Moja kwa moja, Tangazo la Marekani la mashambulizi ya kiuchumi ni kukiri kushindwa kijeshi - Iran

Brigedia Jenerali Hossein Mohebibi, msemaji wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran, amesema kauli za Marekani kuhusu mashambulizi ya kiuchumi ni sawa na kukiri kwa njia isiyo ya moja kwa moja kuwa imepata pigo kubwa katika mapigano ya kijeshi.

Muhtasari

Tangazo la Marekani la mashambulizi ya kiuchumi ni kukiri kushindwa kijeshi - Iran

Ruka Video uendelee
  • xx
  • Besigye
  • .
  • xx
  • xx
  • xx
  • Lungu
  • xx
  • xx
  • d
  • s
  • a
  • Sonko
  • xx
  • xx
  • xx
  • xx
  • xx
  • Dangote
  • Lydia Wanjiku

Moja kwa moja

Na Mariam Mjahid

  1. Waziri Mkuu wa Uingereza aanza ziara yake ya kwanza nje ya nchi

    d

    Chanzo cha picha, Reuters

    Waziri Mkuu wa Uingereza, Andy Burnham, anatarajiwa kuzuru Kyiv Jumatatu ya tarehe 24 Agosti 2026, katika ziara yake ya kwanza nje ya nchi tangu alipokuwa Waziri Mkuu.

    Burnham anatarajiwa kuonyesha mshikamano wa Uingereza na Ukraine, huku akishiriki pia katika maadhimisho ya miaka 35 tangu Ukraine ilipopata uhuru.

    Pia ataongoza kwa mara ya kwanza mkutano wa Coalition of the Willing, muungano ulioanzishwa na Uingereza na Ufaransa chini ya Waziri Mkuu wa zamani, Keir Starmer.

    Burnham pia atapokea tuzo kwa niaba ya wananchi wa Uingereza, ikiwa ni kutambua mchango wa Uingereza katika kuiunga mkono Ukraine, kabla ya kushiriki katika sherehe za Siku ya Uhuru.

    Ziara hiyo inafanyika wakati mashambulizi ya Urusi nchini Ukraine yakiongezeka. Ijumaa, shambulio katika kituo cha ununuzi liliripotiwa kuua watu wasiopungua 16.

    Burnham amesema Ukraine ina uhakika na uungwaji mkono wa Uingereza.

    Wakati huo huo, Moscow imeionya Uingereza kuhusu "madhara" yanayoweza kujitokeza kutokana na matumizi ya ndege zisizo na rubani zinazotolewa na Uingereza kwa Ukraine, ambazo Kyiv imekuwa ikitumia kushambulia miundombinu ya Urusi.

  2. Tangazo la Marekani la mashambulizi ya kiuchumi ni kukiri kushindwa kijeshi - Iran

    Brigedia Jenerali Hossein Mohebibi, msemaji wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran

    Chanzo cha picha, IRNA

    Maelezo ya picha, Brigedia Jenerali Hossein Mohebibi, msemaji wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran

    Brigedia Jenerali Hossein Mohebibi, msemaji wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran, amesema kauli za Marekani kuhusu mashambulizi ya kiuchumi ni sawa na kukiri kwa njia isiyo ya moja kwa moja kuwa imepata pigo kubwa katika vita vya kijeshi.

    Akizungumza na waandishi wa habari katika mkoa wa Alborz kaskazini mwa Iran, Mohebibi amesema kama Marekani na washirika wake wangekuwa wamefanikiwa kijeshi, kusingekuwa na haja ya kuzungumzia hatua hizo za kiuchumi.

    Amesema majeshi yanayoichukia Iran yamelazimika kwa kiasi kikubwa kuondoa meli zao katika eneo hilo, huku juhudi za kufungua Mlango wa Hormuz na kudhoofisha uwezo wa Iran wa kujilinda zikishindwa.

    Kwa mujibu wa shirika la habari la Iran, IRNA, msemaji huyo amezitaka vyombo vya habari nchini humo kuwaelimisha wananchi kuhusu uhalisia wa vita na pande zinazohusika, kwa kutoa taarifa sahihi.

    Amesema vyombo vya habari havipaswi kuruhusu upande ulioshindwa kwenye vita vya kijeshi kujijenga mbele ya umma kama mshindi.

    Soma pia:

  3. Hujambo na karibu kwa matangazo ya moja kwa moja ya tarehe 24 Agosti 2026.