Jeshi la Iran: Tuko tayari kwa vita vya muda mrefu

Jeshi la Iran limesema kuwa Jamhuri ya Kiislamu iko tayari kwa mapambano ya muda mrefu na kuendelea na operesheni zake.

Ruka Video uendelee
  • xx
  • Besigye
  • .
  • xx
  • xx
  • xx
  • Lungu
  • xx
  • xx
  • d
  • s
  • a
  • Sonko
  • xx
  • xx
  • xx
  • xx
  • xx
  • Dangote
  • Lydia Wanjiku

Moja kwa moja

Na Mariam Mjahid

  1. Jeshi la Iran: Tuko tayari kwa vita vya muda mrefu

    Jeshi la Iran

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Jeshi la Iran limesema kuwa Jamhuri ya Kiislamu iko tayari kwa mapambano ya muda mrefu na kuendelea na operesheni zake.

    Katika mahojiano na Shirika la Habari la Mehr, Naibu Afisa Mtendaji wa jeshi, Alireza Sheikh alisema kuwa Iran inaweza kuwa mhusika mwenye ufanisi kwa kutumia nyenzo zake za nguvu, kutoa majibu yanayofaa, na hata kuchukua hatua za kuzuia mashambulizi kabla hayajatokea.

    Naibu mkuu wa wafanyakazi wa jeshi la Iran alitathmini mabadiliko ya maamuzi ya Donald Trump kuhusu kufanya mashambulizi zaidi ya kijeshi dhidi ya Iran, akizingatia uwezo wa Tehran. Alisema:

    “Busara za Iran kwenye ubao wa chess umeilazimisha Ikulu ya White House kuendelea kufafanua upya malengo yake ya kisiasa.”

    Bw. Sheikh pia alizungumzia mabadiliko ya mafunzo ya kijeshi ya Iran, kutoka msimamo wa kujilinda pekee hadi kwenye kuzuia mashambulizi na kuchukua hatua kwa ufanisi.

    Alisema uwezo wa Iran wa kutengeneza makombora na ndege zisizo na rubani ni miongoni mwa mambo makuu yanayoiwezesha kuendelea na operesheni za kijeshi kwa muda mrefu.

    Hapo awali, Mohammad Reza Naqdi, mshauri wa kamanda mkuu wa jeshi la Iran, alisema kuwa uamuzi wa kubadili kutoka mafunzo ya kujihami kwenda kwenye kushambulia ulikuwa tayari umefanywa, na kwamba mazingira sasa yako tayari kwa utekelezaji wake.

    Unaweza kusoma;

  2. Idadi ya waliofariki baada ya boti kuzama katika nchini Zimbabwe yafikia 44

    Kariba

    Chanzo cha picha, AFP via Getty Images

    Takribani watu 44 wamefariki baada ya boti kuzama katika Ziwa Kariba nchini Zimbabwe siku ya Jumanne, polisi wamesema.

    Feri hiyo ilikuwa na uwezo wa kubeba abiria 90 na wafanyakazi watano, lakini afisa wa ziwa aliripoti kwamba watu 120, wakiwemo watoto 12, walikuwa ndani ya feri hiyo.

    Polisi walisema chombo hicho kilipigwa na wimbi kubwa na kupinduka. Video zilizosambazwa mtandaoni zinaonekana kuonesha sehemu ya chini ya feri ikiwa imepinduka na kuelea majini.

    Shughuli za utafutaji na uokoaji zinaendelea kwa nguvu zaidi. Kufikia sasa, watu 77 wameokolewa.

    Ziwa Kariba Linatumika kwa usafirishaji na uvuvi, na pia linazalisha umeme muhimu wa nguvu za maji kwa nchi zote mbili.

    Mapema, Mutsa Murombedzi, mbunge wa eneo hilo, alichapisha video kwenye X akionesha feri hiyo mwanzoni mwa safari. Alisema wakazi walikuwa wakivuka ziwa kuelekea mji wa Kariba, safari ambayo huchukua takriban saa tano.

    Murombedzi aliandika: “Tuna maswali mazito sana yanayohitaji majibu ya kweli. Maafisa lazima watoe idadi sahihi ya watu waliokuwa ndani ya feri.”

