Kwanini China imenyamaza wakati mshirika wake Cuba anakabiliwa na shinikizo la Marekani?

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Iliyochapishwa
Muda wa kusoma: Dakika 6

"Ndugu mzuri, ndugu wapendwa, marafiki wazuri."

Haya ni maneno ambayo kiongozi wa China Xi Jinping ametumia mara kadhaa kuelezea uhusiano kati ya nchi yake na Cuba.

Na hii sio tu kauli mbiu ya kidiplomasia, bali ni kiashiria cha uhusiano wa karibu ambao umejengwa na mataifa haya mawili kwa miongo kadhaa.

Kisiwa hicho kinachukuliwa kuwa mojawapo ya madaraja makuu ya Beijing kuelekea Amerika ya Kusini, na uhusiano wa kiitikadi na kisiasa kati ya nchi hizo mbili ni wa kihistoria na wa muda mrefu.

Lakini licha ya uhusiano huu maalum, China imechukua hatua kwa tahadhari katika kukabiliana na moja ya migogoro mbaya zaidi katika nchi hiyo ya Caribbean.

Kwa nini taifa hili lenye uwezo mkubwa wa kiuchumi sio tu barani Asia ''linamtelekeza'' mshirika huyu wa kihistoria?

Usuhuba wa Beijing

XI na Trump

Chanzo cha picha, Getty Images

Ni jambo lisilopingika kwamba China imekuwa mshirika muhimu wa Cuba katika miongo ya hivi karibuni, lakini uungaji mkono wake unaonekana kufifia hasa kuhusiana na masuala ya kimkakati, kiuchumi na kijiografia.

Taifa hilo lenye uchumi mkubwa duniani limekuwa mshirika mkuu wa kibiashara wa Cuba kwa miaka mingi, na pia imeiruhusu nchi hiyo kwa zaidi ya mara moja kupanga upya madeni yake kutokana na matatizo ya kiuchumi katika kukidhi malipo yake.

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

"Kwa muda mrefu, uhusiano huo umeonekana kama msingi wa wazo la kusaidia Cuba kutoka kwa mtazamo wa kisiasa na kiitikadi. Na mtazamo huo unaendelea hadi wa leo," anasema Margaret Meyers, mkurugenzi wa Programu ya Asia na Amerika Kusini katika Mazungumzo ya Amerika ya Kati yenye makao yake makuu mjini Washington.

Huku mzozo wa sasa, ukichochewa na tishio la vikwazo kutoka kwa Marekani kwa usafirishaji wa mafuta kwenye kisiwa hicho tangu mwisho wa Januari, China imetuma misaada mbalimbali kwa Cuba.

Hizi ni pamoja na takribani tani 60,000 za mchele na mchango wa dola milioni 80 wa vifaa vya umeme na miundombinu ya nishati.

China pia imeisaidia Cuba kwa uwekezaji na michango ya moja kwa moja katika uimarishaji wa nishati mbadala, haswa kupitia uwekaji wa mbuga za Photovoltaic zinazoruhusu kisiwa hicho kuwa kidogo na kidogo kutegemea uhaba wa mafuta.

Kulingana na Kituo cha Mafunzo ya Nishati cha Ember, Cuba inajishughulisha na moja ya miradi mikubwa ya ufuaji wa nishati kwa kutumia nguvu za kwa msaada wa Beijing.

Thamani ya uagizaji wa paneli za sola na betri za photovoltaic kutoka China hadi Cuba iliongezeka kwa zaidi ya 1,800% kati ya 2020 na 2025, kulingana na takwimu zilizotolewa na Ember kwa CNN.

Xi Jinping alimpokea Rais Miguel Díaz-Canel mjini Beijing 2025, wakati wa ukumbusho wa miaka 80 ya kumalizika kwa Vita vya pili vya dunia. Katika hafla hiyo, walithibitisha tena uhusiano wa kirafiki kati ya mataifa hayo mawili.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Xi Jinping alimpokea Rais Miguel Díaz-Canel mjini Beijing 2025, wakati wa ukumbusho wa miaka 80 ya kumalizika kwa Vita vya pili vya dunia. Katika hafla hiyo, walithibitisha tena uhusiano wa kirafiki kati ya mataifa hayo mawili.

Usaidizi mdogo

Wataalamu walioshauriwa na BBC Mundo wanasema kwamba ingawa mshikamano wa Wachina umekuwa muhimu kwa Wacuba, uungwaji mkono wake bado ni mdogo.

Kulingana na Helen Yafe, mtaalamu wa kiuchumi wa kisiasa wa Amerika ya Kusini katika Chuo Kikuu cha Glasgow, "China imekuwa na sauti kubwa, ikisema wazi kupinga hatua zinazochukuliwa na Marekani na kutetea haki ya Cuba ya kuwa na mfumo wake wa kiuchumi na kisiasa. Lakini haya ni maneno tu. Kwa upande wa hatua madhubuti, uungwaji mkono umekuwa mdogo."

Imebainika pia kuwa China imechukua msimamo wa kujidhibiti zaidi kuliko washirika wengine wa Havana kama vile Urusi au Venezuela.

"Ikilinganishwa na washirika wengine au washirika wa nje, China ni wazi iko kuwa makini zaidi," Meyers anasisitiza.

