Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tundu Lissu: Kesi yaahirishwa baada ya mshitakiwa kusema hajala
Mashahidi wa upande wa mashtaka wameanza kutoa ushahidi dhidi ya Tundu Lissu, kiongozi wa chama kikuu cha upinzani Tanzania CHADEMA ambaye anakabiliwa na kesi ya uhaini katika Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam.
Muhtasari
- Urusi yaamuru kuzuiwa kwa WhatsApp katika msako wa programu za kutuma ujumbe
- Tundu Lissu: Sijala lakini naomba tuendelee
- Tundu Lissu: Kesi yaahirishwa baada ya mshitakiwa kusema hajala
- Afueni kwa Sifuna baada ya mahakama kusitisha ufurushwaji wake
- Kim Jong Un amchagua binti yake kijana kuwa mrithi
- Tundu Lissu: Nukisha inatokana na neno nuka inaweza kuwa harufu nzuri au harufu mbaya
- 'Niliona video ya Lissu akisema atakinukisha na uchaguzi mkuu hautafanyika' - Shahidi
- Mashahidi 5 kati ya 30 kutoa ushahidi katika kesi ya Tundu Lissu leo
- IShowSpeed aiorodhesha Kenya kama kivutio chake bora zaidi katika ziara ya Afrika
- Bangladesh yapiga kura katika uchaguzi wa kwanza baada ya msukosuko wa kisiasa
- Kimbunga kikali chaua takriban watu 31 Madagascar
- Waziri Mkuu wa Uingereza amtaka mmiliki wa Man United kuomba radhi kwa kusema Uingereza 'imetawaliwa na wahamiaji'
- Iran yakutana na viongozi wa Hamas na Houthi wakati wa ziara ya Netanyahu nchini Marekani
- Polisi wamtambua kijana wa miaka 18 kama mshukiwa wa shambulio la Tumbler Ridge
- Trump baada ya kukutana na Netanyahu: Ninasisitiza kuendelea na mazungumzo na Iran
- Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani: Makombora ya Iran yanatishia si Israel pekee bali hata Ulaya
Moja kwa moja
Na Abdalla Seif Dzungu, Ambia Hirsi & Asha Juma
Urusi yaamuru kuzuiwa kwa WhatsApp katika msako wa programu za kutuma ujumbe
Urusi imeagiza kuzuiwa kwa WhatsApp, huku ikiendelea kuweka masharti makali kwenye programu hiyo ya kutuma ujumbe.
WhatsApp inayomilikiwa na Meta ilisema hatua hiyo ililenga kuwasukuma zaidi ya watumiaji milioni 100 wa programu zake nchini Urusi kwenye "programu ya ufuatiliaji inayomilikiwa na serikali".
WhatsApp inayomilikiwa na Meta ilisema hatua hiyo inalenga kuwashinikiza zaidi ya watumiaji milioni 100 wa programu hiyo nchini Urusi watumie "programu inayomilikiwa na serikali" yenye kuwachunguza.
Msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov aliambia BBC kwamba uamuzi huo umefanywa "kutotakana na [Meta] kutofuata kanuni na sheria ya Urusi". Amesema Meta inaweza kuanza tena shughuli zake ikiwa "itafuata sheria na kuingia katika majadiliano".
Alipoulizwa kama mamlaka ilikuwa inajaribu kuwalazimisha Warusi kutumia programu ya Max iliyotengenezwa na serikali, Peskov alisema "programu ya kitaifa [ni] mbadala" kwa Warusi.
Pia unaweza kusoma:
Tundu Lissu: Sijala lakini naomba tuendelee
Kiongozi wa chama kikuu cha upinzani Tanzania CHADEMA ambaye anakabiliwa na kesi ya uhaini anasema hajala licha ya kesi dhidi yake hapo awali kuahirisha aliposema hajala chakula.
Wafuasi wake waliokuwa mahakamani waliangua kilio baada ya kusikia kauli hiyo.