    Kitengo cha Ulinzi wa Raia cha Zimbabwe (CPU) kilisema rekodi za mauzo ya tiketi zinaonesha kwamba abiria watu wazima 114 walikuwa ndani ya feri hiyo. Kiliongeza kuwa huenda pia kulikuwa na idadi isiyojulikana ya watoto ambao walikuwa chini ya umri wa kulipiwa tiketi.

  3. Walowezi wa Israel wazingira familia za Wapalestina katika Ukingo wa Magharibi

    Walowezi wa Israel wazingira familia za Wapalestina katika Ukingo wa Magharibi

    Walowezi wa Israel wamekuwa wakizingira familia mbili za Wapalestina katika nyumba zao katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu tangu Jumapili.

    Familia hizo zimesema kwamba akiba yao ya mahitaji muhimu inaendelea kuisha, huku mashirika ya kutetea haki za binadamu yakizitaka mamlaka kuingilia kati.

    Jumatano, iliripotiwa kwamba vikosi vya usalama vya Israel viliondoka katika kituo cha walowezi wa Kiyahudi katika kijiji cha Qusra, karibu na Nablus, baada ya mapigano kati yao na kundi la walowezi wenye msimamo mkali. Inasemekana kwamba walowezi kadhaa bado wako katika eneo hilo.

    Baada ya wamiliki wa nyumba hizo za Wapalestina kutoa taarifa yao ya kwanza kwa jeshi la Israel, wanajeshi wa kwanza waliofika eneo hilo walinaswa kwenye video wakisali pamoja na walowezi.

    Familia za Abu Ridi na Hassan zimekuwa zikichapisha ujumbe kwenye mitandao ya kijamii kuomba msaada baada ya maji na umeme kukatwa, huku akiba yao ya chakula ikianza kuisha.

    Haya yanakuja wakati afisa wa ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa alipoliambia Baraza la Usalama la UN mjini New York siku ya Jumanne kwamba “Ukingo wa Magharibi umefikia hatua ya hatari sana.”

    Makazi yote ya walowezi yanachukuliwa kuwa kinyume cha sheria chini ya sheria za kimataifa. Vituo vya walowezi huanzishwa bila idhini rasmi ya serikali ya Israel.

    Picha kutoka kamera za usalama za Wapalestina zinaonesha walowezi wakibomoa ukuta nje ya nyumba ya familia ya Abu Ridi Jumapili jioni na kutumia mawe yaliyobomoka kuzuia barabara.

    Hali hiyo iliwaacha watu saba,wakiwemo wasichana wawili wadogo wakiwa hawawezi kutoka kwenye nyumba zao, huku Wapalestina wengine pia wakishindwa kuwafikia.

    Familia hizo zinaishi katika eneo linalojulikana kama Area B, sehemu ya Ukingo wa Magharibi ambayo iko chini ya utawala wa kiraia wa Wapalestina lakini udhibiti wa kiusalama wa Israel.

    Unaweza kusoma;

  4. Mhalifu wa mauaji kwa ajili ya ngono ahukumiwa kifungo cha maisha jela

    .

    Chanzo cha picha, Julia Quenzler

    Mhalifu wa mauaji kwa ajili ya ngono ambaye aliwaua wanawake wawili na kumbaka wa tatu amehukumiwa kifungo cha maisha jela.

    Simon Levy, mwenye umri wa miaka 40, alimuua bibi Carmenza Valencia-Trujillo, mwenye umri wa miaka 53, mwezi Machi 2025, na mama wa watoto wanne Sheryl Wilkins, mwenye umri wa miaka 39, mwezi Agosti mwaka huo huo.

    Matendo yake ya uhalifu yalizidi kuwa mabaya, yakianza na kuwashambulia kingono wanawake hadi kufikia mauaji ya wanawake wawili.

    Aliwanyonga wanawake wote wawili hadi kufariki katika mashambulizi yaliyokuwa na msukumo wa kingono. Bi. Valencia-Trujillo aligunduliwa katika jengo la vyumba lililokuwa karibu kuachwa kabisa kwenye eneo la Aylesbury, kusini-mashariki mwa London, huku Bi. Wilkins akipatikana nyuma ya ukuta wa maegesho ya magari karibu na Tottenham High Road, kaskazini mwa London.

