Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.

Bofya kuelekea tovuti kuu

Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data

Moja kwa moja, Makubaliano ya kumaliza vita vya Iran 'yamejadiliwa kwa kiasi kikubwa' - Trump

Mpango wa kurefusha muda wa usitishaji mapigano umeripotiwa na vyombo vya Habari vya pande zote mbili lakini hakuna makubaliano rasmi yaliyofikiwa.

Muhtasari

Moja kwa moja

Na Ambia Hirsi

  1. Wanne wauawa katika wimbi la mashambulizi yaUrusi mjini Kyiv

    Watu wanne wameuawa na wengine zaidi ya 50 kujeruhiwa katika wimbi kubwa la mashambulizi ya makombora na ndege zisizo na rubani za Urusi mjini Kyiv na maeneo yanayoizunguka.

    Milipuko ilisikika mjini humo usiku wa kuamkia Jumapili.

    Meya wa Kyiv Vitali ⁠Klitschko alisema "ulikuwa usiku wa kutisha", na uharibifu uliripotiwa katika wilaya zote za mji mkuu, ikiwa ni pamoja na majengo ya makazi na shule.

    Watoto watatu ni miongoni mwa waliojeruhiwa, kazi ya uokoaji ikiendelea.

    Mashambulizi hayo yanafuatia tishio la Rais wa Urusi Vladimir Putin cha kulipiza kisasi baada ya kuishutumu Ukraine kwa kutekeleza shambulio baya kwenye bweni la wanafunzi katika mji wa Starobilsk siku ya Ijumaa ambapo watu 18 waliuawa.

    Wafanyakazi wa jumla wa vikosi vya jeshi vya Ukraine walisema walifanya shambulizi karibu na Starobilsk mashariki mwa Ukraine inayokaliwa na Urusi usiku wa kuamkia leo, lakini walishikilia kuwa walishambulia kitengo cha kijeshi cha Urusi.

    Mashambulizi ya usiku ya Urusi siku ya Jumapili yalikuja baada ya Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky kuonya kuwa kuna dalili kwamba Urusi inatayarisha "mgomo wa pamoja katika ardhi ya Ukraine".

    Alitoa mfano wa kijasusi kutoka Ukraine, Ulaya na Marekani kupendekeza Urusi inaweza kuwa na mpango wa kutumia kombora la Oreshnik, ambalo linaripotiwa kusafiri zaidi ya mara 10 ya kasi ya sauti na kwa sasa haliwezekani kulinasa.

    Bado haijathibitisha ikiwa Urusi ilitumia kombora katika shambulio lake la hivi punde.

  2. Mlango wa bahari wa Hormuz 'hautarejea' ulivyokuwa kabla ya vita - vyombo vya habari vya Iran

    Chini ya makubaliano kati ya Marekani na Iran, Mlango wa bahari wa Hormuz "hautarejea katika hali yake ya kabla ya vita" linaripoti shirika la habari la Iran la Tasnim.

    Chombo hicho cha habari kilicho na uhusiano na Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) kimekuwa kikiripoti maelezo yaliyomo kwenye makubaliano hayo na Marekani asubuhi hii, lakini Marekani haijathibitisha kuhusu maelezo ya makubaliano yoyote.

    Tasnim inaripoti kwamba mlango huo wa bahari hautarudi katika "ilivyokuwa" lakini idadi ya meli zinazopita inaweza kurudi katika viwango vya kabla ya vita ndani ya siku 30.

    Hata hivyo, inaongeza kuwa Iran "inasisitiza kutumia mamlaka yake kuhusu uamuzi huo".

    Inaongeza kuwa kizuizi cha majini cha Marekani dhidi ya meli zinazoingia na kutoka bandari za Iran lazima "kiondolewa kabisa" ndani ya siku 30.

    Maelezo zaidi:

  3. Makubaliano ya kumaliza vita vya Iran 'yamejadiliwa kwa kiasi kikubwa' - Trump

    Rais wa Marekani Donald Trump anasema makubaliano ya kumaliza vita vya Iran "yamejadiliwa kwa kiasi kikubwa" na maelezo yatatangazwa hivi karibuni.

    Katika chapisho kwenye mtandao wake wa kijamii wa Truth Socialsiku ya Jumamosi, Trump alisema makubaliano hayo yatajumuisha kufunguliwa tena kwa Mlango-Bahari wa Hormuz.

    Asubuhi ya leo, shirika la habari la Iran la Tasnim limesema kuwa Mlango wa Bahari utarejea katika viwango vya kabla ya vita ndani ya siku 30, na kuongeza kuwa makubaliano huenda yakasimamisha mashambulizi pande zote.

    Muda mfupi ujao tunatarajia tamko kutoka kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio kufuatia mkutano wake na waziri wa mambo ya nje wa India mjini New Delhi - unaweza kufuatilia moja kwa moja hapo juu pindi atakapoanza.

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Iran Esmail Baghaei aliambia televisheni ya taifa jana kuwa wawakilishi wa Marekani na Iran wamekuwa wakikutana katika wiki za hivi karibuni.

    Lakini alionya hilol haimaanishi kuwa makubaliano yatafikiwa katika masuala muhimu na kuwashutumu Wamarekani kwa kutoa "taarifa zinazokinzana".

    Trump pia alisema alikuwa na "mazungumzo mazuri" na viongozi wa Saudi Arabia, Umoja wa Falme za Kiarabu, Qatar, na wengine kuhusu "Mkataba wa Maelewano unaohusu AMANI".

    Maelezo zaidi:

  4. Karibu kwa matangazo ya moja kwa moja.