Moja kwa moja, Mafuriko Nepal na Tibet yaua zaidi ya 160, mamia ya watalii hawajulikani walipo
Mamia ya watu hawajulikani walipo baada ya mafuriko Nepal, baadhi ni wakimbizi
Muhtasari
Waziri Mkuu wa Qatar anatarajiwa kuzuru Iran hii leo
Moja kwa moja
Na Beldeen Waliaula
Iran yaishtumu Marekani kwa kujaribu kuzuia mazungumzo yao na Oman
Chanzo cha picha, Getty Images
Jeshi la Iran IRGC,
limeishtumu Marekani kwa kile wamekitaja ‘kujaribu kuzuia’ makubaliano kati ya
Iran na Oman, kuhusu usimamizi wa Mlango Bahari wa Hormuz.
Jeshi hilo limesema
wamefikia makubaliano na Oman, ya kugawana mapato watakayokusanya katika
usimamizi wao wa Pamoja wa Mlango wa Hormuz,ila Marekani inajaribu kuzuia
kukamilika kwa makubaliano hayo.
Tehran
na Muscat zimejadili kuanzishwa kwa njia nyingingine ya bahari na mfumo
utakaoendesha safari za meli katika Mlango wa Hormuz.
Aidha, Tehran imeonya kuwa njia hiyo ya bahari haitafunguliwa tena hadi Marekani
isitishe vita.
Mazungumzo kati ya Iran na Oman, yanajiri
baada ya Washington kutangaza vikwazo vipya vinavyolenga kuilemaza Iran kiuchumi.
Mafuriko Nepal na Tibet yaua zaidi ya 160, mamia ya watalii hawajulikani walipo
Chanzo cha picha, Reuters
Zaidi ya watu 160 wamefariki nchini Nepal, huku mamia ya watalii wakiwa hawajulikani walipo baada ya mafuriko makubwa ya ghafla na maporomoko ya udongo katika eneo la mpaka kati ya Nepal na Tibet.
Nchini China, idadi ya watu ambao hawajulikani walipo baada ya maporomoko ya udongo katika kaunti ya Gyirong, Tibet, imefikia 558, kwa mujibu wa shirika la utangazaji la serikali CCTV.
Kati yao, 260 ni raia wa kigeni. Idadi ya waliofariki imeendelea kuwa watatu.
Mpaka wa Gyirong ni njia kuu inayotumiwa na watalii na magari kusafiri kati ya China na Nepal.
Nepal awali ilisema watu 579 hawajulikani walipo, wakiwemo raia 466 wa kigeni. Haijafahamika mara moja iwapo baadhi ya watu hao wamehesabiwa mara mbili katika takwimu za nchi hizo mbili.
Jeshi la Nepal limetuma wanajeshi 2,000 kushiriki katika shughuli za utafutaji na uokoaji kwa njia ya ardhini na angani katika maeneo yaliyoathiriwa na mafuriko.
Msemaji wa jeshi, Brigedia Jenerali Rajaram Basnet, ameiambia BBC kuwa wanajeshi hao wamejikita katika maeneo yaliyoathirika zaidi, yakiwemo wilaya za Rasuwa na Nuwakot.
Jeshi hadi sasa limefanikiwa kuwaokoa watu 97 waliokuwa wamekwama kwenye mafuriko. Watatu kati yao walikuwa wafanyakazi waliokwama katika handaki la mradi wa kuzalisha umeme wa maji wa Trishuli A.
Polisi na kikosi cha polisi wenye silaha cha Nepal pia vimepeleka maafisa katika maeneo yaliyoathiriwa kusaidia shughuli za utafutaji.
Awali mamlaka zilidhani kuwa huenda tetemeko la ardhi lilitangulia mafuriko hayo. Hata hivyo, Utafiti wa Jiolojia wa Marekani, USGS, sasa umesema nishati iliyosababisha mtikisiko huo ilitokana na maporomoko ya udongo, badala ya tetemeko la ardhi.
Waziri Mkuu wa Qatar kuzuru Tehran
Chanzo cha picha, Getty Images
Waziri
Mkuu wa Qatar anatarajiwa kuzuru
Tehran hii leo, katika
juhudi za kuanzisha tena
mazungumzo ya kidiplomasia, baada ya makubaliano ya kusitisha vita kati ya Iran na
Marekani kuvunjika.
Washington tayari imetangaza kuiwekea Iran
vikwazo vya kiuchumi pamoja na washirika wake wa karibu.
Qatar,
ambayo ni jirani wa Iran katika eneo la Ghuba
na pia mshirika wa Marekani, imekuwa mpatanishi wa siri kati ya pande hizo mbili zinazozozana, na ilichangia pakubwa katika kufanikisha makubaliano
ya kusitisha mapigano yaliyoafikiwa mwezi Juni.
Ziara ya
Waziri Mkuu wa Qatar, Mohammed bin Abdulrahman bin Jassim bin Jaber Al Thani, inafanyika wakati vita kati ya Iran na Marekani vinaingia mwezi wake wa sita huku kukiwa hakuna
dalili ya mafanikio yoyote ya kidiplomasia.
Marekani na Iran bado zinatofautiana
kuhusu Mlango Bahari wa Hormuz ambayo ni njia muhimu ya usafirishaji mafuta
duniani.