    Kufikia wakati Levy alipogeuka kuwa muuaji, tayari alikuwa amemfanyia mwanamke wa tatu ubakaji wa kikatili katika maegesho hayo hayo ambako baadaye mwili wa Bi. Wilkins ulipatikana.

    Mwathirika huyo aliyenusurika alikuwa tayari ameiambia polisi alipokuwa mshambuliaji wake.

  5. Raia watatu wa Pakistan wameuawa katika shambulio la Houthi

    Mpiganaji

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Waziri wa Mambo ya Nje wa Pakistan, Mohammad Ishaq Dar, alitangaza Jumatano kwamba raia watatu wa Pakistan waliuawa katika shambulio lililofanywa na wapiganaji wa Houthi dhidi ya meli katika Bahari ya Shamu.

    Katika ujumbe aliouchapisha kwenye ukurasa wake wa X, Ishaq Dar alisema: “Raia watatu wa Pakistan wamepoteza maisha, huku mtu mmoja akijeruhiwa katika tukio hili.”

    Kauli yake ilitolewa siku moja baada ya walinzi wa pwani wa Yemen kuthibitisha kwamba takribani watu sita waliuawa katika shambulio lililofanywa na wapiganaji wa Houthi dhidi ya boti iliyokuwa karibu na pwani ya nchi hiyo.

    Hadi sasa, hakuna taarifa zaidi zilizotolewa kuhusu vifo hivyo wala hali ya meli iliyoshambuliwa.

    Unaweza kusoma;

  6. Mkuu wa zamani wa Mossad: Iran haijafikia hatua ya kutengeneza bomu la nyuklia

    maeneo ya Urani

    Chanzo cha picha, PLANET LABS

    Mkuu wa zamani wa Taasisi ya Ujasusi na Operesheni Maalum (Mossad) amesema kuwa shirika la ujasusi la Israel lilikuwa likifuatilia kwa karibu kituo cha nyuklia cha chini ya ardhi cha Fordow nchini Iran.

    Alieleza shambulio la Marekani dhidi ya kituo hicho kuwa “kutimia kwa ndoto zangu zote.”

    Mkuu huyo wa zamani wa Mossad, Yossi Cohen, alisema katika mkutano uliofanyika Jumanne kwamba idara ya ujasusi ya Israel ilikuwa imefanya uchunguzi wa karibu na wa kina kuhusu kituo cha nyuklia cha chini ya ardhi cha Fordow nchini Iran.

    Afisa huyo wa zamani wa ujasusi wa Israel hakutoa maelezo zaidi kuhusu alichomaanisha kwa kauli hiyo.

    Pia alizungumzia urani ya Iran iliyorutubishwa kwa kiwango cha asilimia 60, akisema kwamba licha ya kiwango hicho cha juu cha urutubishaji, haimaanishi kwamba utengenezaji wa silaha ya nyuklia uko karibu kutokea.

    “Urani iliyorutubishwa kwa asilimia 60 bado iko mbali sana na kutengeneza bomu,” alisema.

    Mwaka jana, Marekani ilishambulia kituo cha nyuklia cha Fordow kwa kutumia ndege za mabomu za kisasa pamoja na mabomu maalum yenye uwezo wa kupenya ngome na miundombinu iliyo chini ya ardhi.

    Unaweza kusoma;

  7. Iran yatishia kushambulia vituo vya Marekani na washirika wake

    S

    Chanzo cha picha, Tasnim news agency

    Afisa wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran, Hossein Mohebi, amesema Marekani na washirika wake watakabiliwa na mashambulizi dhidi ya vituo muhimu iwapo Iran itashambuliwa tena.

    Mohebi ameonya kuwa Iran inaweza kulenga mitambo ya kuzalisha umeme, njia za kusambaza nishati na miundombinu mingine muhimu ya Marekani na washirika wake.

    Amesema pia sehemu kubwa ya mitandao ya intaneti duniani inaweza kuwa katika hatari iwapo Iran itashambuliwa tena.

    Aidha, Mohebi amesema kwa sasa hakuna meli za Marekani katika Ghuba ya Uajemi.

