Maandamano makubwa kupinga wahamiaji haramu yafanyika Afrika Kusini

Maafisa wa polisi wamesambazwa kote Afrika Kusini kutokana na hofu kwamba maandamano yanayopinga uhamiaji yanaweza kugeuka kuwa ya vurugu.

Muhtasari

Skip Video and continue reading
  • Lungu
  • xx
  • xx
  • d
  • s
  • a
  • Sonko
  • xx
  • xx
  • xx
  • xx
  • xx
  • Dangote
  • xx
  • Lydia Wanjiku

Moja kwa moja

Na Mariam Mjahid na Lizzy Masinga

  1. Mahakama yakataa jaribio la Trump la kunyima uraia wa kuzaliwa watoto wa wahamiaji wasio na nyaraka

    Kuna makumi ya kamera za televisheni zilizowekwa nje ya jengo la mahakama

    Chanzo cha picha, Reuters

    Mahakama Kuu ya Marekani imekataa jaribio la Rais Donald Trump la kuondoa haki ya uraia wa kuzaliwa kwa watoto wanaozaliwa nchini humo na wazazi wasio na nyaraka halali za uhamiaji.

    Trump na timu yake ya wanasheria walikuwa wamewasilisha hoja iliyokuwa na uungwaji mkono mdogo miongoni mwa watunga sera na wataalamu wa sheria kwa muda mrefu.

    Hata hivyo, hoja hiyo ilifikishwa hadi Mahakama Kuu, jambo lililoonekana kuwa hatua kubwa kisiasa na kisheria.

    Mwisho wa yote, majaji wengi kati ya tisa wa Mahakama Kuu hawakuwa tayari kubatilisha uamuzi wa mahakama uliowekwa takriban miaka 150 iliyopita, wala kutafsiri upya sheria za muda mrefu za nchi na katiba ya Marekani kwa lengo la kumpatia Trump ushindi.

    Uamuzi huo ni pigo kwa Trump na huenda ukamlazimu kutafuta mbinu nyingine za kuzuia wahamiaji wasiokuwa na nyaraka kuingia Marekani.

    Ikiwa wahamiaji hao hawatafanikiwa kufika nchini humo, basi suala la uraia wa watoto wao wanaozaliwa nchini Marekani halitazuka.

  2. Qatar yasema wajumbe wa Marekani wako Doha kukutana na wapatanishi, na si maafisa wa Iran

    Wajumbe wa Marekani, Jared Kushner na Steve Witkoff, walishiriki katika duru ya kwanza ya mazungumzo kati ya Marekani na Iran yaliyofanyika nchini Uswisi.

    Chanzo cha picha, Reuters

    Mjumbe maalum wa Marekani, Steve Witkoff, pamoja na mkwe wa Rais Donald Trump, Jared Kushner, wamewasili jijini Doha, Qatar, kwa ajili ya mazungumzo kati ya Marekani na Iran na wapatanishi, kwa mujibu wa msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Qatar.

    Msemaji huyo, Majed Al-Ansari, amesema hakuna mikutano ya ngazi ya juu wala mazungumzo ya moja kwa moja yaliyopangwa kati ya wajumbe wa Marekani na maafisa wa Iran katika siku zijazo.

    Marekani na Iran zilikubaliana kusitisha mashambulizi dhidi ya kila upande na kutuma wajumbe nchini Qatar baada ya kushambuliana kwa muda wa siku nne.

    Mashambulizi hayo yalichochewa na mvutano kuhusu kufunguliwa tena kwa njia muhimu ya baharini ya Mlango bahari wa Hormuz

    Mashambulizi hayo yalitishia makubaliano ya awali yaliyolenga kumaliza vita vya miezi minne vilivyohusisha Marekani, Israel na Iran.

    Unaweza kusoma;

  3. Serikali ya Uganda yatetea hatua ya kufunga vyombo vikuu vya habari

    Muhoozi

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Serikali ya Uganda imetetea kufungwa kwa baadhi ya vyombo vikuu vya habari nchini humo vikiwemo Daily Monitor, NTV Uganda, na taasisi nyingine zinazomilikiwa na Nation Media Group Uganda.