Hata hivyo Tundu Lissu alisema hajala baada ya kesi kuendelea, na ikamlazimu Jaji kuahirisha kesi hiyo hadi kesho saa tatu asubuhi, ambapo shahidi No 2 anatarajiwa kuendelea kutoa ushahidi wake.
Jaji: Afya ni haki ya msingi ya kila mmoja kwa kuzingatia hayo mahakama inawajibu kuhakikisha (fair trial).
Jaji: Mahakama inaona sio sawa kuendelea na shauri wakati mshitakiwa hajapata chochote sababu mnasema chakula kinapaswa kutoka gerezani.
Jaji: Tutaendelea na shauri kesho saa tatu asubuhi.
Jaji: Mahakama inaelekeza mshitakiwa aletewe chakula kwa wakati sababu tulieleza shauri hili litakuwa linasikilizwa mpaka saa kumi na moja jioni.
Ni takriban miezi kumi imepita tangu mwanasiasa huyo wa chama cha upinzani Tanzania, kuanza kusota rumande.
Soma zaidi:
Tundu Lissu: Kesi yaahirishwa baada ya mshitakiwa kusema hajala
Mashahidi wa upande wa mashtaka wanaendelea kutoa ushahidi dhidi ya Tundu Lissu, kiongozi wa chama kikuu cha upinzani Tanzania CHADEMA ambaye anakabiliwa na kesi ya uhaini.
Waliki wa serikali Renatus Mkude ameanza kungumza na kusema wao wako tayari na wana shahidi wa siri P6 wakiwa tayari kuendelea.
Kwa mujibu wa sheria ya magereza wafungwa mahabusu wanajinunulia chakula.
Mshitakiwa anasema yuko tayari kuendelea lakini anasema nyie wote mmekula ila mimi sijala.
"Wana pesa zangu na inapofika muda wa kula wananinulia chakula lakini mpaka, sasa sijala sio kwamba pesa hakuna ila ni mambo ya kutesa tesa watu," mshtakiwa Tundu Lissu alisema.
Jaji anasema kuwa wakili wa serikali kwa kuwa hajala basi tunaomba ahirisho mshtakiwa akale ili kuwa na usikilizaji wa haki asije akashindwa kumuuliza shahidi maswali.
Tundu Lissu hata hivyo anasema mimi ninaweza kuendelea na napenda liingie kwenye rekodi muone utaratibu ulivyo tu.
Lakini Jaji anasisitiza kuwa ikiwa ni kweli hujala tangu asubuhi ‘’tusingetamani tuendelee na shauri wakati hujala inakuwa ni kinyume cha haki za binadamu.’’
Wakili wa serikali akasisitiza kuwa Sisi tutaahirisha hata kwa nusu saa ili upate chakula.
Tundu Lissu anaendelea kusema, mheshimiwa unapokuwa mfungwa unakuwa kwenye mikono ya watu na wenye wajibu huo ni magereza na wakati tunatoka hapa niliwaambia wanitafutie hata chips kavu.
Lakini ieleweke siko tayari kwa aahirisho sababu sijala.
Hata hivyo Jaji alisisitiza kuwa kesi itaitaahirishwa kwa dakika 15 upatiwe chakula.
Afueni kwa Sifuna baada ya mahakama kusitisha ufurushwaji wake
Mahakama imesimamisha tangazo la kuondolewa madarakani kwa Edwin Sifuna kama Katibu Mkuu wa chama cha ODM.
Mahakama ya Mizozo ya Vyama vya Siasa imetoa uamuzi huo ambao umechukuliwa na baadhi ya wachanganuzi kama ushindi kwake kwa sasa.
Mahakama ilizuia utekelezaji wa tangazo hilo lililopitishwa na Baraza la chama cha ODM (NEC) mnamo Februari 11, 2026.
Mahakama hiyo pia imezuia kuchapisha azimio hilo katika gazeti la Kenya Gazette, hatua muhimu ambayo ingekuwa imehalalisha na kusababisha kuondolewa kwake.
Maagizo yatasalia kutumika kusubiri kusikilizwa na kuamuliwa kwa ombi kwa misingi ya pande zote.
