Marekani iko tayari kuanza tena mashambulizi dhidi ya Iran ikiwa hakuna makubaliano - Waziri wa Ulinzi
Marekani iko tayari kuanzisha upya mashambulizi dhidi ya Iran ikiwa makubaliano hayatafikiwa, Waziri wa Ulinzi Pete Hegseth amesema leo Jumamosi, huku wapatanishi kutoka Marekani na Iran wakijitahidi kupunguza tofauti kubwa zinazozuia makubaliano.
"Uwezo wetu wa kuanza upya inapobidi...tunao na tuko tayari sana," Hegseth alisema akiwa Singapore.
"Hifadhi zetu ziko imara zaidi kwa hilo, huko na kote ulimwenguni, kwa hivyo tumejipanga vizuri," ameongeza.
Hegseth, akizungumza hayo katika kongamano kuu la Asia kwa viongozi wa ulinzi, wanajeshi na wanadiplomasia, alisema Marekani haijalipa kisogo eneo la Asia-Pasifiki.
"Tunaweza kufanya mambo mawili kwa wakati mmoja. Tunaongeza nguvu zaidi katika kituo chetu cha ulinzi ili tuwe na silaha mara 2, 3, 4 zaidi hivi karibuni ili kuhakikisha kwamba mipango yetu yote (ya operesheni) inafadhiliwa ipasavyo kote ulimwenguni," alisema.
Hegseth alisema Rais Donald Trump alikuwa "mvumilivu" na anataka kufanya "makubaliano makubwa" ambayo yatahakikisha Iran haipati silaha.
Soma zaidi: