Marekani yatangaza ushuru wa 50% kwa bidhaa kutoka Canada

Chanzo cha picha, Reuters
Marekani imetangaza ushuru wa asilimia 50 kwa baadhi ya bidhaa kutoka Canada, baada ya kushindwa kufikia makubaliano ya kibiashara.
Ushuru huo, ulioanza kutekelezwa jana usiku, itaathiri bidhaa za Canada zenye thamani ya takribani dola bilioni 20 za Marekani.
Ushuru huo mpya umeongeza mvutano kati ya Rais wa Marekani Donald Trump na Waziri Mkuu wa Canada Mark Carney, na huenda ukalemaza biashara huru kati ya mataifa hayo mawili.
Carney amesema amesitisha mazungumzo ya kibiashara na Marekani na kwamba Canada italipiza kisasi kwa kuweka ushuru wa thamani sawa, “dola kwa dola,” dhidi ya ushuru huo mpya.
“Nimeamua kusitisha mazungumzo ya kibiashara na Marekani na nimewaelekeza wajumbe wa Canada wanaoshiriki katika mazungumzo hayo kurejea Ottawa,” alisema Carney.

