Tetesi Ulaya: Sano, Bouaddi wazigonganisha City, United, Liverpool na Arsenal

Chanzo cha picha, AFP via Getty Images
Manchester City, Manchester United na Bayern Munich zimejiunga na Arsenal katika kuwania kiungo wa Morocco Ayyoub Bouaddi mwenye umri wa miaka 18. Hata hivyo, Lille inataka angalau pauni milioni 70 na pia inapendelea kumbakiza kwa mkopo msimu ujao. (Daily Mail)
Liverpool, Arsenal, Manchester United na Borussia Dortmund zinamfuatilia kiungo wa Mainz Kaishu Sano, mwenye umri wa miaka 25, ambaye aliifungia Japan katika mchezo wao wa hatua ya 32 bora ya Kombe la Dunia dhidi ya Brazil. (Bulinews, via Nikkan Sports)
Mabingwa wa Ulaya Paris Saint-Germain (PSG) wanasema thamani ya winga wa Ufaransa Bradley Barcola ni zaidi ya pauni milioni 116, huku wakisisitiza kuwa hawana mpango wa kumuuza mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 licha ya kuvutiwa na Liverpool na Arsenal. (The Athletic)
Liverpool pia imehusishwa na winga wa Ubelgiji Matias Fernandez-Pardo, mwenye umri wa miaka 21, anayekipiga Lille, katika jitihada zake za kuimarisha safu ya ushambuliaji. (Express)
Everton ina matumaini ya kumsajili moja kwa moja winga wa Chelsea Tyrique George, mwenye umri wa miaka 20, ambaye aliichezea klabu hiyo kwa mkopo msimu uliopita. (Teamtalk)

Chanzo cha picha, Kaishu Sano
Chelsea inataka kuongeza nguvu katika safu yake ya ushambuliaji kwa kumsajili mshambuliaji wa Bournemouth Eli Junior Kroupi. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa chini ya miaka 21 mwenye umri wa miaka 20 alifunga mabao 13 katika Ligi Kuu ya England msimu uliopita. (Caught Offside)
Tottenham imekubaliana masharti binafsi na kiungo wa Newcastle Sandro Tonali, mwenye umri wa miaka 26, na ipo tayari kutoa karibu pauni milioni 100 kumsajili Muitaliano huyo. (Teamtalk)
Winga wa AC Milan Samuel Chukwueze, mwenye umri wa miaka 27, ameikataa Trabzonspor ya Uturuki kwa kuwa anataka kubaki Milan baada ya Fulham kuamua kutomsajili moja kwa moja kufuatia kipindi chake cha mkopo. (Daily Post)
Brentford ipo kwenye mazungumzo ya kumsajili mshambuliaji wa England Callum Wilson, mwenye umri wa miaka 34, kwa uhamisho wa bure baada ya mkataba wake na West Ham kumalizika mwishoni mwa msimu uliopita. (The Athletic)















