Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Kisiwa cha Marekani kinachotawaliwa na nyoka wa kigeni na buibui
Guam ina buibui mara 40 zaidi ya visiwa jirani - na idadi ya nyoka vamizi waharibifu sana, waliojaa katika misitu ambayo ni makazi ya ndege.
Miaka mitano iliyopita, Haldre Rogers alihudhuria mkutano katika kisiwa cha Guam – eneo lenye uchafu wa kijani kibichi huko magharibi mwa Bahari ya Pasifiki, karibu kilomita 2,492 (maili 1,548) kutoka Ufilipino.
Lakini ghafla sherehe hiyo ilikatishwa na mgeni ambaye hakualikwa.
Ilikuwa jioni, na nje kulikuwa na nyama ya nguruwe iliyochomwa - mabaki ya chakula cha jioni. Moto ulikuwa ukiwaka, Kila mtu alikuwa ameondoka kwa muda mfupi kwenda kuzungumza hapa na pale.
Waliporejea, kulikuwa na kiumbe chenye umbo la kahawia lililomzunguka nguruwe - kitu kinachong'aa chenye magamba, na macho ya wima na mdomo mpana.
Kiumbe huyo alikuwa akipasua vipande vya nyama ya nguruwe na kuvimeza vikiwa vizima - akizimeza polepole kwenye mwili wake uliopauka na kunyooka.
‘’Hakuwa nguruwe wa uzito wa kilo 181, lakini alikuwa nguruwe wa kuliwa kwenye karamu kubwa," anasema Rogers, profesa msaidizi katika Idara ya Uhifadhi wa Samaki na Wanyamapori katika chuo cha Virginia nchini Marekani, ambaye amekuwa akitafiti ikolojia ya Guam kwa miaka 22 iliyopita.
Mgeni asiye na adabu ya mezani alikuwa nyoka wa kahawia - mgeni asiyealikwa ambaye anadhaniwa kuletwa Guam katika miaka ya 1940, labda baada ya kupenya kwenye meli ya mizigo.
Kabla ya ujio wake, ndege wengi wa asili walikuwa wakifurahia kuishi katika misitu ya kisiwa hicho.
Lakini katika muda wa miongo minne tu baada ya nyoka huyo kuingia msituni humo, wawindaji hao wakali walikuwa wameanza kuwamaliza kila mmoja wao msituni.
Kati ya spishi 12, 10 sasa zimetoweka kwenye kisiwa hicho, huku mbili zilizobaki zikisalia kwenye mapango yasiyofikika na maeneo ya mijini.
Kwa vile sasa jamii ya ndege imeangamizwa kabisa, idadi ya nyoka hao milioni mbili katika eneo hilo la Guam - hakuna anayejua ni wangapi - watakusanya chochote wanachoweza kupata, ikiwemo panya, mijusi, au, katika tukio hili, mabaki ya binadamu.
‘’Ninamaanisha,watakula chochote’’anaeleza Henry Pollock, mkurugenzi mtendaji wa Southern Plains Land Trust, shirika la Colorado, ambaye hapo awali alisoma ikolojia ya Guam.
Kwa tauni itokanayo na nyoka hao wakali, na misitu ambayo haina kabisa urafiki,milio na miluzi ambayo hapo awali ilitawala mandhari yao ya sauti, Guam imekuwa maarufu kama mojawapo ya maeneo yenye uharibifu wa mazingira zaidi.
Lakini madhara ya nyoka katika kisiwa hicho yanaenea zaidi katika misitu yake ya kutisha isiyo na ndege.
Mtandao wa buibui
Rogers haogopi buibui - na ndivyo hivyo.
Katika Visiwa vya Mariana, kuna buibui wachache hasa katika msimu wa mvua, wakiwa na mwiba mkubwa hali ya hewa inapokauka.
Lakini sio Guam. Misitu ya kisiwa hicho kina buibui waliotanda karibia kila hatua unayopiga hukutana na mwingine.
