Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.

Bofya kuelekea tovuti kuu

Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data

Moja kwa moja, Gwiji wa muziki wa country Dolly Parton afariki dunia akiwa na miaka 80

Parton, aliyekulia katika Milima ya Smoky katika jimbo la Tennessee, atakumbukwa kwa nyimbo zake zilizokuwa zikisimulia hadithi za maisha, zikiwemo Coat of Many Colors, Jolene na I Will Always Love You.

Muhtasari

Moja kwa moja

Na Mariam mjahid

  1. Baraza la amani Gaza laonya Hamas kuhusu kuchochea vita

    Baraza linalosimamia amani eneo la Gaza, linaloongozwa na Marekani, limeionya Hamas dhidi ya kurusha tiara au ndege za karatasi, baada ya Israel kutishia kufanya mashambulizi ya kulipiza kisasi.

    “Shughuli zozote za kijeshi huko Gaza lazima zisitishwe, ikiwemo kurusha ndege za karatasi,” afisa mmoja wa Baraza la Amani, ambaye hakutaka kutajwa jina, alisema. “Tumewasilisha ujumbe huu moja kwa moja kupitia utaratibu uliopo.”

    Aliongezea kuwa “Israel nayo lazima iheshimu usitishaji mapigano.”

    Ndege za karatasi zilizorushwa kutoka Ukanda wa Gaza siku za hivi karibuni zimeongeza tena mvutano katika maeneo yanayopakana na Gaza.

    Kulingana na vyombo vya habari vya Israel, takriban ndege 10 za karatasi zimepatikana au kuzuiwa katika siku za hivi karibuni, huku Israel pia ikiripoti kurusha ndege zisizo na rubani.

    Hamas imekanusha kuhusika na urushaji wa ndege hizo za karatasi, ikisema watoto walioko Gaza ndio waliozirusha.

    Shirika la Utangazaji la Israel, Kan, lilinukuu jeshi la Israel lilolosema kuwa ndege hizo zilizopatikana hazikuwa na vilipuzi wala vitu vya kutiliwa shaka.

    Soma pia:

  2. Canada yalipiza kisasa kwa kuongeza ushuru kwa bidhaa za Marekani

    Canada imetangaza ushuru wa kulipiza kisasi wa hadi asilimia 50 dhidi ya bidhaa mbalimbali kutoka Marekani, ikiwa ni hatua ya kujibu ushuru mpya kwa bidhaa za Canada uliotangazwa na Rais Donald Trump mwishoni mwa wiki iliyopita.

    Ushuru huo wa Canada utatozwa kwa bidhaa za Marekani zenye thamani ya karibu dola bilioni 28 za Canada, sawa na dola bilioni 20 za Marekani, kuanzia bidhaa za chuma hadi samani,pamba na Samaki aina ya tuna.

    Orodha ya bidhaa za Marekani zitakazolengwa imeandaliwa ili kuendana na bidhaa za Canada ambazo zimewekewa ushuru na Marekani. Ushuru huo wa Canada utaanza kutekelezwa tarehe 8 mwezi Septemba.

    Hatua hii inajiri baadaya kuongezeka kwa mvutano wa kibiashara kati ya nchi hizo mbili, baada ya mazungumzo ya kibiashara kati ya Marekani na Canada kugonga mwamba wiki iliyopita.

    Soma pia:

  3. Tumeondoa mabomu yote ya baharini katika Mlango wa Hormuz - Trump

    Rais wa Marekani Donald Trump amesema Jeshi la Wanamaji la Marekani limeondoa na kulipua mabomu yote ya baharini katika Mlango Bahari wa Hormuz,ambayo ni njia muhimu ya majini ambayo Iran kwa kiasi kikubwa imeifunga tangu kuanza kwa vita Mashariki ya Kati.

    “Iran imearifiwa kwamba meli au boti yoyote itakayoweka mabomu mapya ya baharini itaharibiwa mara moja,” Trump alisema kupitia mtandao wake wa Truth Social.

    Iran haijatoa maoni kuhusu madai hayo.

    Kufungwa kwa Mlango huo kumesababisha kupanda kwa bei ya mafuta katika masoko ya dunia. Trump amekuwa akisema mara kwa mara kwamba Marekani inadhibiti eneo hilo, huku Iran ikifyatulia risasi meli zilizojaribu kuvuka bila idhini yake.

    Soma pia:

  4. Gwiji wa muziki wa country Dolly Parton afariki dunia akiwa na miaka 80

    Mwanamuziki mashuhuri wa muziki wa country, Dolly Parton, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 80, familia yake imetangaza kupitia mitandao yake ya kijamii.

    "Maumivu yako kwetu, si kwa Dolly," alisema mpwa wake, Brian Seaver, katika video iliyotangaza kifo chake.

    Parton, aliyekulia katika Milima ya Smoky katika jimbo la Tennessee, atakumbukwa kwa nyimbo zake zilizokuwa zikisimulia hadithi za maisha, zikiwemo Coat of Many Colors, Jolene na I Will Always Love You.

    Gwiji huyo wa muziki wa country aliuza zaidi ya rekodi milioni 100 duniani kote na aliandika zaidi ya nyimbo 3,000.

    Parton aliuchukulia uandishi wa nyimbo kwa uzito mkubwa na alijitambulisha zaidi kama mtunzi wa nyimbo.

    "Ni njia yangu ya kujieleza. Ni tiba yangu," aliwahi kusema.

    Mbali na muziki, Parton alikuwa mfanyabiashara mahiri. Ucheshi na haiba yake vilimsaidia kudumu katika tasnia ya burudani kwa zaidi ya miaka 60.

    "Dolly aliishi katika mwanga na sasa yuko mikononi mwa Yesu, bila shaka," alisema mpwa wake.

    Dolly Parton alizaliwa mwaka 1946 katika familia maskini ya wakulima iliyokuwa ikiishi katika nyumba ndogo yenye chumba kimoja kando ya Mto Little Pigeon huko Tennessee.

    Alikuwa wa nne kati ya watoto 12. Baba yake, Robert Lee Parton, alikuwa mkulima wa tumbaku na alilipa misionari kwa gunia la unga wa mahindi ili amsaidie kumleta duniani.

    Parton alisema mama yake, Avie Lee, alikuwa akiimba nyimbo za jadi mara kwa mara. Pia alipewa msukumo na shangazi yake, aliyekuwa akipiga gitaa na kutunga nyimbo.

  5. Hujambo natumai umzima karibu kwa matangazo ya moja kwa moja ya tarehe 26/08/2026.