Jeshi la Iran: Tuko tayari kwa vita vya muda mrefu

Chanzo cha picha, Getty Images
Jeshi la Iran limesema kuwa Jamhuri ya Kiislamu iko tayari kwa mapambano ya muda mrefu na kuendelea na operesheni zake.
Katika mahojiano na Shirika la Habari la Mehr, Naibu Afisa Mtendaji wa jeshi, Alireza Sheikh alisema kuwa Iran inaweza kuwa mhusika mwenye ufanisi kwa kutumia nyenzo zake za nguvu, kutoa majibu yanayofaa, na hata kuchukua hatua za kuzuia mashambulizi kabla hayajatokea.
Naibu mkuu wa wafanyakazi wa jeshi la Iran alitathmini mabadiliko ya maamuzi ya Donald Trump kuhusu kufanya mashambulizi zaidi ya kijeshi dhidi ya Iran, akizingatia uwezo wa Tehran. Alisema:
“Busara za Iran kwenye ubao wa chess umeilazimisha Ikulu ya White House kuendelea kufafanua upya malengo yake ya kisiasa.”
Bw. Sheikh pia alizungumzia mabadiliko ya mafunzo ya kijeshi ya Iran, kutoka msimamo wa kujilinda pekee hadi kwenye kuzuia mashambulizi na kuchukua hatua kwa ufanisi.
Alisema uwezo wa Iran wa kutengeneza makombora na ndege zisizo na rubani ni miongoni mwa mambo makuu yanayoiwezesha kuendelea na operesheni za kijeshi kwa muda mrefu.
Hapo awali, Mohammad Reza Naqdi, mshauri wa kamanda mkuu wa jeshi la Iran, alisema kuwa uamuzi wa kubadili kutoka mafunzo ya kujihami kwenda kwenye kushambulia ulikuwa tayari umefanywa, na kwamba mazingira sasa yako tayari kwa utekelezaji wake.
Unaweza kusoma;



