    Katika taarifa rasmi iliyotolewa leo, msemaji wa serikali na Waziri wa Habari, Kasule Lumumba, amesema kufungwa kwa vyombo hivyo ni sehemu ya "uchunguzi unaoongozwa na vyombo vya usalama" ulioagizwa na Rais Yoweri Museveni.

    "Matukio ya tarehe 28 Juni 2026 yaliyosababisha kusitishwa kwa shughuli za Nation Media Group yalisababishwa na uchunguzi unaoongozwa na vyombo vya usalama. Serikali itatoa taarifa kwa umma mara uchunguzi huo utakapokamilika," amesema Lumumba.

    Kauli hiyo ya serikali imekuja siku mbili baada ya maafisa wenye silaha wa vyombo vya usalama kufunga ofisi za Nation Media Group mjini Kampala na kuamuru vituo vyake vya televisheni na redio kusitisha matangazo.

    Mkuu wa Majeshi ya Uganda, Jenerali Muhoozi Kainerugaba, ambaye pia ni mtoto wa Rais Yoweri Museveni, alithibitisha kupitia mtandao wa X kwamba aliamuru jeshi kufunga taasisi hiyo ya habari baada ya kupata idhini kutoka kwa baba yake.

    Aidha, Muhoozi alisema kuwa haamini kuwepo kwa uhuru wa vyombo vya habari.

    Wakati huo huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Nation Media Group Uganda, Susan Nsibirwa, amesema mazungumzo yanaendelea katika ngazi mbalimbali na jeshi kwa lengo la kuhakikisha vyombo hivyo vya habari vinafunguliwa tena na kurejea hewani.

    Hatua hiyo ya kufungwa kwa vyombo vya habari imekuja wakati ambapo serikali inaendelea kuongeza ukandamizaji dhidi ya wakosoaji wake.

  4. Ulinzi ni mkali Afrika Kusini wakati waandamanaji wanaopinga wahamiaji wakimiminika mitaani

    Waandamanaji

    Chanzo cha picha, Reuters

    Maafisa wa polisi wamesambazwa kote Afrika Kusini kutokana na hofu kwamba maandamano yanayopinga uhamiaji yanaweza kugeuka kuwa ya vurugu, huku Rais Cyril Ramaphosa akiwataka waandamanaji kujiepusha na "vitisho, vitendo vya kutisha au kutoa masharti."

    Maandamano hayo yanaashiria tarehe ya mwisho isiyo rasmi iliyowekwa na wanaharakati wanaotaka raia wote wa kigeni wasiokuwa na nyaraka halali waondoke nchini.

    Wengi tayari wameondoka ili kuepuka vurugu na vitisho. Polisi wa Afrika Kusini wanasema watu 25,000 tayari wamerejeshwa katika nchi zao. Wengi wao wanatoka katika mataifa mengine ya Afrika.

    Mhamiaji mmoja kutoka Malawi ambaye hana nyaraka halali aliiambia BBC kwamba alikuwa "na furaha kurudi nyumbani," lakini pia "amevunjika moyo" kwa kuwaacha watoto wake wanne wadogo.

    Wizara ya Polisi ilisema maandamano mengi nchini yalikuwa ya amani, ingawa kulikuwa na matukio machache ya uporaji na majaribio ya uporaji.

    Maandamano
    Muandamanaji akiwa na bango
    Maandamano
    Maandamano

    Johannesburg, ambako moja ya maandamano hayo yanafanyika, inaonekana kuwa tulivu isivyo kawaida. Maduka mengi katikati ya jiji yamefungwa, huku polisi wakionekana kwa wingi katika barabara kuu.

    Baadhi ya waandamanaji walirusha mawe, na kuvunja madirisha ya baadhi ya majengo ya makazi katika eneo la Yeoville, kitongoji cha Johannesburg kinachokaliwa na wahamiaji wengi kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika.

    Polisi walisema watu watano walikamatwa katika mji mkubwa wa Soweto kwa tuhuma za kushiriki katika uporaji wa duka linalomilikiwa na raia wa kigeni.

    Unaweza kusoma;

  5. Je, Tanzania na Kenya zimeondoa vikwazo vya biashara?

    Rais wa Kenya, Ruto na Samia wa Tanzania

    Chanzo cha picha, Ikulu Tanzania

    Na Alfred Lasteck

    Leo Juni 30, 2026 ni mwisho wa muda ambao Tanzania na Kenya zilijiwekea kuondoa vikwazo visivyo vya ushuru vinavyokwamisha biashara kati ya nchi hizo mbili.

    Hatua hiyo inalenga kuongeza biashara, uwekezaji na kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi katika Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Eneo huru la biashara barani Afrika (AfCFTA).

    Ahadi hiyo ilitolewa Mei 4 mwaka huu na Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, na Rais wa Kenya, William Ruto, wakati wa Jukwaa la Biashara la Tanzania na Kenya lililofanyika Dar es Salaam.

    Viongozi hao waliagiza taasisi zinazohusika na biashara, forodha na mipaka kuhakikisha vikwazo vilivyosalia vinaondolewa ifikapo Juni 30. "Ni lazima tuondoe kwa haraka vikwazo visivyo vya ushuru, ikiwemo ucheleweshaji mipakani, kutokuwiana kwa viwango na vikwazo vya upatikanaji wa masoko," alisema Rais Ruto.

    Aliongeza kuwa nchi hizo mbili zimeweka lengo la kuongeza biashara mpya yenye thamani ya dola bilioni moja pamoja na uwekezaji wa kuvuka mipaka wa dola milioni 504.

    Kwa upande wake, Rais Samia alisema Tanzania itaendelea kuboresha mifumo ya forodha kwa njia ya kidijitali na kuanzisha dirisha la siku 30 la kushughulikia migogoro ya wafanyabiashara kupitia Baraza la Pamoja la Biashara la Tanzania na Kenya.

    Vikwazo visivyo vya ushuru ni pamoja na ucheleweshaji wa mizigo mipakani, ukaguzi unaojirudia wa bidhaa, tofauti za viwango vya ubora, mabadiliko ya ghafla ya leseni na taratibu za forodha.

    Kwa mujibu wa wadau wa biashara, changamoto hizo huongeza gharama za bidhaa kwa kati ya asilimia 10 hadi 40. Jitihada za kuviondoa si za leo.

    Mwaka 2022, mawaziri wa biashara na uwekezaji wa Tanzania na Kenya walitambua vikwazo 68 vya biashara. Kufikia mwaka huu, 54 vilikuwa vimeondolewa, huku vingine vinne vikiondolewa Oktoba mwaka jana. Serikali zilisema vilivyosalia ndivyo vilivyolengwa kuondolewa ifikapo leo.

    Utafiti wa mwaka 2024 uliofanywa na Yohana Hasinati D. ulibaini kuwa vikwazo vya kiutawala bado vinaendelea katika eneo la Namanga. Utafiti huo ulieleza kuwa kutokuaminiana kati ya taasisi, hatua za kulipizana kisera, masuala ya kisiasa na tofauti za kodi vinaendelea kuchangia changamoto hizo, na kupendekeza utekelezaji kamili wa Itifaki ya Soko la Pamoja la Afrika Mashariki.

    Kwa mujibu wa Baraza la Biashara Afrika Mashariki (EABC), licha ya kuwepo kwa Umoja wa Forodha wa Afrika Mashariki tangu mwaka 2005, tofauti za kanuni na ucheleweshaji katika vituo vya mipakani bado vinaathiri biashara.

    Hatua hiyo inakuja wakati biashara kati ya nchi hizo mbili ilipopungua kwa mara ya kwanza ndani ya muongo mmoja. Takwimu za Kenya National Bureau of Statistics (KNBS) Economic Survey 2026 zinaonyesha biashara kati ya Tanzania na Kenya ilishuka kwa asilimia 9.4 mwaka 2025, kutoka shilingi za Kenya bilioni 125.9 mwaka 2024 hadi shilingi bilioni 114.1.

