Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Je, mvutano umeibuka kati ya Iran na Oman kuhusu Mlango-Bahari wa Hormuz?
Vyombo vya habari vya Uarabuni vimechunguza athari za ukanda wa muda ulioundwa katika maji ya Omani kwenye Mlango-Bahari wa Hormuz.
Baadhi vilisema ukanda huo haukuwa "mbadala" kwa njia ya jadi kupitia Mlango-Bahari wa Hormuz, wakati vingine vikiamini kuwa huenda ikaifanya Iran kupoteza "uwezo wa kimkakati."
Wakati huo huo, vyombo vya habari viliripoti tofauti za misimamo kati ya Oman na Iran kuhusu ukusanyaji wa ushuru wa meli zinazovuka Mlango wa Bahari wa Hormuz.
Matukio katika Mlango wa Bahari wa Hormuz yanandelea kungonga vichwa vya habari katika vyombo vya habari vya kikanda na vya ndani katika ulimwengu wa Kiarabu, na baadhi ya vyombo hivyo vilichunguza ufanisi wa ukanda wa muda wa Oman kwa meli zinazonuia kupita njia hii ya kimkakati ya majini.
Mnamo Juni 23 Oman ilitangaza kwamba imetoa ukanda wa baharini wa muda kwa meli zinazojaribu kuvuka Mlango-Bahari wa Hormuz, kwa ushirikiano na Shirika la Kimataifa la Bahari.
Kitengo cha ufuatiliaji wa matukio cha BBC kiliripoti kwamba vituo vingi vya televisheni vya Kiarabu vilizingatia taarifa ya pamoja ya Marekani na Baraza la Ushirikiano la Ghuba, iliyotolewa baada ya mkutano wa mawaziri huko Manama, ambao ulikataa mashtaka yoyote kutoka kwa meli zinazopita kwenye Mlango wa Hormuz.
Vyombo hivi vya habari viliangazia msisitizo wa taarifa hiyo kuhusu "lengo la pamoja la kuzuia Iran kumiliki silaha za nyuklia au kuitengeneza silaha hizo kwa namna yoyote."
Vyombo vingine vya habari pia viliangazoa taarifa tofauti za Muscat na Tehran kuhusu ukusanyaji wa ushuru wa kuvuka Mlango-Bahari wa Hormuz.
Je, Iran itapoteza "udhibiti"?
Al Jazeera Qatar ilichunguza ikiwa Iran itapoteza udhibiti wa Mlango-Bahari wa Hormuz kama "mbinuya kimkakati." Mtandao huo uliangazia tofauti za mitazamo kuhusu usimamizi wa Mlango-Bahari wa Hormuz, ukitoa mfano wa "kutoridhishwa" kwa Iran na Ukanda wa Oman.
Mtaalamu wa kijeshi Nidal Abu Zeid aliiambia Al Jazeera kwamba njia ya muda "huenda ikavutia meli zaidi," kwa sababu baadhi ya meli za kivita za mataifa ya Magharibi, zikisaidiwa na vikosi vya Marekani, hutoa huduma za usalama kwa meli zinazopitia kwenye njia hii, na njia hiyo haifiwi nai la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran.
Abu Zeid alisema hatua hiyo itakuwa na athari "dhidi ya Iran" na kwamba Iran "itapoteza ushawishi katika mazungumzo yake na Marekani," akiongeza kuwa hali hii "huenda ikaifanya Iran kujaribu kuvuruga njia ya Oman."
''Mbadala" sio njia ya jadi
Sky News Arabia, iliyo na makao yake mjini Abu Dhabi, iliripoti kwamba Ukanda wa bahari wa Oman sio mbadala wa njia ya jadi kupitia Mlango wa Bahari wa Hormuz, ambayo kabla ya vita iliruhusu meli 120 hadi 140 kupita kila siku. Mtandao huo uliongeza kuwa ukanda huo mpya unaweza kuruhusu meli chache kupita.
Wakati huo huo, mtandao huo uliripoti kuwa Umoja wa Mataifa umesitisha kwa muda operesheni yake ya kuowaondoa mabaharia waliokuwa wamekwama katika Mlango-Bahari wa Hormuz baada ya Marekani kuishutumu Tehran kwa kushambulia meli ya mizigo katika Bahari ya Oman.
Wakati huo huo, baadhi ya vyombo vya habari viliashiria tofauti ya misimamo kati ya Oman na Iran kuhusu ukusanyaji wa ushuru wa kuvuka Mlango-Bahari wa Hormuz.
Idhaa ya Al Arabi ya Qatar iliandika katika kichwa chake kikuu: "Mipango katika Mlango-Bahari wa Hormuz kati ya Iran na Oman... Kupokea ada za usafiri au kutopokea ada?"
Mtandao huo pia uliangazia onyo kutoka kwa Jeshi la Wanamaji la Walinzi wa Mapinduzi ya Iran kwamba meli katika Mlango-Bahari wa Hormuz zinatakiwa kutumia njia zilizoidhinishwa na Iran pekee.
Tovuti ya The Middle East Online pia iliandika: "Usimamizi wa Mlango-Bahari wa Hormuz umesababisha mpasuko kati ya Iran na Oman."
Tovuti hiyo imeongeza kuwa Iran bado inazingatia "mtazamo wake wa jadi wa Mlango-Bahari wa Hormuz kama zana ya kimkakati ambayo inaweza kutumika dhidi ya shinikizo au wakati wa migogoro ya kikanda," wakati Oman "inaweka kipaumbele cha kutoegemea upande wowote."