu zisizo za Ulaya.

"Hii imeonyesha kuwa tuna timu zenye uwezo wa kushinda Kombe la Dunia," mshambuliaji wa zamani wa Uingereza Wayne Rooney aliambia BBC Sport baada ya ushindi wa Uingereza wakati Mexico wakiwa nyumbani.

"Imani hii itawapa wachezaji nguvu kubwa."

Wakati huo huo, Ufaransa ilikabiliana na “mbinu chafu” za Paraguay ili kusonga mbele hadi raundi ya nane huku Ubelgiji ikikabiliana na mashabiki wa nyumbani waliokuwa wakitarajia ushindi wa Marekani katika raundi yao ya 16.

Ubelgiji watakabiliana na mabingwa wa Ulaya, Uhispania, katika nusu fainali.

Kwa nini Ulaya inatawala?

m
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Ulaya siku zote ina uwezekano mkubwa wa kuwa na wawakilishi wengi ikizingatiwa kwamba wanapewa nafasi ya kupeleka timu 16 katika Kombe la Dunia - zaidi ya bara jingine lolote.

Timu za Ulaya pia zinatawala viwango vya dunia vya Fifa zikiwa na timu tano kati ya nane bora. Ureno, iliyoorodheshwa ya saba, ilitolewa na Uhispania katika mechi ya raundi ya 16 bora ya Ulaya.

Ufaransa imeanza mashindano haya kama timu inayopewa nafasi kubwa ya kushinda Kombe la Dunia na wanakwenda vyema hadi sasa, huku mshambuliaji Kylian Mbappe akiwa miongoni mwa wale walio kwenye kinyang'anyiro cha Golden Boot (mfungaji bora) akiwa na mabao saba.

"Ni vigumu kuipuuza Ufaransa kwa nguvu waliyonayo," kiungo wa zamani wa Uingereza Danny Murphy alisema katika utabiri wake kabla Kombe la Dunia kuanza.

"Wachezaji kama Rayan Cherki, Ousmane Dembele na Desire Doue hawawezi kucheza wote kwa wakati mmoja, lakini wanaweza kubadilisha mchezo ikiwa wataingia hata baada ya dakika 70.”

Beki wa zamani wa Ufaransa Gael Clichy alisema: "Ufaransa, Uhispania na Uingereza ndizo timu tatu kwangu ambazo zitafanya vizuri."

Timu za Ulaya zinasonga mbele

Huenda kungekuwa na mshangao zaidi kama kusingekuwa na Ufaransa, Uhispania, Uingereza kufikia hatua hii ya mashindano.

Lakini kumekuwa na timu kadhaa za Ulaya zikifanya vizuri zaidi ya matarajio ya wengi.

Norway wanatumia vyema kurudi kwao kwenye Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza tangu 1998, wakisaidiwa na Erling Haaland kung'aa kwenye jukwaa la kimataifa.

Mshambuliaji huyo wa Manchester City amefunga mabao saba hadi sasa katika mashindano hayo na huenda ataongeza mabao dhidi ya England siku ya Jumamosi.

Wakati huo huo, Uswisi pia wameonyesha ubora na utulivu licha ya kukabiliwa na hali ngumu katika ushindi wao wa mikwaju ya penalti dhidi ya Colombia katika mechi ya mwisho ya hatua ya 16 bora.

Ushindi wao unamaanisha kuwa kikosi cha Murat Yakin kimefika hatua ya nane bora ya Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza tangu 1954, lakini kinakabiliwa na kibarua kigumu dhidi ya mabingwa watetezi Argentina.

"Huu ni wakati wa kihistoria," alisema Yakin. "Tumefikia kiwango bora zaidi kwa timu ya Uswisi lakini safari inaendelea."

Safari inaendelea huku timu za Ulaya ziendelea na mbio za kutoa mshindi wa Kombe la Dunia 2026, katika mashindano yanayochezwa nje ya bara la Ulaya