    Kauli ya afisa huyo wa IRGC imekuja saa chache baada ya Rais wa Marekani Donald Trump kusema hana imani na Iran, akidai kuwa Tehran imekuwa ikimdanganya.

    Trump pia amesisitiza kuwa Mlango wa Hormuz uko chini ya udhibiti wa Marekani na kwamba ni wa Marekani.

    Soma Zaidi Hapa:

  8. Ilhan Omar ashinda kura za mchujo wa chama cha Democratic Minnesota

    G

    Chanzo cha picha, Reuters

    Mwakilishi wa Marekani Ilhan Omar ameshinda kwa kishindo mchujo wa chama cha Democratic katika jimbo la Minnesota, baada ya kupata zaidi ya asilimia 80 ya kura.

    Omar, ambaye ni mbunge wa Democratic kwa muhula wa nne, anawakilisha eneo la 5 la uchaguzi linalojumuisha sehemu kubwa ya Minneapolis. Aliwashinda wapinzani wake kadhaa katika kura za mchujo zilizofanyika Jumanne, kwa mujibu wa makadirio ya vyombo vya habari nchini Marekani.

    Baada ya zaidi ya asilimia 95 ya kura kuhesabiwa, matokeo yasiyo rasmi yalionyesha Omar akiongoza kwa kura 122,640. Julie Trang Le alifuata kwa kura 10,201, huku Latonya T. Reeves akipata kura 9,131, kwa mujibu wa takwimu zilizoripotiwa na The New York Times.

    Wagombea wengine waliokuwa wakichuana na Omar ni Abena McKenzie na Nate Schluter. Le ni mwendesha mashtaka wa zamani wa serikali ya Marekani.

    Omar aliendesha kampeni yake bila kuungwa mkono na AIPAC, kundi la ushawishi linalounga mkono Israel.

    Ushindi huo unamweka Omar katika nafasi nzuri ya kutetea kiti chake katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Novemba.

    Katika mchujo wa Republican kwa kiti hicho hicho, John Nagel alitarajiwa kushinda kwa asilimia 52.1 ya kura.

    Omar aliingia katika Bunge la Marekani mwaka 2019, na kuwa Mmarekani wa kwanza mwenye asili ya Somalia kuchaguliwa katika Bunge hilo.

    Ameibuka kuwa mkosoaji mkubwa wa Rais Donald Trump na mara kwa mara amepinga sera za utawala wake kuhusu uhamiaji.

    Ukosoaji wake umeongezeka kufuatia operesheni ya utekelezaji wa sheria za uhamiaji nchini Minnesota, ambako raia wawili wa Marekani wameuawa kwa kupigwa risasi katika matukio mawili tofauti.

    Soma Zaidi:

  9. Watu 15 wafa maji baada ya boti kupinduka Ziwa Kariba nchini Zimbambwe

    d

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Takriban watu 15 wamekufa maji na wengine 27 hawajulikani walipo baada ya feri iliyokuwa imebeba abiria kupinduka katika Ziwa Kariba nchini Zimbabwe, kwa mujibu wa Kitengo cha Ulinzi wa Raia.

    Boti hiyo ilipinduka Jumanne baada ya kukumbwa na mawimbi makubwa, huku watu wasiopungua 77 wakiokolewa, shirika hilo limesema.

    Boti hiyo hutumika kusafirisha watu kati ya mji wa Kariba kaskazini mwa nchi hiyo na visiwa kadhaa pamoja na maeneo ya uvuvi.

    Mamlaka zimesema feri hiyo ilikuwa imebeba watu zaidi ya uwezo wake wa abiria 90 ilipopinduka.

    Ingawa idadi kamili ya abiria na wafanyakazi bado haijathibitishwa, mamlaka zimesema taarifa za mauzo ya tiketi zinaonyesha kuwa kulikuwa na abiria watu wazima 114 pamoja na wafanyakazi watano.

    Aidha, huenda kulikuwa na watoto ambao hawakuwa wamefikia umri wa kulipia tiketi na hivyo idadi yao haijajulikana.

    Jeshi la Polisi nchini Zimbabwe limesema shughuli za uokoaji zinaendelea.