Kisiwa hicho kimekabiliwa na mzozo wa nishati usio na kifani.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kisiwa hicho kimekabiliwa na mzozo wa nishati usio na kifani.

Biashara

Cuba haijasazwa katika mbinu ya kisayansi na ya kimkakati inayotumiwa na China kuendesha sera yake ya kiuchumi.

Kwa Beijing, manufaa ya uhusiano wa kibiashara na Cuba ni mdogo, na hili ni jambo linaloonekana wazi katika uagizaji kati ya mataifa hayo mawili.

Cuba iko mbali na kuwa mshirika mkubwa zaidi wa kibiashara wa China katika Amerika ya Kusini. Ushirikiano wake wa kiuchumi ni mkubwa zaidi wakati wa kuzingatia biashara na nchi kama vile Agentina, Brazili au Chile.

Uagizaji kutoka Cuba hadi China—wa bidhaa kama vile nickel, zinc, na nyinginezo—ulipungua kwa karibu dola milioni 600 kati ya 2017 na 2022, kulingana na takwimu za World Integrated Trade Solution (WITS). Lakini, Havana inadai kuwa biashara iliongezeka kati ya 2024 na 2025.

Emily Morris, mtafiti mwandamizi katika Chuo Kikuu cha London Institute of the Americas (UCLIA), anasema kwamba msaada wa China umekuwa muhimu, hasa katika sekta ya nishati.

Hata hivyo, pia anashikilia kuwa "China haitaki kutoa fedha kiholela kwa Cuba. Haitaki kubeba mzigo unaotokana na ushikiano wa zamani wa Umoja wa Soviet. Pia haitaki kuwa na mataifa yanayoitegemea. Uhusiano unaendeshwa kulingana na vigezo vya kibiashara."

"Kwa mtazamo huo wa kibiashara, China bila shaka haina mengi ya kupata nchini Cuba. Haijakuwa sehemu ya faida," Meyers anaongeza.

Kulingana na mtaalamu huyo, mtazamo wa Beijing unajibu, miongoni mwa mambo mengine, kwa maslahi ya kiuchumi ya China yenyewe na sera yake ya viwanda:

"China leo ina mtaji mdogo kuwekeza kote duniani na inahitaji kuielekeza fedha zake mwenye miradi muhimu zaidi na ya kimkakati."

"Na ikiwa kufanya kazi katika eneo kunaonekana kuwa na matatizo - kwa sababu za kiuchumi, kijiografia, au usalama - basi mtaji huo utaelekezwa kwenye maeneo mengine. Na hilo ndio jambo linalofanyika kwa sasa ."

Vikwazo na vikwazo vya Marekani vimezidisha mzozo wa kiuchumi na nishati unaoikabili Cuba.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Vikwazo na vikwazo vya Marekani vimezidisha mzozo wa kiuchumi na nishati unaoikabili Cuba.

Mchango wa Marekani katika mzozo unaoikabili Cuba si jambo dogo kwa China linapokuja suala la kuzingatia maslahi yake.

Mgogoro wa kiuchumi na nishati unaoathiri kisiwa hicho - uliochochewa na vikwazo vya mafuta vya Marekani na shinikizo la kisiasa la Marekani dhidi ya nchi hiyo - Beijing inafuatilia hali hiyo kwa wasiwasi mkubwa.

China imelaani vikwazo hivyo na vizuizi hivyo hivi karibuni ilifanya vivyo hivyo kuhusiana na uamuzi wa Donald Trump wa kumkabili kisheria Rais wa zamani wa Cuba Raúl Castro.

Wakati wasiwasi ukiongezeka huko Havana kuhusu uwezekano wa kuvamiwa na Marekani, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje Guo Jiakun alitangaza kwamba "Marekani inapaswa kuacha kutumia vikwazo na mfumo wa mahakama kama zana za ukandamizaji dhidi ya Cuba na kujiepusha na matamshi ya vitisho vya kutumia nguvu wakati wowote."

Lakini, kulingana na wataalam, China haina nia ya kuchukua jukumu ambalo linapita zaidi ya maneno ya kupendelea Cuba na ambayo inahusisha kuhatarisha uhusiano wake na nguvu ya Amerika Kaskazini.

Trump amezingatia upya, "Falsafa ya Monroe" Amerika Kusini na hii ni hatua muhimu.

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Ikulu ya White House imekuwa ikisema wazi kwamba lengo lake ni kuzingatia maslahi ya taifa kwanza "Marekani kwa Wamarekani" kwa madhumini ua kurudisha nyuma ushawishi wa kigeni kama vile China katika eneo hilo.

Kwa mujibu wa Shawn Yuan, mhariri wa BBC idhaa ya Kichina, ishara zilizotumwa na Marekani kwa kuvamia kijeshi Venezuela na kampeni yake ya kurejesha udhibiti kamili katika ulimwengu zimepatana na mtazamo wa Beijing.

"China inaelewa kikamilifu maana ya hilo kwa Marekani," anasema.

"Beijing haina nia ya kujitosa mzima mzima kwenye masuala ya Cuba. Bila shaka siokatika muktadha wa kauli kali zilizotolewa naTrump kuhusu kisiwa hicho," anaongeza.