Uamuzi huo unaashiria ahueni kubwa kwa Sifuna, ikiwa ni siku moja tu baada ya NEC kutangaza azimio lake la kumwondoa katika nafasi hiyo yenye nguvu katika chama.
Pia unaweza kusoma:
Habari za hivi punde, Tundu Lissu: Shahidi wa pili anatarajiwa kutoa ushahidi wake
Kesi dhidi ya kiongozi wa upinzani nchini Tanzania Tundu Lissu imeaanza tena.
Shahidi wa pili anatarajiwa kutoa ushahidi wake- anaitwa P6, atakua shahidi wa pili kwa leo, na shahidi wa tano upande wa jamhuri tangu ushahidi uanze kutolewa.
majaji wameshaingia, na mshitakiwa pia ameingia mahakamani.
Kim Jong Un amchagua binti yake kijana kuwa mrithi
Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un amemchagua binti yake kuwa mrithi wake, shirika la ujasusi la Korea Kusini liliwaambia wabunge siku ya Alhamisi.
Ni machache sana yanayojulikana kuhusu Kim Ju Ae, ambaye katika miezi ya hivi karibuni amekuwa akipigwa picha pamoja na baba yake katika matukio maarufu kama vile ziara ya Beijing mnamo mwezi Septemba - safari yake ya kwanza inayojulikana nje ya nchi.
Huduma ya Kitaifa ya Ujasusi (NIS) ilisema ilizingatia "mambo mbalimbali" ikiwa ni pamoja na uwepo wake unaozidi kuwa maarufu hadharani katika matukio rasmi" katika kufanya tathmini hii.
NIS pia ilisema itafuatilia kwa karibu kama atahudhuria mkutano mkuu wa chama cha Kaskazini baadaye mwezi huu - tukio kubwa zaidi la kisiasa ambalo hufanyika mara moja kila baada ya miaka mitano.
Chama tawala ndio chenye kutarajiwa kutoa maelezo zaidi kuhusu vipaumbele kama vile sera za kigeni, mipango ya vita na matarajio ya nyuklia kwa miaka mitano ijayo.
Siku ya Alhamisi mbunge Lee Seong-kwen aliwaambia waandishi wa habari kwamba Ju Ae, ambaye hapo awali alielezewa na NIS kama "anayefunzwa" kuwa mrithi, sasa alikuwa katika hatua ya "uteuzi wa mrithi".
Soma zaidi:
Shahidi P5 amemaliza kutoa ushahidi
Tundu Lissu amemalza kumuuliza maswali Upande wa jamuhuri nao hawana la ziada.
Shahidi anayefuata hajafika upande wa serikali umeomba ahirisho mpaka saa nane.
Upande wa jamhuri uliomba kuahirishwa kwa kesi hadi kesho, lakini jaji wa kesi hiyo, Jaji Dastan Nduguru anasema maelezo yake ya awali yalikua ya wazi kuwa anataka leo wasilikile mashahidi watatu.
Hivyo kesi hiyo imeahirishwa hadi saa nane mchana leo.
Tundu Lissu: Nukisha inatokana na neno nuka inaweza kuwa harufu nzuri au harufu mbaya
Lissu anaendelea kumuuliza maswali kwa shahidi wa kwanza, P5.
Ulisema uliona nimevaa gwanda na tisheti nyeusi waeleze majaji kama yako kwenye maelezo yako ya polisi na kuwa nyuma kulikuwa na bendera ya taifa yapo hayapo ….. hayapo?
Tundu Lissu anaendelea: Ulisema ulipotoka posta ulipanda gari na kwenda kijiwe cha kahawa ‘'maskani’'ubungo waeleze majaji kama yapo kwenye maelezo yako ya polisi …. kwa hapa siyaoni Ulisema ulipofika maskani ulikuta mzozo… kweli si kweli …. kweli waeleze majaji kama kuna hayo maeelezo kwenye maelezo yako ya polisi ulikuta mzozo tuambie …. hapa haupo Ulisema uliporudi nyumbani ulimpigia ndugu yako askari ambaye anafanya kazi tabata relini waleze majaji kama hayo maelezo yapo kwenye maelezo yako uliyotoa Polisi … kimya … tunasubiri… hapa hayapo…. huyo ndugu yako askari ana jina?
