Tetesi za Soka Ulaya: Galatasaray yamtaka Martinelli wa Arsenal

Iliyochapishwa
Muda wa kusoma: Dakika 2

Galatasaray imewasilisha ofa ya euro milioni 45, sawa na takriban pauni milioni 38.4, kwa Gabriel Martinelli wa Arsenal. Mshambuliaji huyo wa Brazil ana umri wa miaka 25. (Florian Plettenberg)

Arsenal iko tayari kumuuza kiungo wa Hispania Martin Zubimendi kwa dau la kuanzia pauni milioni 77, huku Chelsea ikitajwa kuwa miongoni mwa timu zinazowania saini ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27. (Teamtalk)

Aston Villa imefanya mazungumzo na West Ham United kuhusu kumsajili beki wa kulia Aaron Wan-Bissaka. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 kutoka DR Congo anathamani ya pauni milioni 25. (The Athletic)

Kiungo wa Newcastle Joe Willock yuko tayari kujiunga na Beşiktaş, huku dau la euro milioni 20, sawa na takriban pauni milioni 17, likitajwa kuwa linaweza kutosha kukamilisha uhamisho wa Mwingereza huyo mwenye umri wa miaka 26. (Foot Mercato)

Newcastle pia inamfuatilia kiungo wa Brighton & Hove Albion, Carlos Baleba, 22, kutoka Cameroon, wakati klabu hiyo ikitafuta njia za kuimarisha safu yake ya kiungo baada ya kuondoka kwa Bruno Guimaraes na Sandro Tonali. (Daily Mail)

Ipswich Town inatarajiwa kukamilisha usajili wa Abdoul Ouattara, beki wa kulia na kiungo mwenye umri wa miaka 20, aliyezaliwa Ivory Coast, kutoka Strasbourg. (Sky Sports)

Aston Villa imeipa Bayern Munich ofa ya kumchukua kwa mkopo kiungo wa Ureno João Palhinha, 31, ikiwa na kipengele cha kumnunua moja kwa moja. Hata hivyo, Bayern inapendelea uhamisho wa moja kwa moja. (Florian Plettenberg)

Newcastle United inaendelea kwa kasi na mazungumzo ya kumsajili beki wa kulia Amar Dedic kutoka Benfica. Mchezaji huyo wa Bosnia na Herzegovina mwenye umri wa miaka 23 anakadiriwa kuwa na thamani ya karibu pauni milioni 25. (Daily Mail)

Hull City ina matumaini ya kukamilisha usajili wa kiungo Mjerumani Mert Komur kutoka FC Augsburg, licha ya ofa yake ya pauni milioni 10.2 kukataliwa kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21. (Teamtalk)

Hull City iko karibu kukamilisha usajili wa kudumu wa mshambuliaji Joe Gelhardt kutoka Leeds United. Mchezaji huyo Mwingereza mwenye umri wa miaka 24 alitumia misimu miwili iliyopita kwa mkopo Hull City. (Sky Sports)