    Mmoja wa wafanyabiashara wa mahindi kutoka Moshi anayesafirisha mazao yake kwenda Kenya ana matumaini kuwa kuondolewa kwa vikwazo hivyo kutarahisisha biashara. "Tutafarijika kama vikwazo vyote vitaondolewa.

    Kenya na Tanzania ni ndugu; ni watu mmoja waliotenganishwa na mipaka ya kikoloni. Tukirahisishiwa biashara, sote tutanufaika na kuinuka kiuchumi," anasema.

    Sekta binafsi kupitia EABC pia imezitaka serikali mbili kuharakisha utekelezaji wa makubaliano hayo. "Kuna haja ya kuchukua hatua za haraka kuondoa vikwazo visivyo vya ushuru, kuboresha utabirikaji wa sera, kuoanisha viwango na kuharakisha taratibu za forodha ili kuongeza ushindani wa biashara katika ukanda," limesema Baraza hilo.

    Hata hivyo, hadi kufikia leo haijawekwa wazi iwapo vikwazo vyote vilivyokuwa vimesalia vimeondolewa kama ilivyoahidiwa.

  6. Kesi ya uhaini dhidi ya Kizza Besigye kuanza kusikilizwa leo Uganda

    f

    Chanzo cha picha, Reuters

    Kiongozi wa upinzani nchini Uganda, Kizza Besigye, anatarajiwa kufikishwa mahakamani leo mjini Kampala kuanza kusikilizwa kwa kesi ya uhaini inayomkabili.

    Besigye na msaidizi wake, Obeid Lutale, wanakabiliwa na mashtaka ya kupanga njama za kuipindua serikali ya Uganda.

    Besigye alikamatwa mjini Nairobi mnamo Novemba 2024 na kurejeshwa kwa nguvu nchini Uganda, ambako amekuwa akizuiliwa tangu wakati huo.

    Kesi hiyo inaanza kusikilizwa leo baada ya kuahirishwa mara kadhaa hapo awali.

    Besigye, aliyekuwa daktari wa binafsi wa Rais Yoweri Museveni, mwaka jana hali ya afya yake ilidhoofika na kukimbizwa hospitalini kabla ya kurejeshwa gerezani.

    Katika uamuzi wa kihistoria mwaka jana, Mahakama ya Juu ya Uganda ilitangaza kuwa ni kinyume cha katiba kwa mahakama za kijeshi kuwahukumu raia, na kuamuru kesi zote hizo kuhamishiwa katika mahakama za kiraia.

    Uamuzi huo ulimkasirisha Rais Museveni, ambaye alipuuzilia mbali na kuutaja kuwa "uamuzi usio sahihi" na kuapa kuupinga.

    Raia wengi wa Uganda ikiwemo mpinzani mwenza Bobi Wine aliandika kwa mtandao wa kijamii kushurutisha Besigye aachiliwe huru na aruhusiwe kupata huduma za matibabu.

    Soma Zaidi:

  7. Hofu ya ghasia huku Afrika Kusini ikiimarisha ulinzi kabla ya maandamano dhidi ya wahamiaji

    h

    Chanzo cha picha, Anadolu via Getty Images

    Vyombo vya usalama vimeimarishwa kote nchini Afrika Kusini kutokana na hofu kwamba maandamano dhidi ya wahamiaji yanaweza kugeuka na kuwa ya vurugu, huku Rais Cyril Ramaphosa akiwataka watakaoshiriki kufanya hivyo bila "vitisho au kutoa masharti."

    Maandamano hayo yanafanyika baada ya wanaharakati kuweka tarehe ya mwisho isiyo rasmi ya kuwataka wageni wote wasio na nyaraka halali kuondoka nchini.

    Wengi wao tayari wameondoka ili kuepuka vitisho na ghasia. Polisi wa Afrika Kusini wanasema watu 25,000 wamekwisharejeshwa katika nchi zao, wengi wao wakitoka mataifa mengine ya Afrika.

