Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.

Bofya kuelekea tovuti kuu

Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data

Moja kwa moja, Iran yatishia kushambulia nchi itakayoisaidia Marekani

Katibu wa Baraza Kuu la Usalama la Iran, Mohsen Rezaei, amesema "nchi yoyote itakayoisaidia Marekani kutekeleza vikwazo vya kiuchumi dhidi ya nchi yetu inachukuliwa kuwa adui."

Moja kwa moja

Na Ambia Hirsi

  1. Botswana yahaha kuhusu raia wake kujiunga na jeshi la Urusi

    Botswana inasema kuwa takribani raia wake wanane waliokuwa wakijaribu kujiunga na jeshi la Urusi wamezuiwa.

    Waziri wa Mambo ya Nje wa Botswana, Fenyo Butal, aliambia bunge mnamo Agosti 21 kuwa alizuia raia wanane wa nchi hiyo waliokuwa na mpango wa kujiunga na jeshi la Urusi ili kushiriki katika vita dhidi ya Ukraine.

    "Serikali ina wasiwasi mkubwa kuhusu visa vinavyoongezeka vyaa raia wa Botswana kusajiliwawa ili kushiriki katika mzozo kati ya Urusi na Ukraine," alisema Bw. Butal.

    Aliongeza kuwa serikali ina "ripoti za kutia wasiwasi" kuhusu "ahadi za ajira, mafunzo au kazi za usalama nchini Urusi" zinazotolewa katika ngazi ya jamii, kwa lengo la kuwahadaa raia na kuwapeleka kwenye mstari wa mbele wa vita vya nchi nyingine.

    "Kufikia sasa raia 22 wa Botswana wamedanganywa na mipango hii ya uajiri," alisema waziri wa mambo ya nje wa Botswana.

    Aliongeza: "Tulifanikiwa kuwazuia raia wetu wanane katika viwanja vya ndege vya Siretse Khama, O.R. Tambo, na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Addis Ababa, muda mfupi kabla ya safari yao kwenda Urusi na kuwarejesha nyumbani.

    " Ripoti za maelfu ya Waafrika kusajiliwa katika jeshi la Urusi kwa njia za udanganyifu na zisizo halali katika miaka ya hivi karibuni zimeibua mivutano ya kidiplomasia.

  2. Iran yatishia kushambulia nchi itakayoisaidia Marekani

    Katibu wa Baraza Kuu la Usalama la Iran, Mohsen Rezaei, amesema kwamba "nchi yoyote itakayoisaidia Marekani kutekeleza vikwazo vya kiuchumi dhidi ya nchi yetu inachukuliwa kuwa adui."

    Rezaei aliongeza katika taarifa kwa televisheni ya taifa: "Tunaziarifu nchi jirani na nchi zingine duniani: Msijiunge na vita vya kiuchumi vinavyoendeshwa na Marekani."

    "Maslahi ya nchi zinazosaidia Marekani kuendesha vita vya kiuchumi dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu italengwa," alisema Rezaei, na kuongeza: "Kwa nchi jirani zitashirikiana na Wamarekani katika vita hivyo vya kiuchumi, hakuna tone hata moja la mafuta litakalotoka..." Ghuba na Lango la Hormuz.

    Kauli ya Rezaei inakuja baada ya Washington kutangaza kuwa itaimarisha vikwazo vya kiuchumi ili kuishinikiza Tehran kurejea kwenye meza ya mazungumzo.

    Rezaei aliendelea kusema: "Bado hatujashambulia maslahi yoyote ya kiuchumi ya Marekani, mpaka sasa tumelenga kambi za kijeshi tu; lakini iwapo wanataka kutuwekea vikwazo vya kiuchumi, basi kampuni za mafuta na za kiuchumi za Marekani zilizo karibu na Iran na maeneo mengine, zijiandae kwa mapigo yetu ."

    Soma pia:

  3. Karibu kwa matangazo ya moja kwa moja.