Tetesi za soka Ulaya: Arsenal kusajili beki wawili, Martinelli kuondoka

Chanzo cha picha, Getty Images
Arsenal wanatafuta kuimarisha safu ya ulinzi msimu huu wa joto, huku wakilenga kumsajili beki wa Real Madrid, Victor Valdepenas (19), pamoja na beki wa kati wa Como na timu ya vijana ya Hispania chini ya miaka 21, Jacobo Ramon (21). (CaughtOffside)
Winga wa Brazil Gabriel Martinelli (24) anasisitiza kubaki Arsenal licha ya dalili kutoka klabuni kuwa anaweza kuuzwa msimu huu wa joto. (Football Insider)
Borussia Dortmund wanafikiria kufanya jaribio la tatu kumsajili winga wa England, Jadon Sancho (26), ambaye kwa sasa yuko kwa mkopo huko Aston Villa na anatarajiwa kuondoka Manchester United kama mchezaji huru msimu huu wa joto. (Telegraph)
Tottenham Hotspur wanataka kumsajili kipa wa Manchester City na timu ya taifa ya England, James Trafford (23), kama sehemu ya mipango yao ya dirisha kubwa la usajili. (Teamtalk)
Nottingham Forest wanatarajia kiungo wa England Elliot Anderson (23) kujiunga na Manchester United au Manchester City ikiwa ataondoka, lakini wanataka ada ya kati ya pauni milioni 100-120. (Florian Plettenberg)

Chanzo cha picha, Getty Images
Everton hawatarajiwi kutoa pauni milioni 50 kumnunua winga wa England Jack Grealish (30) kutoka Manchester City, lakini wana matumaini ya kufikia makubaliano mapya ili aendelee kubaki klabuni. (Athletic)
Manchester City wamejiunga na vilabu kadhaa vya Bundesliga na Ligi kuu England (EPL) katika kinyang'anyiro cha kumsajili kiungo wa miaka 16 wa Hertha Berlin, Kennet Eichhorn. (Fabrizio Romano)
Leeds United wako tayari kumruhusu mshambuliaji wa Hispania Mateo Joseph (22) kuondoka baada ya mkopo wake huko Mallorca. (Football Insider)
Chelsea hawana mpango wa kumuza beki kinda wa England Josh Acheampong (19) licha ya kupata nafasi chache za kucheza. (Express)
Kocha wa River Plate, Eduardo Coudet, amewasiliana moja kwa moja na Chelsea pamoja na winga wa Argentina Alejandro Garnacho (21) kuhusu uwezekano wa kumnunua kwa mkopo wa mwaka mmoja. (TyC / Football London)