Shahidi anajibu: Ndio ana jina
Tundu Lissu: Waeleze majaji kama polisi ulimtaja Jina … Shahidi: kimya…. Polisi sikumtaja jina …. ana ka cheo fulani ….. sijui … unajua kama ana force namba
Shahidi: Sijui
Tundu Lissu: hujui sitaki kukuliza vitu usivyojua Tundu lissu anaendelea.. Unasema ulipotazama video ya kukinukisha ulipata hofu kwenye maelezo yako ya polisi hayo maneno yapo kwamba nilipata hofu….. hapa hayapo…. hapa hayapo au sio Waleze majaji kuwa kilichotokea tahere 29 octoba uliwahi kuandika melezo ya ziada Polisi au umekuja kuyatolea hapa kwamba ile hofu uliyokuwa nayo ndicho kilitokea oktoba haya maelezo hayapo kwenye maelezo yako ya Polisi kweli si kweli hayapo ? Sasa polisi walikuuliza wewe unasema wao hawaandiki?
Tundu Lissu anaendelea na kumshukuru shahidi: Ahsante shahidi Walau nimemaliza kuthibitusha kuwa wewe sio mtu wa kuaminika.
Tundu Lissu anaendelea .. Hii video uliyokuwa unaangalia Facebook ilikuwa kwenye akaunti ya nani? huo wakati ulipokua unaperuzi….
Shahidi: Sikufahamu kupitia account gani Tundu Lissu: majaji hawajaona hiyo video , unaweza kuwaonesha Shahidi: hapana sijawaonesha simu yangu ilipotea.
Tundu Lissu: Je umeiwasilisha hiyo video mahakamani ?
Shahidi: Sijaiwasilisha. Lissu anaendelea kuuliza, Umesema ulipompigia yule askari ndugu yako simu na kumuuliza kama amesikia hayo ya mtandaoni ya Bwana tundu Lissu Je ulienda kutoa taarifa polisi na kupata RB
Shahidi: hapana sikwenda Tundu Lissu: Je huyo ndugu yako polisi ulimueleza alikuambia kwenda polisi kufungua RB?
Shahidi: Hapana hakuniambia kwenda kufungua RB
Tundu Lissu: Shahidi umesema ulisikia nimesema nitakinukisha Maana ya kukinukisha ni nini?
Shahidi: Ni uashiria wa kuchochea vurugu au fujo.
Tundu Lissu: Hayo umeyatoa wapi?
Tundu Lissu: Nina kamusi ya kiswahili hapa unataka nikusomee maana ya nukisha.
Shahid: Ndio nisomeee.
Tundu Lissu: Majaji naomba nimsomee Nukisha – inatokana na neno nuka inaweza kuwa harufu nzuri au harufu mbaya.
Tundu Lissu: Haya yako ya kufanya fujo umeyatoa wapi kaka?
Shahidi: Mimi nimesikia mitandaoni ….Na kupitia watu pia.
Tundu Lissu: Nataka uangalie kilelezo chako hiyo kesi ya polisi nataka uwaeleze majaji kwamba kwenye maelezo yako Polisi maana ya neno kukinukisha ni kufanya fujo? yapo….. Kimyaaaaaa…. Yapooo… kwamba umewaeleza Polisi kwamba aliposema atakinukisha alikuwa anasema anaenda kufanya fujo…. yapo nikiyatolea maelezo … kwenye maelezo yako uliyoshika mkononi yapo.
Shahidi: hapa hayapo
Tundu Lissu: Waheshimiwa majaji mimi sina swali zaidi kwa shahidi.
Habari za hivi punde, 'Niliona video ya Lissu akisema atakinukisha na uchaguzi mkuu hautafanyika' - Shahidi
Shahidi aliyepewa jina shahidi P5 ameanza kutoa ushahidi wake ambapo amenukuliwa akisema: “Niliona video ya lissu mtandao wa Facebook akisema atakinukisha uchaguzi mkuu hautafanyika .