Kuna buibui wakubwa wenye tumbo la manjano, na utando wao wa dhahabu,wenye ukubwa kama mkono wa binadamu; buibui wenye kutanda hema, ambao huweka nyuzi za hariri kwenye matundu ya miti.
Rogers anaita aina hiyo mtandao wa "condo", kwa sababu kila moja ni sawa na viumbe wenye miguu minane - wana mamia ya macho yanayometa.
"Huko Guam utando wa buibui huenda kutoka ngazi ya chini, hadi kwenye dari inaweza kuwa kila mahali," anasema.
Utapata wengi wa kike katika viwango tofauti vya mtandao huu wa buibui,na baadae walio wengi wa kiume wakizagaa jirani’’anaeleza Rogers.
Mara nyingi, msitu mzima unaonekana kama umefunikwa na utando wa buibui bandia kwa ajili ya Halloween. "Kiasi kwamba unapotembea kwa miguu, ni kawaida kwa mtu aliye mbele kuchukua fimbo ya buibui na kuangusha utando wanapopita ," anasema Rogers, "vinginevyo utafunikwa na utando wa buibui ... napenda. , lakini ni vigumu kuvuka."
Kila kunapokuwa na uwazi katika miti Eneo lote hilo litajazwa utando kutoka aina tofauti za buibui,wakivutia mwanga kutoka pande tofauti.
Juhudi hizi za pamoja zinaweza kuchukua nafasi ya ukubwa wa chumba kwa urahisi. "Nilikuwa na rafiki ambaye alikimbia na kujizungusha tu kwenye utando, anasema Rogers," alifanya hivyo ili kuwaogopesha watu aliokuwa nao." .
Wakati mmoja, msaidizi wa Rogers alijitolea kumsaidia huko msituni – baada ya kuingia mita kadhaa msituni alibadilisha mawazo yake. Na kusema, 'Hapana, siwezi kuendelea," anasema Rogers.
Hata bila buibui, ambao katika lugha ya asili ya Chamorro hujulikana kama sånye'ye', misitu ya chokaa ya Guam ingekuwa mahali pa kushangaza na hatari, kama pengine popote.
Ardhi ina udongo mdogo sana. Badala yake, mimea hukua moja kwa moja kwa kulazimisha mizizi yake kwenye mipasuko midogo iliyo kwenye miamba - msitu umekaa juu ya mwamba wa kale wa matumbawe ambao umesukumwa juu kwa mamilioni ya miaka na kufanya uwanda.
Vichwa vya matumbawe bado vinatapakaa kwenye msitu, na mahali ambapo mwamba umemomonyoka, kuna mashimo na mapango.
Nadhani jambo la kipekee ni, kama vile, ni vigumu sana kutembea kwa sababu - hebu fikiria kutembea kwenye miamba iliyochongoka," anasema Rogers.
Anapowapeleka wataalamu wapya kwa ajili ya uchunguzi, wanahitaji muda wa kuzoea eneo hili la mawe - anazungumza kuhusu watu kupata miguu ya baharini - kuweza kutembea bila kuzingatia kila hatua," anasema.
Kwa hivyo, Rogers alipoamua kufanya uchunguzi wa idadi ya buibui mnamo 2012, alijua itakuwa changamoto.
Mara zote kumekuwa na uvumi kwamba Guam yalikuwa makazi ya buibui pekee na hii huenda ndio sababu ya kukosekana kwa ndege,ambao kwa kawaida walipenda kula buibui.
Hata hivyo, Rogers anaelezea kuwa wakazi wa kisiwa hicho chenye takriban watu 180,000 hawasafiri hadi Visiwa vingine vya Kaskazini mwa Mariana - wakati kote ni sehemu ya jumuiya ya madola, ni Guam pekee ambayo ni eneo la Marekani.
Matokeo yake, kuna fursa ndogo ya kulinganisha. Na wanasayansi hawakuwahi kuangalia.
Imetafsiriwa na Martha Saranga