Tetesi za soka Ulaya: Enzo kutimka Chelsea

s

Chanzo cha picha, Getty Images

Muda wa kusoma: Dakika 2

Chelsea na kiungo wa Argentina, Enzo Fernandez, 25, anajiandaa kuwasilisha ombi la kuondoka na kuhamia Real Madrid msimu wa joto. (El Chiringuito, via Goal)

Tottenham wanamtaka kipa wa Manchester City na England, James Trafford, 23, kama mbadala wa Guglielmo Vicario, huku Inter Milan ikiwa na nia ya kumchukua Vicario, 29. (Sun)

Mlinzi wa England, Harry Maguire, 33, alikataa kuhamia Inter Miami kabla ya kusaini mkataba mpya na Manchester United, ambapo anataka kumalizia soka lake Old Trafford. (Sun)

Liverpool wameungana na Newcastle kumfuatilia Marco Palestra, 21, ambaye kwa sasa yuko kwa mkopo Cagliari akitokea Atalanta. (Teamtalk)

Manuel Ugarte,

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Manuel Ugarte

Manchester United watamuuza kiungo wa Uruguay, Manuel Ugarte, 24, msimu wa joto huu huku Galatasaray, Newcastle, na Tottenham wote wakionyesha nia ya kumsajili. (Fabrizio Romano)

United wanaonekana kushindwa kumfanya kiungo wa England, Elliot Anderson, 23, aungane nao, kwani anapendelea kuhamia Manchester City kutoka Nottingham Forest. (Mirror)

Kiungo wa Barcelona, Marc Casado, 22, yuko tayari kuondoka klabuni hapo baada ya kupoteza nafasi yake ya kuanza kwenye kikosi cha kwanza. (SER Catalunya)

Klabu ya Fenerbahce, wanataka kumchukua kiungo wa Tottenham, Yves Bissouma, 29, msimu wa joto huu. Mchezaji huyo wa Mali amecheza michezo minane tu msimu huu. (TurkishFootball)

Tottenham na Chelsea zote zinaangalia uwezekano wa kumsajili kiungo wa Sporting, Maxi Araujo, 26. (CaughtOffside)