Akizungumza mahakamani, shahidi huyo alisema kwamba maafisa wa polisi pia 'walitumika kuiba kura huku akiongezea kwamba majaji waliopo katika mahakama hiyo ni washirika wa CCM na kwamba hawatendi haki.
Vilevile aliongezea kwamba 'aliihofia video hiyo ingesababisha uvunjifu wa amani, kukwamisha biashara na kusababishia njaa'.
'Niliwasiliana na ndugu yangu ambaye ni Polisi na kumuuliza akaniambia niwe na amani huku akinihakikishia kwamba watalifanyia kazi suala hilo kikamilifu'.
''Nilihofia kutokana na lile neno 'kukinukisha nikaona kutakuwa na uvunjifu wa amani’’
Baadaye anasema kwamba aliitwa katika kituo cha polisi ili kurekodi taarifa hiyo
’Niliitwa kituo cha polisi cha kati tarehe 9/4/ 2025 kutoa ushahidi’’
Endelea kufuatilia habari hii hapa
Habari za hivi punde, Mashahidi 5 kati ya 30 kutoa ushahidi katika kesi ya Tundu Lissu leo
Mashahidi wa upande wa mashtaka wameanza kutoa ushahidi dhidi ya Tundu Lissu, kiongozi wa chama kikuu cha upinzani Tanzania CHADEMA ambaye anakumbwa na kesi ya uhaini katika mahakama kuu jijini Dar esSalaam.
Awali mahakama hiyo iliridhia kizimba maalumu cha kulinda utambulisho wa mashahidi wa siri kimekidhi vigezo vya kisheria.
Katika kesi hii Tundu Lissu anajitetea mwenyewe .
Hapo Jana kesi hiyo ilihairishwa kufuatia uamuzi mdogo uliotolewa kuhusu kizimba cha mashahidi wa siri ambacho Mahakama iliagiza kirekebishwe.
Kizimba hicho kimerekebishwa kuwapa majaji nafasi ya kumuona shahidi kama sheria inavyosema.
Lissu alikamatwa April mwaka jana mkoani Iringa kwenye shughuli za chama akituhumiwa kwa kesi ya mbili za uhaini na kesi nyingine ya uchochezi.
IShowSpeed aiorodhesha Kenya kama kivutio chake bora zaidi katika ziara ya Afrika
Mtiririshaji maudhui maarufu duniani kutoka Marekani IShowSpeed ametaja ziara yake nchini Kenya kuwa ya kukumbukwa na yenye matokeo bora kati ya matukio yote aliyopata wakati wa ziara yake ya siku 28 ya IRL (In Real Life) barani Afrika.
IShowspeed ambaye jina lake halisi ni Darren Jason Watkins Jr, ambaye hivi majuzi alihitimisha ziara yake ya kwanza ya bara la Afrika akizuru nchi nyingi za Kiafrika na kujitumbukiza katika mchanganyiko wa tamaduni na uzoefu wa kipekee, mwanzoni alitatizika kutaja jambo moja ambalo lilimgusa sana barani Afrika - kabla ya kuitaja Kenya.
Akiongea na watangazaji wa Yahoo Sports Daily Caroline Fenton na Jason Fitz, Speed aliombwa kutaja kumbukumbu yake anayoipenda zaidi kutokana na ziara yake ya utiririshaji ya Afrika yenye mafanikio makubwa.
"Namaanisha, ukiangalia picha hizi zote, inaonekana tu ulikuwa na uzoefu mzuri sana. Umeingiana na watu, na utamaduni.
Ikiwa unaweza kutaja moja, ni eneo gani ambalo linakupatia kumbukumbu uliyoipenda zaidi au hadithi kutoka kwa safari yako ya Afrika?" Caroline Fenton aliuliza.
Speed alikiri kwamba kuulizwa kutaja uzoefu wa 'moja' ilikuwa ngumu kidogo kwani swali lilikuwa 'pana zaidi', akikiri kuwa mengi yalitokea kwenye ziara yake.
