Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tofauti ya viti vya ndege za kivita za Marekani na Urusi
Ndege za kivita za Urusi, kama vile Su-34 Fullback, hutumia viti ambavyo rubani hukaa kando ya rubani mwingine upande wa kushoto au kulia, ni tofauti na ndege za kivita za Marekani ambapo viti vya marubani kiko nyuma ya kiti kingine.
Mfumo huu wa viti vya Urusi husaidia kuboresha shughuli za marubani, kupunguza uzito wa ndege, na kusaidia marubani kukaa muda mrefu katika ndege wakati wa operesheni za masaa mengi.
Ndege za kivita za Marekani kama vile F-15E Strike Eagle au F/A-18F Super Hornet hutumia viti vya nyuma na mbele ili kulifanya umbo la ndege kuwa jembamba ili kupunguza ukinzani na hewa na kupelekea kupunguza mwendo angani.
Faida kubwa kwa ndege za kivita za Urusi ni kutoa kipaumbele kwa ushirikiano wa marubani na ndege kuwa na nafasi zaidi wawapo angani.
Viti vya ndege za Urusi
Katika kuboresha utendaji kazi wa marubani, marubani wote wawili na silaha zao hukaa karibu, na kuwaruhusu kutazama mbele na kufanya kazi pamoja kwa kutumia vifaa ambavyo viko mbele yao wote wawili.
Viti hivi huondoa hitaji la baadhi ya vifaa kuwepo viwili viwili kwa ajili ya afisa mwingine wa nyuma, katika ndege za kimarekani ambapo rubani mmoja huwa mbele na mwingine huwepo nyuma.
Katika suala la kuwalinda marubani, kukaa pembeni ya mwenzako huruhusu wahandisi kutengeneza mifumo ya kumlinda rubani na afisa anayeshughulikia silaha, ndani ya chumba kimoja chenye unene wa milimita 17.
Mfumo huu wa Urusi hupunguza uzito wa jumla wa ndege ikilinganishwa na mfumo wa Marekani wenye vyumba viwili vya marubani na afisa silaha, ambapo mhandisi hulazimika kuunda mifumo ya kuvilinda vyumba viwili tofauti.
Mfumo wa Urusi pia husaidia kwenye kupunguza uchovu kwa marubani, wakati wa doria ya masafa marefu na misheni za mashambulizi ambazo zinaweza kudumu hadi saa 10.
Mpangilio wa viti viwili vya kando kwa kando, yaani kulia na kushoto hutoa nafasi ya kutosha kwa huduma kama vile bomba la kujisaidia na nafasi ya kusimama na kujinyoosha, mambo ambayo ni muhimu katika kupambana na uchovu wa rubani.
Viti vya ndege za Marekani
Ndege za kivita za Marekani hutumia viti vya kuketi rubani mmoja nyuma ya mwingine, ili kuboresha kasi ya ndege, kudumisha utendaji kazi wa ndege, na kutoa uwezo maalum kwa marubani.
Katika kuongeza ufanisi wa anga, viti vya aina hii huruhusu ndege kuwa nyembamba zaidi, ambayo hupunguza kwa kiasi kikubwa mkinzano na anga na kuongeza kasi ya ndege na katika kugeuka, kushuka na kupanda.
Kwa misheni ngumu, ndege kama F-15E Strike Eagle au EA-18G Growler, mpangilio wa viti viwili vya nyuma na mbele humruhusu rubani kuzingatia tu suala la kuendesha ndege na kuepuka vitisho, huku Afisa wa Mifumo ya Silaha (WSO) aliye nyuma akishughulikia rada, kulenga kombora, na kushughulikia mifumo ya kielektroniki.
Ndege hizi ambazo huwa nyembamba, zinakuwa na nguvu zaidi kimuundo na huhimili zaidi mvuto wa dunia wakati wa kupaa na kugeuka, kuliko ndege zenye viti vya kulia na kushoto.