Tetesi za Soka Ulaya Ijumaa: Mustakabali wa Rashford Barcelona haujulikani

Chanzo cha picha, Getty Images
Barcelona hawana uhakika kama watailipa Manchester United kipengee cha ununuzi cha euro milioni 30 ili kumsajili mshambuliaji wa Uingereza Marcus Rashford, 28, kwa mkataba wa kudumu. (Marca - kwa Kihispania),
Winga wa Newcastle United na England Anthony Gordon yuko tayari kuondoka klabu hiyo msimu huu wa joto na Bayern Munich ikivutiwa. (Telegraph - usajili unahitajika)
Arsenal pia imejiunga na kinyang'anyiro cha kumsajili Gordon huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 akipendelea kuhamia London kuliko jiji lingine lolote. (Sun)
Manchester City na Barcelona wanaongoza mbio za kumsajili mshambuliaji wa Palmeiras mwenye umri wa miaka 16 Eduardo Conceicao. (Mail + - usajili unahitajika)
Newcastle inajiandaa kwa msimu wa joto wenye shughuli nyingi huku wachezaji saba wa kikosi cha kwanza wakihusishwa na tetesi za kuondoka St James' Park. (Sun)
Wachezaji tisa wa Liverpool wanatarajiwa kuhama klabu hiyo majira ya kiangazi, akiwemo kiungo wa Argentina Alexis Mac Allister, 27 na beki wa Uingereza Joe Gomez, 28. (Telegraph - usajili unahitajika)
Jurgen Klopp na Mauricio Pochettino wanawania kuwa meneja wa Real Madrid Alvaro Arbeloa akitimuliwa. (mail)

Chanzo cha picha, Getty Images
Beki wa Uingereza Matt Targett, 30, ambaye anakipiga Middlesbrough kwa mkopo kutoka Newcastle, anafuatiliwa na Everton na Leeds. (Team talk)
Tottenham iko tayari kumuuza Conor Gallagher, 26, huku vilabu kadhaa vya Ligi ya Premia vikumuwania kiungo huyo wa kati wa Uingereza, ambaye alijiunga na Spurs mwezi Januari. (Football Insider)
Beki wa Uingereza Levi Colwill, 23, anatarajiwa kujiunga na mchezaji mwenzake wa Ecuador Moises Caicedo, 24, kusaini mkataba mpya wa muda mrefu na Chelsea. (Times - usajili unahitajika)
AC Milan wanavutiwa na mshambuliaji wa Serbia Dusan Vlahovic, 26, ambaye mkataba wake na Juventus unamalizika msimu wa joto. (Gazzetta dello Sport - kwa Kiitaliano)
Klabu ya Marseille ya Ufaransa ina nia ya kumsajili beki wa Morocco Adam Aznou, 19, ambaye bado hajaichezea Everton kwenye Ligi ya Premia. (Team talk )















