Tetesi za Soka Ulaya: Liverpool, Man Utd 'zatoana roho' kwa Wharton

Chanzo cha picha, Getty Images
Liverpool wameungana na Manchester United katika mbio za kumsajili kiungo wa England, Adam Wharton, kutoka Crystal Palace, ambao wanahitaji angalau pauni milioni 80 kumuuza mchezaji huyo mwenye miaka miaka 22. (Talksport)
Tottenham Hotspur wamefikia makubaliano ya awali ya kumsajili beki wa Argentina, Marcos Senesi, msimu wa joto, ambapo mkataba wake unamalizkka na anatarajiwa kuondoka AFC Bournemouth. Hata hivyo, dili hilo linategemea Spurs kusalia ligi kuu. (Talksport)
Newcastle United wako tayari kusikiliza ofa kwa ajili ya mshambuliaji Yoane Wissa, 29, licha ya kumnunua kutoka Brentford kwa pauni milioni 50 msimu uliopita. (The I)
Arsenal wanavutiwa na winga mwenye miaka 16 wa timu za vijana wa England, Jeremy Monga, anayekipiga katika klabu ya Leicester City. (Telegraph)
Kocha wa zamani wa Liverpool, Jurgen Klopp, hayupo kwenye orodha ya makocha wanaotarajiwa kuchukua mikoba Real Madrid msimu wa joto. (El Chiringuito)

Chanzo cha picha, Getty Images
Klabu ya Bayern Munich ina nia ya dhati ya kumsajili winga wa Newcastle United, Anthony Gordon, lakini Newcastle wanataka karibu pauni milioni 80 kwa ajili ya mchezaji huyo wa England. (The I)
Beki wa kati wa West Ham United, Konstantinos Mavropanos, anatarajiwa kuondoka msimu huu wa joto huku Borussia Dortmund wakimhitaji, ingawa wana wasiwasi kuhusu bei yake. (Florian Plettenberg)
Beki wa Austria, David Alaba, anatarajiwa kuondoka Real Madrid mkataba wake utakapomalizika msimu huu wa joto. (Fabrizio Romano)
Kiungo wa Real Madrid na timu ya taifa ya Hispania, Dani Ceballos, anawindwa na klabu ya Uholanzi, Ajax. (AS)
Rais wa heshima wa Bayern Munich, Uli Hoeness, angependa kipa Manuel Neuer aendelee kubaki klabuni kwa mwaka mmoja zaidi ili kumlea na kumsaidia kipa chipukizi Jonas Urbig. (Sky Sports Germany)