"Kumbumbuku yangu moja, hilo ni swali pana sana kwa sababu kuna mengi yametokea, unaniweka, lakini, ziara yangu ya Kenya ilikuwa hivyo, ilikuwa inashangaza jinsi watu walivyotoka kwa ajili yangu," alisema.
"Nadhani ilikuwa labda watu 30,000 waliotoka jijini ili kunitazama tu nikitiririsha na kuwa nami."
Maelezo zaidi:
Bangladesh yapiga kura katika uchaguzi wa kwanza baada ya msukosuko wa kisiasa
Zaidi ya watu milioni 120 kote Bangladesh wanatazamiwa kupiga kura zao leo kwa serikali mpya.
Huu ni uchaguzi wa kwanza tangu vuguvugu linaloongozwa na vijana kumuondoa madarakani kwa kiasi kikubwa aliyekuwa Waziri Mkuu Sheikh Hasina.
Maandamano hayo mnamo 2024 yalimaliza miaka 15 ya utawala wa kimabavu chini ya Hasina.
Wengi wanatumai kuwa uchaguzi wa leo utaleta enzi mpya ya utawala wa uwakilishi kwa Bangladesh. Endelea kuwa nasi tunapokuletea masasisho na uchambuzi wa hivi punde.
Kimbunga kikali chaua takriban watu 31 Madagascar
Takriban watu 31 wamefariki baada ya kimbunga kikali kuikumba Madagascar, imesema mamlaka ya maafa katika kisiwa cha Bahari ya Hindi.
Kimbunga Gezani kilianguka Jumanne, na kugonga bandari kuu ya kisiwa hicho, Toamasina.
Ofisi ya usimamizi wa majanga ya Madagaska ilisema kulikuwa na "machafuko " - ikiripoti kuwa nyumba zilianguka katika eneo la athari, ambapo miili ilipatikana.
Vitongoji vilitumbukizwa gizani huku nyaya za umeme zikikatika, huku miti na paa ziking'olewa
"Kilichotokea ni maafa, karibu asilimia 75 ya mji wa Toamasina uliharibiwa," kiongozi wa kijeshi wa nchi hiyo Kanali Michael Randrianirina, ambaye alichukua mamlaka mwezi Oktoba, aliambia shirika la habari la AFP.
"Hali ya sasa inazidi uwezo wa Madagaska pekee," aliongeza. Maporomoko ya kimbunga hicho huenda yakawa mojawapo ya matukio makali zaidi yaliyorekodiwa kuzunguka jiji hilo katika enzi ya satelaiti, kulingana na mtabiri wa kimbunga cha CMRS kwenye kisiwa cha Reunion cha Ufaransa, AFP inaripoti.
Ofisi ya Kitaifa ya Kudhibiti Hatari na Majanga ilisema wengi waliuawa wakati nyumba zilipoporomoka.
Kimbunga Gezani kilipiga Toamasina - jiji la pili kwa ukubwa nchini - na upepo unaofikia kilomita 250 kwa saa (155 mph). "Ni machafuko makubwa, asilimia 90 ya paa za nyumba zimeng’olewa, kabisa au kwa sehemu," mkuu wa usimamizi wa majanga katika shirika la misaada la Action Against Hunger, Rija Randrianarisoa, aliiambia AFP.
Ofisi ya usimamizi wa maafa ya Madagaska imewahamisha makumi ya watu waliojeruhiwa na mamia ya wakaazi kutoka wilaya karibu na Toamasina, makazi ya watu 400,000.
Waziri Mkuu wa Uingereza amtaka mmiliki wa Man United kuomba radhi kwa kusema Uingereza 'imetawaliwa na wahamiaji'
Sir Keir Starmer ametaja maoni kuhusu uhamiaji yaliyotolewa na mmiliki mwenza na bilionea wa Manchester United Sir Jim Ratcliffe kuwa "ya kukera na yasiyo sahihi".