    Shirika la utangazaji la taifa, ZBC, limeonyesha picha za boti za mwendo kasi zikielekea kwenye feri hiyo iliyopinduka, huku helikopta ikiruka juu ya ziwa.

    Timu ya wapiga mbizi pia imetumwa kufanya shughuli za utafutaji na uokoaji katika ziwa hilo kubwa.

    Pia unaweza kusoma:

  10. Cristiano Ronaldo amuoa Georgina Rodríguez baada ya miaka 10

    d

    Chanzo cha picha, Anadolu via Getty Images

    Nyota wa soka Cristiano Ronaldo amemuoa mpenzi wake wa muda mrefu, mwanamitindo na mshawishi Georgina Rodríguez, nchini Ureno.

    Ronaldo alichapisha picha kwenye akaunti yake ya Instagram ikionyesha mikono miwili, unaodhaniwa kuwa wake ukiwa juu ya wa mke wake, huku wote wakiwa wamevalia pete za ndoa.

    Vyombo vya habari nchini Ureno vimeripoti kuwa wawili hao walifunga ndoa tarehe 11 Agosti katika mji wa pwani wa Cascais, karibu na Lisbon, huku watoto wao watano wakihudhuria.

    Picha hiyo ilipata uungwaji mkono wa mitandaoni milioni tatu ndani ya dakika 30 baada ya kuchapishwa.

    Ronaldo na Rodríguez wamekuwa pamoja kwa miaka 10, baada ya kukutana katika duka la Gucci mjini Madrid, ambako Rodríguez alikuwa akifanya kazi. Wakati huo Ronaldo alikuwa akiichezea Real Madrid.

    Wawili hao walitangaza uchumba wao tarehe 11 Agosti mwaka jana.

    Ronaldo amefunga karibu mabao 1,000 katika maisha yake ya soka, akichezea Sporting Lisbon, Manchester United, Real Madrid, Juventus, Al Nassr ya Saudi Arabia na timu ya taifa ya Ureno.

    Hivi karibuni alishiriki katika Kombe lake la Dunia la sita, rekodi ya ushiriki katika fainali za Kombe la Dunia kwa upande wa wanaume, ambayo anaishikilia pamoja na Lionel Messi wa Argentina.

    d

    Chanzo cha picha, Ronaldo Instagram account

  11. Mwanamke aliyezikwa na vifusi aokolewa akiwa hai baada ya saa 36

    g

    Chanzo cha picha, Reuters

    Kwa mujibu wa Idara ya Zimamoto ya Bogotá, timu za uokoaji zimemtoa mwanamke akiwa hai baada ya kunaswa chini ya vifusi kwa saa 36 katika mji wa Pereira.

    Waziri wa Mambo ya Ndani wa Colombia, Rodrigo Lara, amesema katika ujumbe kwenye mtandao wa X kwamba Daniela Largo Sanchez, mwenye umri wa miaka 32, alipatikana chini ya vifusi vya hoteli.

    Mwanamke huyo alihamishiwa mara moja katika kituo cha afya cha eneo hilo, ambako anaendelea kupatiwa matibabu.

    Kwa mujibu wa Rais Abelardo de la Espriella, waokoaji mjini Pereira bado wanaendelea kuwatafuta zaidi ya watu 40 ambao hawajulikani walipo.

    Idadi ya waliofariki katika tetemeko la ardhi lililoikumba Colombia imefikia watu 181, huku vifo vingi vikiripotiwa katika miji ya Cali na Pereira.

    Tetemeko hilo lenye ukubwa wa 7.4 lilitokea saa 1:34 asubuhi kwa saa za nchini humo Jumatatu, na mitikisiko yake ilihisiwa katika maeneo makubwa ya magharibi mwa Colombia, huku mitetemeko midogo ikiendelea hadi Jumanne.

    Ingawa idadi rasmi ya vifo ni 181, mamlaka za eneo hilo zinasema huenda idadi hiyo ikaongezeka na kuvuka watu 240 kadiri shughuli za uokoaji zinavyoendelea.

    Rais wa Colombia Abelardo de la Espriella ametangaza hali ya dharura nchini humo.