    Mhamiaji mmoja kutoka Malawi asiye na nyaraka halali ameiambia BBC kuwa ana furaha kurejea nyumbani, lakini amevunjika moyo kwa kuacha nyuma watoto wake wanne wadogo.

    Johannesburg, ambako moja ya maandamano hayo yanatarajiwa kufanyika, imeonekana kuwa tulivu isivyo kawaida, huku maduka yote karibu na eneo la mkusanyiko wa waandamanaji yakiwa yamefungwa.

    Rais Ramaphosa amesisitiza mara kadhaa kuwa maandamano yafanyike kwa amani na uwajibikaji, huku pia akitambua haja ya kufanya mageuzi ya sera za uhamiaji.

    Aliwakumbusha wananchi kuwa baadhi ya raia wa kigeni wanaishi Afrika Kusini kihalali.

    "Wanafanya kazi, wanasoma, wanalea familia, wanawekeza katika uchumi wetu na wanachangia kwa njia chanya katika jamii yetu. Nao pia wana haki ya kulindwa na sheria na Katiba yetu."

    Aliongeza kuwa:

    "Haki ya kuandamana na uhuru wa kujieleza havitoi ruhusa ya kutishia au kuwahofisha wengine, wala kushiriki vitendo vya uharibifu au vurugu."

    Kwa mujibu wa takwimu rasmi, kuna zaidi ya wahamiaji milioni tatu wenye nyaraka halali nchini Afrika Kusini.

    Kabla ya kufika kwa muda huo wa mwisho, maelfu ya wahamiaji wamekuwa wakisubiri kushughulikiwa katika kambi za muda kwa wiki kadhaa kutokana na hofu ya usalama wao.

    Huko Durban, ambako baadhi ya maandamano makubwa zaidi yamefanyika, mahema meupe yanayowahifadhi zaidi raia wa Malawi yameanza kubomolewa huku mamlaka zikikimbizana kuondoa kambi hiyo ya mpito.

    Mwanamume mmoja kutoka Malawi, Hassan Phiri, alitoa ujumbe kwa waandamanaji:

    "Ninachotaka kuwaambia Waafrika Kusini ni kwamba sisi sote ni kitu kimoja. Afrika haiwezi kuwa Afrika bila Afrika Kusini, bila Malawi na bila mataifa mengine. Lazima tupendane na tushikamane kama Waafrika."

    Soma Zaidi:

  8. Polisi wenye silaha za moto watanda katika jiji la Dar es Salaam, Tanzania

    g

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Kumekuwa na ongezeko la Polisi wanaoshika doria katika jiji la kibiashara la Dr es Salaam, Tanzania katika siku ya hivi karibuni.

    BBC imeshuhudia Polisi wenye silaha za moto katika makutano ya barabara na vituo vya mabasi ya mwendo kasi, wakiwa na magari ya polisi na magari ya washawasha.

    Gazeti la The Citizen, limeripoti kushuhudia polisi katika maeneo ya Magomeni, Buguruni, Tazara, Ubungo, Uhasibu, Fire na Mwenge.

    Kuongezeka ulinzi huo kunakuja huku kukiwa na taarifa zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu maandamano yanayopangwa kufanyika Julai 7.

    Haya yanajiri, siku chache tangu serikali ya Tanzania kusimamisha mikutano ya hadhara ya vyama vyote vya siasa, kwa madai ya kuwepo kwa uwezekano wa uvunjifu wa amani katika kipindi cha Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba.

    Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro ameviambia vyombo vya habari kwamba kuwepo kwa askari hao ni sehemu ya operesheni za kawaida za polisi zinazolenga kulinda raia na mali zao.

    Soma Zaidi Hapa:

  9. Waomba hifadhi nchini Uingereza kulipa hadi pauni 10,000 baada ya kupata kazi

    f

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Serikali ya Uingereza imetangaza kuwa watu watakaopewa hifadhi nchini humo watalazimika kulipa hadi pauni 10,000 (takribani Shilingi milioni 35 za Tanzania) kufidia gharama za makazi na msaada waliopatiwa baada ya kupata ajira.

    Sheria hizo mpya zitakuwa sehemu ya Muswada wa Uhamiaji na Hifadhi utakaowasilishwa bungeni Jumanne. Chini ya utaratibu huo, fedha hizo zitakusanywa kwa awamu kutoka kwa watu wazima wenye uwezo wa kifedha.

    Sharti hilo litawahusu wakimbizi wenye haki ya kufanya kazi nchini Uingereza, na watalazimika kulipa kiasi hicho kabla ya kupewa haki ya kuishi nchini humo kwa kudumu.

    Waziri wa Mambo ya Ndani, Shabana Mahmood, amesema mabadiliko hayo yanaakisi ukweli kwamba "msaada wa hifadhi ni haki, lakini pia unaambatana na wajibu."

    Alisema: "Tunatarajia watu wenye uwezo wa kifedha wachangie na kurejesha ukarimu walioonyeshwa na wananchi wa Uingereza."

    Chini ya mapendekezo hayo, wahamiaji wanaofikia kiwango fulani cha mapato watalazimika kulipa kiasi maalumu, kinachotarajiwa kuwa pauni 10,000.

    Wizara ya Mambo ya Ndani bado haijaweka kiwango cha chini cha mapato kitakachomlazimu mtu kuanza kulipa kwa awamu.

    Pia, Waziri wa Mambo ya Ndani atakuwa na mamlaka ya kurekebisha kiwango hicho na vigezo vya malipo ili kuhakikisha mfumo huo unakuwa wa haki kwa walipa kodi na haubagui wahamiaji.

    Watu ambao maombi yao ya hifadhi yatakataliwa pia watalazimika kurejesha gharama hizo ikiwa watakuwa na mapato yanayokidhi viwango vya serikali.

    Kwa mujibu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Uingereza, karibu pauni bilioni nne za fedha za walipa kodi zilitumika mwaka jana kuwasaidia waomba hifadhi.

    Hata hivyo, Baraza la Wakimbizi la Uingereza limepinga mpango huo, likisema ni "usio wa haki na usiowezekana kutekelezwa", na kwamba ni sawa na "kodi ya ziada kwa wakimbizi" ambayo itafanya iwe vigumu kwa familia nyingi kujijenga upya na kuanza maisha mapya.

    Wataalamu wa uhamiaji kutoka Chuo Kikuu cha Oxford pia wamehoji kiasi cha fedha ambacho serikali itaweza kurejesha kupitia mfumo huo, wakibainisha kuwa viwango vya ajira na mapato miongoni mwa wakimbizi bado ni vya chini.

    Soma Zaidi:

  10. Lewandowski kujiunga na ligi ya MLS huku Bournemouth ikikataa kumuuza Alex Scott

    Robert Lewandowski

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Robert Lewandowski

    Na Beldeen Waliaula

    Mwandishi BBC Swahili

    Robert Lewandowski amejiunga na timu ya mpira ya Chicago Fire akipewa mkataba wa miaka miwili baada ya kuondoka Barcelona.

    Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 37 kutoka Poland, amecheza kwa muda wa miaka minne kwenye ligi ya La Liga, ambapo mkataba wake ulimalizika mwishoni mwa ligi hiyo.

    AC Milan na ligi ya Saudi Pro League wamekuwa wakimmezea mate mshambuliaji huyo huku akitarajiwa kuwa miongoni mwa wachezaji wanaolipwa fedha nyingi sana katika ligi ya MLS.

    Ujio wake utaipiga jeki mji wa Chicago ambao una wakaazi wengi kutoka Poland.

    Lewandoski amecheza misimu 12 katika ligi ya Ujerumani ya Bundesliga kupitia timu ya Borussia Dortmund na Bayern Munich, na kushinda taji 10 za ligi pamoja na kuiwezesha Bayern kutwaa ushindi wa ligi ya Champions League mwaka wa 2020.