Sir Jim, mwanzilishi wa kampuni kubwa ya kemikali duniani, Ineos, aliiambia Sky News Jumatano kwamba Uingereza ilikuwa "imetawaliwa na wahamiaji" na kusema waziri mkuu "ni mzuri sana" kufanya "mambo magumu" kuleta utulivu wa uchumi wa nchi.
Katika karipio lake Jumatano jioni, Sir Keir aliongeza kuwa Uingereza ni "nchi yenye fahari, vumilivu na yenye watu mbalimbali" na kumtaka Sir Jim kuomba radhi.
Msemaji wa afisi ya waziri mkuu pia alimtaka mfanyabiashara huyo kuomba radhi, akisema maoni "yanapendelewa na wale wanaotaka kugawanya nchi yetu".
BBC imewasiliana na Ineos na Manchester United ili kutoa maoni yao kuhusiana na matamshi ya Sir Jim. Sir Jim aliliambia shirika la utangazaji:
"Huwezi kuwa na uchumi wenye watu milioni tisa wanaonufaika na viwango vikubwa vya wahamiaji wanaoingia." Aliongeza: "Namaanisha, Uingereza imetawaliwa.
Inagharimu pesa nyingi sana. "Uingereza imetawaliwa na wahamiaji, sivyo? Ninamaanisha, idadi ya watu nchini Uingereza ilikuwa milioni 58 mnamo 2020, sasa ni milioni 70.
Hiyo ni watu milioni 12." Hathivyo, data kutoka Ofisi ya Takwimu ya Kitaifa inakadiria kuwa idadi ya watu wa Uingereza katikati ya 2025 ilikuwa milioni 69.4, ikilinganishwa na milioni 66.7 katikati ya 2020.
Sir Jim alitoa maoni hayo wakati wa mahojiano na mhariri wa uchumi wa Sky News Ed Conway, pembezoni mwa Mkutano wa Kiwanda wa Ulaya huko Antwerp, Ubelgiji.
Matamshi hayo pia yalilaaniwa na makundi mbalimbali ya mashabiki, ikiwa ni pamoja na Manchester United Supporters Trust ambayo ilisema kwenye X: "Hakuna shabiki anayepaswa kuhisi kutengwa kuifuata au kuiunga mkono klabu kwa sababu ya rangi, dini, utaifa au asili yake.
Iran yakutana na viongozi wa Hamas na Houthi wakati wa ziara ya Netanyahu nchini Marekani
Ali Larijani, Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran amekutana na kundi la viongozi wa Hamas katika ziara yake nchini Qatar akiwemo Khaled Meshaal, Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Hamas.
Bw. Larijani pia alikutana na msemaji wa Houthi nchini Qatar. Kikao cha Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran na viongozi wa makundi yanayoungwa mkono na Jamhuri ya Kiislamu katika eneo kilikwenda sambamba na ziara ya Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu mjini Washington na kukutana na Rais Donald Trump wa Marekani.
Bwana Netanyahu anatarajiwa kumtaka rais wa Marekani kutafuta mapatano na Iran ambayo sio tu kwamba yatasimamisha urutubishaji wa madini ya uranium nchini humo bali pia kupunguza mpango wake wa makombora ya balistiki na uungaji mkono wake kwa makundi yanayoungwa mkono na Tehran katika eneo kama vile Hamas na Hezbollah.
Hii ni licha ya Iran kusisitiza kila mara kuwa mazungumzo yake na Marekani yatahusu tu mpango wake wa nyuklia.
Polisi wamtambua kijana wa miaka 18 kama mshukiwa wa shambulio la Tumbler Ridge
Kijana wa miaka 18 ametajwa kuwa mshukiwa wa shambulio la risasi lililoua watu wanane na kujeruhi makumi ya wengine huko British Columbia, Canada.
Polisi walisema Jesse Van Rootselaar alipatikana amefariki katika eneo la tukio kutokana na kujipiga risasi.
Sababu ya shambulio hilo bado haijajulikana. Watu sita waliuawa na wengine 25 kujeruhiwa katika Shule ya Sekondari ya Tumbler Ridge.