    Akitoa taarifa kuhusu hali ilivyo mjini Pereira, mojawapo ya maeneo yaliyoathirika zaidi, rais amesema watu wapatao 2,600 wamejeruhiwa na takriban watu 200 bado hawajulikani walipo.

    Aidha, amesema zaidi ya nyumba 1,100 zimeharibiwa kabisa, huku zaidi ya nyumba 8,000 zikiharibiwa kwa viwango tofauti.

    Soma Zaidi Hapa:

  12. Idadi ya visa vya Ebola yafikia 4,449 nchini DRC

    g

    Chanzo cha picha, Anadolu via Getty Images

    Idadi ya visa vilivyothibitishwa vya Ebola katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, imeongezeka hadi 4,449, huku watu 2,061 wakifariki, kwa mujibu wa takwimu za serikali zilizotolewa Jumanne usiku.

    Idadi ya waliofariki imeongezeka kwa asilimia 8.7 ndani ya siku mbili, hali inayoonyesha kasi ya kuongezeka kwa mlipuko huo.

    Haya yanajiri baada ya Shirika la Afya Duniani WHO kutangaza kuwa ebola 'inasambaa kwa kiwango cha kutisha'.

    Maambukizi ya sasa yamesababishwa na aina adimu ya virusi vya Ebola inayojulikana kama Bundibugyo, ambayo husababisha vifo kwa takribani robo ya watu wanaoambukizwa.

    Linalotia wasiwasi wanasayansi ni kuwa aina hii ya Ebola haina tiba.

    Maelezo zaidi:

  13. Wasyria washerehekea baada ya aliyekuwa rais Bashar Al Assad kuhukumiwa kifo

    D

    Chanzo cha picha, Reuters

    Wakazi wa mji wa Idlib nchini Syria wamekusanyika kusherehekea baada ya mahakama kumhukumu kifo rais wa zamani wa nchi hiyo, Bashar al Assad.

    Picha za mitandaoni zinaonyesha watu wakishangilia katika mitaa ya Idlib, huku baadhi yao wakipanda magari na wengine wakiimba na kusherehekea uamuzi huo wa mahakama.

    Haya yanajiri baada ya Mahakama ya Syria kumhukumu kifo dikteta aliyeondolewa madarakani Bashar al-Assad licha ya kutokuwa mahakamani, baada ya kumpata na hatia kwa makosa ya kivita na uhalifu dhidi ya binadamu wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo.

    Assad alikimbilia Urusi pamoja na familia yake baada ya utawala wake kupinduliwa mwezi Desemba mwaka 2024, jambo lililohitimisha utawala wa familia yake uliodumu kwa miongo mitano.

    Katika kesi hiyo hiyo, mahakama pia ilimhukumu kifo Atef Najib, binamu yake Assad na aliyekuwa mkuu wa usalama wa kisiasa katika jimbo la Deraa kusini mwa Syria.

    Alionekana akiwa ndani ya kizimba mahakamani wakati jaji akisoma hukumu yake. Jimbo la Deraa linachukuliwa kwa kiasi kikubwa kuwa mahali ambapo vuguvugu la uasi dhidi ya utawala wa Assad lilianzia.

    Mnamo Machi 2011, kukamatwa na madai ya kuteswa kwa kundi la vijana walioshtakiwa kwa kuandika maandishi ya kupinga serikali kwenye kuta kulichochea maandamano jijini humo, ambayo yalikabiliwa na ukandamizaji mkali kutoka kwa vikosi vya usalama.

    Hatua hiyo ilichochea maandamano nchi nzima yaliyogeuka kuwa vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyosababisha vifo vya mamia ya maelfu ya watu.

    Serikali ya mpito ya Syria ilianza kuwashtaki maafisa waliohusishwa na utawala wa Assad ambao ulitawala nchi hiyo kwa zaidi ya miaka 50, mapema mwaka huu.

    Najib ni mmoja wa maafisa wa ngazi ya juu kabisa kufikishwa mahakamani.

    Pia Unaweza kusoma:

  14. Trump asema haiamini Iran na sasa Marekani inadhibiti Hormuz kikamilifu

    S

    Chanzo cha picha, Reuters

    Rais wa Marekani Donald Trump amesema Jumatano kwamba hana imani na Iran, akisisitiza kuwa Marekani ina udhibiti kamili wa Mlango wa Hormuz.

