Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za soka Ulaya: Liverpool inamtolea macho Camavinga
Liverpool wako mguu sawa kwa usajili baada ya Real Madrid kuonyesha utayari wa kumuuza kiungo wa Ufaransa, Eduardo Camavinga, 23, ambaye kwa muda mrefu amekuwa akiwaniwa na klabu hiyo ya Anfield. (L'Equipe)
Barcelona na Juventus ni miongoni mwa vilabu vinavyotaka kumsajili kiungo wa Manchester City na timu ya taifa ya Ureno, Bernardo Silva, 31, kwa uhamisho wa bure majira ya kiangazi. (Sky Sports)
Juventus wanaamini kufuzu michuano ya klabu bingwa Ulaya kutawaweka katika nafasi nzuri ya kumsajili kiungo wa Uruguay, Manuel Ugarte, 24, ambaye amewekewa thamani ya takriban pauni milioni 35 na klabu yake ya Manchester United. (Corriere dello Sport)
Arsenal wanaonekana kuwa mbele ya Liverpool katika kinyang'anyiro cha kumsajili winga wa RB Leipzig na Ivory Coast, Yan Diomande, 19. (Caught Offside)
Tottenham Hotspur hawataki kusikiliza ofa chini ya euro milioni 50 (pauni milioni 43.6) kwa ajili ya nahodha wao, beki wa Argentina, Cristian Romero, ambaye anawaniwa na Atletico Madrid. (Fichajes)
Endapo mshambuliaji wa Brazil, Vinicius Junior, 25, ataamua kuondoka Real Madrid, basi ataelekea Paris Saint-Germain au ligi kuu ya England. (ESPN)
Newcastle United watachuana na vilabu vingine Ulaya kumsajili beki wa Werder Bremen na timu ya taifa ya vijana ya Ujerumani (U21), Karim Coulibaly, 18. (Fabrizio Romano)
Liverpool na Manchester United wameongeza juhudi zao za kumsajili winga wa AS Monaco na Ufaransa, Maghnes Akliouche, 24. (Teamtalk)
Borussia Dortmund wanavutiwa na mchezaji wa RC Strasbourg na Ubelgiji, Diego Moreira, 21, lakini kuna kipengele kwenye mkataba kinachowawezesha Chelsea kumnunua tena mchezaji huyo. (Florian Plettenberg)
AS Roma wanawafukuzia wachezaji wawili wa FC Midtjylland, Dario Osorio, 22, na Franculino, 21, ambao thamani ya wote kwa ujumla ni euro milioni 55 (pauni milioni 48). (Gazzetta dello Sport)