Wengine wawili - mama wa mshukiwa, 39, na kaka wa kambo, 11 - walipatikana wamekufa katika nyumba iliyo karibu.
Mamlaka zilisema Van Rootselaar alizaliwa akiwa mwanamume wa kibaolojia lakini akatambuliwa kama mwanamke.
"Ninaweza kusema kwamba Jesse alizaliwa kama mwanamume wa kibaolojia ambaye takriban miaka sita iliyopita alianza kubadilika kuwa mwanamke," Dwayne McDonald, naibu kamishna wa Polisi wa Kifalme wa Canada (RCMP), alisema.
Tukio la ufyatuaji risasi lilitokea katika nyumba iliyo karibu, kisha mshukiwa akaenda shule, McDonald alisema.
Waliouawa katika shule hiyo ni mwalimu wa kike mwenye umri wa miaka 39, wanafunzi watatu wa kike, wote wakiwa na umri wa miaka 12, na wanafunzi wawili wa kiume, mmoja wa miaka 12 na mwingine 13.
Trump baada ya kukutana na Netanyahu: Ninasisitiza kuendelea na mazungumzo na Iran
Baada ya kukutana na Benjamin Netanyahu, Donald Trump aliandika kwenye jukwaa la mtandao wa kijamii la Truth:
"Hakuna matokeo ya uhakika yaliyopatikana, isipokuwa nilisisitiza kuwa mazungumzo na Iran yanaendelea kuona ikiwa makubaliano yanaweza kufikiwa." Bw. Trump pia aliandika: "Nilimfahamisha Waziri Mkuu [Netanyahu] kwamba mapendeleo yetu ni makubaliano.
Tutaona matokeo yatakuwaje. Mara ya mwisho Iran iliamua kutoshughulika na ikashambuliwa kupitia [Operesheni] Midnight Hammer. Natumai watachukua hatua kwa busara na kuwajibika zaidi wakati huu." Bw.Trump pia aliandika kwamba amezungumza pia masuala ya Gaza na Waziri Mkuu wa Israel.
"Tulijadili maendeleo makubwa ambayo yamepatikana huko Gaza na kanda kwa ujumla," aliandika. Baada ya kikao hicho, ofisi ya Benjamin Netanyahu pia ilitangaza kuwa Waziri Mkuu wa Israel alisisitiza katika kikao hicho kwamba katika mazungumzo ya Marekani na Iran, kipaumbele chake ni kuhakikisha usalama wa Israel.
Kwa mujibu wa AFP, Bw. Netanyahu alikubaliana na Rais wa Marekani "kuratibu na kuwasiliana" ili kuendeleza mazungumzo ya Iran na Marekani.
Bw. Netanyahu alikutana na Steve Whittaker, mjumbe maalum wa Donald Trump, na Jared Kushner, mkwe wa Bw. Trump, jana usiku baada ya kuwasili Washington.
Kwa mujibu wa Ofisi ya Waziri Mkuu wa Israel, wawili hao "walishiriki ripoti na Netanyahu kuhusu duru ya kwanza ya mazungumzo na Iran Ijumaa iliyopita."
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani: Makombora ya Iran yanatishia si Israel pekee bali hata Ulaya
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani amesema nchi yake imejitolea kupata suluhu la kidiplomasia kati ya Marekani na Iran kuhusu mipango ya nyuklia na makombora ya Tehran.
Akizungumza pambizoni mwa mkutano na mawaziri wa mambo ya nje wa nchi za Asia ya Kati mjini Berlin, Johann Wadful amesema:
"Mbali na mpango wa nyuklia, mradi wa kutengeneza makombora ya balistiki ya Iran ni hatari kwa Israel na Ulaya."
Alisisitiza kuwa "ni kwa manufaa yetu kwamba masuala haya yachunguzwe na kutatuliwa kwa mazungumzo."
Katika wiki za hivi karibuni, Ujerumani imechukua msimamo mkali zaidi kati ya nchi za Ulaya dhidi ya mauaji ya waandamanaji nchini Iran.
Soma zaidi:
Natumai hujambo na karibu katika habari zetu za moja kwa moja