Tazama baadhi ya matukio ya kukumbukwa ya Mfalme wa Soka duniani Pele

m

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya video, Tazama baadhi ya matukio ya kukumbukwa ya Mfalme wa Soka duniani Pele

Pele ni miongoni mwa wanasoka bora zaidi katika historia, amefariki akiwa na umri wa miaka 82 nchini Brazil.

Mshindi huyo mara tatu wa Kombe la Dunia alizungumza na vyombo vya habari mwezi Oktoba akiwa hospitalini kuwashukuru mashabiki wake na mungu kwa umri wake.

Pele alizaliwa mwaka wa 1940 katika familia maskini kusini-mashariki mwa Brazil, alifanikiwa kupata umaarufu wa soka licha ya kuvumilia umaskini.