Mitindo iliyovuma ufunguzi Olimpiki Rio 2016

Iliyochapishwa

Huu hapa ni kusanyiko wa picha za mitindo na tamaduni zilizovutia watu sana katika mitandao ya kijamii wakati wa sherehe za ufunguzi wa Michezo ya Olimpiki ya Rio, 2016.

Burundi
Maelezo ya picha, Mavazi ya kitamaduni … na viatu kutoka Burundi
Shelly-Ann Fraser-Pryce
Maelezo ya picha, Shelly-Ann Fraser-Pryce kutoka Jamaica aling'aa kwa mtindo wake wa nywele
India
Maelezo ya picha, Wanamichezo kutoka India nao walivutia kwa koti zao na sari
Ureno
Maelezo ya picha, Ureno mtindo wao ulikuwa wa jeans
Indonesia
Maelezo ya picha, Indonesia waliamua kuvalia kifalme
Bermunda
Maelezo ya picha, Bermunda nao wakavumisha kaptula za Kibermunda
Tonga
Maelezo ya picha, Mbeba bendera huyu wa Tonga alisisimua wengi kwa kifua chake wazi kilichong'aa kutokana na mafuta
Norway
Maelezo ya picha, Norway walitikisa ukumbi kwa vazi hili
Msumbiji
Maelezo ya picha, Kwa Msumbiji, mashati yenye michoro ya vijisanduku ndiyo yalikuwa mavazi ya sherehe
Brazil
Maelezo ya picha, Kina dada wa Brazil walijitokeza na vazi lenye muundo wa majani, wakiwakilisha rangi ya bendera la taifa lao. Brazil ndio wenyeji.