Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za soka Ulaya Jumanne: Villa waingia kwenye mbio za kumwania Pervis Estupiñán
Aston Villa wanamtathmini Pervis Estupiñán, Bruno Guimarães hauzwi, Inter Milan waachana na kumsajili Trevoh Chalobah.
Beki wa kushoto wa Ecuador anayekipiga AC Milan, Pervis Estupiñán mwenye umri wa miaka 28, ni miongoni mwa wachezaji wanaotathminiwa na Aston Villa kwa ajili ya usajili. (Mail)
Newcastle United wanaamini kuwa kiungo wao wa Brazil, Bruno Guimarães, hauzwi, licha ya tetesi zinazoihusisha Arsenal na mpango wa kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 kwa ada ya pauni milioni 50. (Newcastle Chronicle)
Inter Milan wameachana na mpango wa kumsajili beki wa England Trevoh Chalobah baada ya kushindwa kumudu ada ya pauni milioni 30 inayotakiwa na Chelsea. Hata hivyo, Como bado wana nia ya kumsajili beki huyo mwenye umri wa miaka 27. (Corriere dello Sport - in Italian)
Chelsea wanajiandaa kuwasilisha ofa inayoweza kufikia pauni milioni 21 kwa ajili ya kumsajili beki wa kushoto wa Uhispania wa Rayo Vallecano, Pep Chavarría, mwenye umri wa miaka 28. (Marca - in Spanish)
Roma wamekataliwa ofa ya euro milioni 40 waliyopeleka kwa Atletico Madrid kwa ajili ya kumsajili Manu Koné, mwenye umri wa miaka 25. Manchester United na Liverpool pia wanamwania beki huyo wa Ufaransa. ((Corriere dello Sport - in Italian)
Aston Villa, Leeds United, Sunderland, Fulham na Brighton zote zinamfuatilia winga wa Sweden mwenye umri wa miaka 20 anayekipiga Barcelona, Roony Bardghji. (Sport via Sport Witness)
Hull City na Southampton zinaonyesha nia ya kumsajili mshambuliaji wa Werder Bremen kutoka Ujerumani, Justin Njinmah, mwenye umri wa miaka 25. (Bild - in German)
Kiwango bora alichoonyesha Thomas Schjelderup akiwa na Norway kwenye Kombe la Dunia kimeifanya Benfica kuongeza thamani yake hadi pauni milioni 43. Chelsea, Liverpool na Tottenham Hotspur zote zinamwania winga huyo mwenye umri wa miaka 22. (A Bola - in Portuguese)
Sporting, Wolves na Southampton zimegonga mwamba katika juhudi za kumsajili mshambuliaji wa Tottenham Hotspur, Will Lankshear baada ya klabu hiyo kukataa ofa zote zilizowasilishwa. Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 21 ameiwakilisha England katika timu za vijana na msimu uliopita alicheza kwa mkopo Oxford United. (Football.London)
Barcelona iko tayari kumuuza kiungo mshambuliaji wa Hispania, Ferran Torres, mwenye umri wa miaka 26, ili kuepuka kulipa takriban pauni milioni 7 kwa klabu yake ya zamani, Manchester City, endapo mkataba wake utaongezwa. (Athletic - subscription required)