    “Nitakuwa mtu wa mwisho kabisa kuamini Iran, wamekuwa wakinidanganya kila mara.”

    Awali, Kamandi Kuu ya Jeshi la Marekani, CENTCOM, ilisema kuwa imeizuia na kuifanya meli iliyokuwa ikielekea katika bandari ya Iran ishindwe kuendelea na safari.

    Katika taarifa iliyochapishwa kwenye mtandao wa X, CENTCOM ilisema meli hiyo iliyokuwa na bendera ya Panama ilikuwa ikijaribu kupita katika Ghuba ya Oman.

    Kwa upande mwingine, katibu mpya wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran, Mohsen Rezaei, amesema:

    “Mlango wa Hormuz hautafunguliwa hadi Marekani ibadili msimamo wake na ikubali masharti ya Iran.”

    Katika siku mbili zilizopita, Iran na Marekani zimeongeza ukali wa kauli zao kuhusu mzozo huo.

    Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran, Mohsen Rezaei, amesema Jumanne kuwa Mlango wa Hormuz utaendelea kufungwa hadi Marekani ikubali masharti ya Iran ya kumaliza vita.

    Masharti hayo ni pamoja na kuachiliwa kwa mali za Iran zilizogandishwa na kusitishwa kwa vita katika maeneo mbalimbali ya Mashariki ya Kati, likiwemo Lebanon na Gaza.

    Kauli hiyo imekuja baada ya Rais Trump Jumatatu kuitaka Iran ilipe fidia kwa watu waliouawa katika vita, mashambulizi na maandamano katika kipindi cha miaka 50 iliyopita.

    Katika kipindi chote cha mzozo huo, kauli za Trump zimekuwa zikibadilika kati ya kutishia kuongeza mashambulizi na kusema kuwa makubaliano yako karibu kufikiwa.

    Katika mahojiano yaliyorushwa Jumatatu usiku, Trump amesema hali ya sintofahamu inaweza kuendelea kwa muda, akisema huenda akaamua “kusubiri na kuona kitakachotokea.”

    Soma Zaidi:

  15. Trump asema alitumia ndege ya kijeshi kwa kuhofia Iran

    g

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Rais wa Marekani Donald Trump amethibitisha kuwa alibadilisha ndege kwa siri alipokuwa akiondoka kwenye mkutano wa NATO nchini Uturuki mwezi uliopita, kutokana na uwezekano wa kuwepo kwa tishio la kiusalama.

    “Nafuata maelekezo ya Usalama wa Taifa na jeshi. Walitaka nipande ndege nyingine, kwa hiyo nalazimika kufanya wanachoniambia,” Trump aliwaambia waandishi wa habari Jumanne.

    Taarifa hiyo imekuja baada ya kuripotiwa kuwa Trump alipanda ndege ya Air Force One tarehe 8 Julai mbele ya kamera za televisheni, kabla ya kuhamishiwa kwenye ndege ya kijeshi kwa msaada wa gari la kubeba chakula.

    Mabadiliko hayo ya ghafla yameibua maswali kuhusu iwapo watu waliokuwa kwenye ndege iliyotumika kama chambo waliwekwa katika hatari. Hata hivyo, Trump amesema Jumanne kuwa ndege ya kijeshi aliyopanda ilikuwa katika “hatari kubwa zaidi”.

    Maafisa wameiambia CBS News, mshirika wa BBC nchini Marekani, kuwa Marekani ilikuwa imegundua tishio la kuaminika kutoka Iran la kurusha kombora kuelekea ndege hiyo.

    Waandishi wa habari na baadhi ya wafanyakazi wa Ikulu ya Marekani waliokuwa ndani ya ndege hiyo hawakujua kuwa Trump alikuwa ameondolewa kwa siri kupitia mpango maalumu wa kupotosha, kutokana na tishio linalodaiwa kutoka Iran.

    Soma Zaidi:

  16. Hujambo na karibu kwa matangazo ya moja kwa moja ya tarehe 12/08/2026.