    Kwingineko, Bournemouth wamekataa ombi la Arsenal la kumtaka Alex Scott, wakisema kiungo huyo wa kati hatauzwa kwa sasa.

    Timu hiyo iliyojinyakulia taji la Champions League imekuwa ikimtaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22, huku timu zingine kama Manchester City, Manchester United, Tottenham na Chelsea pia wakimmezea mate Scott.

    Timu ya Bournemouth imesema wataendelea kubaki na kiungo huyo wa kati na wana mipango ya kumuongezea mkataba wake kwa muda wa miaka miwili zaidi.

    Soma Zaidi:

  11. Zelensky amshutumu Putin kwa kukataa amani na kuchelewesha mipango ya vita

    d

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky, ameikosoa Urusi kwa kuendelea na vita, akisema Moscow imekuwa ikiahirisha mipango yake ya kijeshi na kukataa mapendekezo yote ya amani yaliyowasilishwa ili kumaliza mzozo huo.

    Kwa mujibu wa Reuters, Rais Volodymyr Zelensky, amesema Kremlin imeweka na kuahirisha mara 15 muda wake wa kujitwalia eneo la mashariki la Donbas katika kipindi cha zaidi ya miaka minne ya vita.

    Kauli za Zelensky zilikuwa jibu kwa matamshi ya Rais wa Urusi, Vladimir Putin, ambaye siku moja kabla alikuwa amekataa kile alichokitaja kuwa pendekezo la Ukraine la kusitisha mashambulizi ya masafa marefu na kupunguza mapigano.

    Soma zaidi;

  12. Morocco yatinga 16 bora kwa penalti

    g

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Michuano ya Kombe la dunia imeendelea kushuhudia matokeo ya kushtua baada ya Morocco kutinga hatua ya 16 bora kwa kuiondoa Uholanzi kwa mikwaju ya penati kufuatia sare ya 1-1 iliyodumu hadi baada ya dakika 120.

    Morocco sasa imeungana na Brazil, Canada na Paraguay katika hatua ya 16 bora, ikivunja rekodi ya Uholanzi ya kutofungwa na timu ya Afrika katika michuano hiyo.

    Katika mechi nyingine ya kusisimua, mabingwa mara nne wa dunia Ujerumani wameaga mashindano hayo baada ya kufungwa na Paraguay kwa mikwaju ya penati 4-3, kufuatia sare ya 1-1 iliyodumu hadi mwisho wa dakika 120.

    Ujerumani haikuwahi kupoteza mechi kwa penati kwenye kombe la dunia.

    Mshambuliaji wa Arsenal, Kai Havertz, pamoja na mshambuliaji wa Newcastle United, Nick Woltemade, walikosa penati zao baada ya kudakwa na kipa wa Paraguay, Orlando Gill.

    Maelezo zaidi:

  13. Trump asema mazungumzo ya Doha ni muhimu huku Iran ikisema hakuna mkutano uliopangwa

    g

    Chanzo cha picha, Bloomberg via Getty Images

    Rais wa Marekani Donald Trump ametangaza mazungumzo mapya kati ya wawakilishi wa Marekani na Iran mjini Doha, akisema kuwa mazungumzo hayo "yanaweza kuwa muhimu".

    Hata hivyo, Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imekanusha kuwepo kwa mpango wowote wa mazungumzo katika siku za karibu, ikisema safari ya wawakilishi wake kwenda Doha inalenga kufuatilia kuachiwa kwa mali za Iran zilizogandishwa.

    Rais wa Iran, Masoud Pezeshkian, amesema dola bilioni sita kati ya dola bilioni 12 za mali za Iran zilizogandishwa zitaachiliwa na hivi karibuni zitapatikana kwa serikali.

    Wakati huo huo, Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imejibu kauli za Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron kwa kusisitiza kwamba shughuli za kuondoa mabomu ya baharini katika Mlango wa Hormuz zitafanywa na Iran pekee.

    Maelezo zaidi:

  14. Hujambo na karibu kwa matangazo ya moja kwa moja ya tarehe 30/06/2026.